Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Ulikuta kitu gani kwa Watu ukajua "hapa pesa ipo"?

Mimi Kuna dogo alikuja kwetu, tukampa makande baada ya kula mtoto akaanza kulalamika ameshiba sana, hapumui vizuri...alivyokuja mama yake akapelekwa Agakhan just for check up....kumbe kwao hawakitambui kama chakula Cha binadamu 🤣🤣🤣
Makande ni CHAKULA Cha wanyama walio shindikana marekani na ulaya nafaka ya makande mchanganyiko wa mahindi ,maharage,njugu mawe E.t.c

Ni kwa ajili ya nguruwe,simbilisi, na wanyama wengine wengine.

🤣🤣😅😅🤣☺️😊
 
HIlivi mnajua kuna nyumba ni kosa la jinai watu kunywa MTINDI

Nyie si mnaambiwa na MADAKTARI mtindi mzuri una faida kiafya

Kuna nyumba maziwa ya mtindi yanaitwa UCHAFU nyie kuna dharau chini ya hili jua kwenye nyumba za watu acheni kabisa.
 
HIlivi mnajua kuna nyumba ni kosa la jinai watu kunywa MTINDI

Nyie si mnaambiwa na MADAKTARI mtindi mzuri una faida kiafya

Kuna nyumba maziwa ya mtindi yanaitwa UCHAFU nyie kuna dharau chini ya hili jua kwenye nyumba za watu acheni kabisa.
 
Kuna madogo wa kihaya nilisoma nao sekondari kwao walizaliwa mapacha wawili wa kike na wawili wa kiume walikuwa wanaishi katika nyumba mbili. Walikuwa na nyumba Mbezi beach apartment Upanga. Wazee wao wakibanwa na kazi wanalala upanga na dereva anatumwa kuwafuata mbezi beach na kuwaleta Upanga. Maana wazee wao walikuwa hawawaruhusu kulala kwenye nyumba peke yao.

Kuna mkuu wa chuo mstaafu wa Mlimani ni mhaya (wajanja watajua code )ana nyumba kubwa hapo makongo. Mke wake amewapa tenda wauza mboga za majano wanaolima mboga katika mto survey na Goba. Wanamletea mboga za majani na anawalisha kuku wake wa kienyeji mbele ya macho yao na yangu nilishuhudia. Huyu mkuu wa chuo amejenga ghorofa pembeni ya nyumba yake kama nyumba ya kupokea wageni. Na cha kuongezea nyumbani kwake amefungiwa transformer special ukipita barabarani unaiona kabisa imejengewa na footing ya zege.

Kuna mzee mmoja ni marehemu alikuwa jaji. Nilienda kwake kwa ajili ya shughuli zangu nikakuta mbwa wamechemshiwa utumbo mzima wa ngombe. Na pembeni walikuwa wamepikiwa wali wa karoti mwingi. Niliona vijana wakikata kata utumbo na kuchanganya na wali pamoja na mchicha kwa ajili ya kulisha mbwa. Huyu mzee alikuwa na Rottweiller walioshiba kama kumi na sita hapo sikuhesabu watoto.

Kuna Injinia mmoja makongo alinikaribisha kwake nilifika na nikakuta kila chumba ni self contained na kina fridge na tv. Huyu jamaa alikuwa na Ghorofa ya vyumba nane . Alikuwa na watoto watano, wawiili wa kiume. Kila mtoto wa kiume alikuwa na chumba chake. Dada mkubwa alikuwa na chumba chake na wadogo zake na chumba chao. Kimoja cha dada wa kazi na cha mwisho kilikuwa cha kupokea wageni. Na hapo alikuwa na sebule ya juu na chini. Nyumba ya huyu jamaa ilini inspire sana hasa katika kazi zangu za ujenzi. Huyu mzee hakuteseka kujenga maana material nyingi alikuwa anachukua kwenye kampuni yake ya ujenzi anapokuwa na miradi.

Kuna injinia mmoja nilimtembelea nyumbani kwake Mbezi beach nilshangaa kuona ana chumba maalumu ya kunyolea ina kiti cha saluni kabisa na anamwita kinyozi kila jumapili amweke sawa. Pia huyu jamaa alikuwa na kaunta kubwa sana imesheheni kila kinywaji. Kila miezi michache alikuwa anatualika tuzimalizie bia zisije kuharibika. Ana ndugu yake ana biashara ya kusambaza vinywaji alikuwa ameeka oder ya kila baada ya muda fulani kumuungisha katika biashara yake.
 
Nilikua naendesha gari ya mizigo nikapata kazi kupeleka mavyuma fulani hivi mbweni, sikwenda na mtu ila nilipewa namba ya simu nikaambiwa ukifika maeneo fulani piga simu kuna mtu atakufuata.

Mie huyoooo nilipofika eneo la tukio nikapiga simu full kufoka nimeshafika muda mrefu hapa, dk 0 ikaja V8 nyeusi tiiii. Ikaja kuni block kwa pembeni, jamaa akashusha kioo akasema nifuate.

Asee kila kona tunayokunja ni mijengo ya maana, mitaa mizuriii halafu pako kimyaaa, tukafika mpaka nje ya mjengo mmoja geti kuubwa, lile lango likafunguliwa kwa rimoti tukazama ndani.

Asee ile kuingia ndani nikawa nashangaa shangaa tu hata sielewi, lilikua bonge la jumba, swimming za maana halafu juu ya paa kuna parking ya helicopter, mataa ya barabarani yapo ndani.

Kuna jamaa nahisi aliona shauku yangu, akaniambia "zunguka zunguka uone nyumba ya rais wako ili uende ukasimulie na wenzio" nilizunguka kidogo tu ila maeneo mengi yalikua na makatazo kupita.(nyumba ilikua haijaisha ila ilikua inatisha aseee)

Nb; ninaposema rais, anaweza akawa wa tff, wa yanga au hata wa chuo.
Hata raisi wa fm academia
 
Back
Top Bottom