Ulikuwa na ndoto za kuwa nani utakapokuwa mkubwa? Umeiishi ndoto yako au maisha yamekupeleka kwingine?

Ulikuwa na ndoto za kuwa nani utakapokuwa mkubwa? Umeiishi ndoto yako au maisha yamekupeleka kwingine?

Kwakuwa nimezaliwa kijijini na kusoma shule ya msingi kijijini,

Ndoto yangu ilikuwa kuwa mwalimu wa shule ya msingi,kwani walimu ndiyo waliokuwa wanaongoza kuwa na maisha mazuri kijijini kwetu miaka ile,ni ndoto niliishi karibu miaka sita.

Upepo ukabadilika baada ya kuanza sekondari mjini mpaka leo sijui nilifikaje huku,ila Mungu ni mwema
 
Nikiwa, darasa la saba, siku ya mtoto wa, Afrika, sherehe ilifanyika UDSM, Nkrumah, nilivutiwa na nikasema, lqzima nifike chuo, nikiwa, form one, nikasema, lazima niwe engineer, nilipokuwa chuo, nikasema, nataka kuwa engineer lakini ndani ya, jwtz!
Siku, nimeenda kufatilia nafasi, pale jkt karibu na kawe, kwanza mapokezi, wakaniuliza, kabila langu! Nikawauliza kabila LA nini? Wakasema litanisaidia, kupata, kazi, kiurahisi,nikapiga chini, nimejaribu Mara nne nafasi ya jeshi, natoswa!
Nikarudi, chuo, ongeza, elimu, niwe muhandisi, nafurahi nimefanikiwa kuwa muhandisi,
Ila bongo fulsa ni chache,kuna watu wana uwezo, makubwa, lakini hawa patients nafasi
 
Kipindi nipo mdogo enzi za shule ya msingi nilitamani kuwa msanii mkubwa sana hapo baadae hadi nlipofika sekondari nilikuw wa moto kwenye kuimba HIP HOP kwa sana mashindano shule shule kitaani nakimbiza kinoma kudance ndo usiseme nawakalisha kwenye Matamasha

Basi bwan nikawa najiona bonge la msanii had kutungia washikaji mashairi[emoji1787][emoji1787]
Kilichofata sasa wazazi wakanikomalia nipige pindi nitoboe mpaka chuo.

Basi nikajikita Kwenye Masomo zaidi mwisho wa siku ndoto ya kuwa msanii mkubwa ishayeyuka nimekua shabiki [emoji1787][emoji1787]
 
Moja ya ndoto yangu ilikuwa ni kuwa mmoja wa Wanazuoni na wakufunzi wa Chuo Kikuu upande wa "Molecular Biology". Nilikuwa natamani na naota niwe Professor wa "Molecular Biology" ila ndio hivyo nimeangukia kwenye kazi nyingine.

Kiukweli, nikiona Maprof au wakufunzi wa vyuo vikuu huwa naumia sana na kuingiwa na uchungu moyoni. Kuna kipindi huwa nikikaa peke yangu pamoja na umri wangu wa 40's huwa nalia tokana na uchungu ila haya yote ni maisha.
 
Back
Top Bottom