Ulikuwa na ndoto za kuwa nani utakapokuwa mkubwa? Umeiishi ndoto yako au maisha yamekupeleka kwingine?

Ulikuwa na ndoto za kuwa nani utakapokuwa mkubwa? Umeiishi ndoto yako au maisha yamekupeleka kwingine?

Moja ya ndoto yangu ilikuwa ni kuwa mmoja wa Wanazuoni na wakufunzi wa Chuo Kikuu upande wa "Molecular Biology". Nilikuwa natamani na naota niwe Professor wa "Molecular Biology" ila ndio hivyo nimeangukia kwenye kazi nyingine.

Kiukweli, nikiona Maprof au wakufunzi wa vyuo vikuu huwa naumia sana na kuingiwa na uchungu moyoni. Kuna kipindi huwa nikikaa peke yangu pamoja na umri wangu wa 40's huwa nalia tokana na uchungu ila haya yote ni maisha.
Unapenda ualimu eh?
 
Nmefurah tu mkuu ndoto ya kibabe sana
Boksi oyeee 😉

IMG_6111.jpeg
 
.......nilipokuwa mdogo nilipenda kuwa kiongozi serikalini especially mbunge, nilipofika sekondari nikagundua ni ngumu sana Mimi kuwa mbunge, nikaanza kudevelop interest kwenye mambo ya fedha, ishu za uchumi na uhasibu, hadi nikaanza kusoma egm, ikanipiga knock out mbaya sana, basi ikabidi niwe mpambanaji wa hapa na pale hadi leo hii, sio mbaya mkono unaenda kinywani ingawa ni kibishi sana......
 
Napenda kufundisha, napenda kusimama mbele za watu kuongea kwa ujasiri na kuaminiwa na watu. Nilikuwa na uwezo wa kuwa Prof, IQ yangu ilikuwa kubwa sana tola nikowa mdogo. Maisha tu haya mbeba mabox wetu.
Nahisi kama vile unaipenda title ya ‘professor’…
 
Nilikuwa natamani kuwa mwandishi wa habari lakini Bado naipigania hii ndoto maana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shikilia hapo hapo Mkuu, kama unakwama usisite kuomba msaada kwa waliokutangulia, na hata humu JF unaweza kupata muongozo toka kwa manguli kama Pascal Mayalla pamoja na kutumia JF kama JF kunoa uwezo wako
 
Dereva wa zile semi. Ndoto ilikufa form 3 nikaanza kujiandaa kuwa daktari bahati mbaya physics ikawa inanisnitch.
Physics ikakufanya vibaya😀😀... sio mbaya tushikilie kwengine tulipojipata
 
Nikiwa, darasa la saba, siku ya mtoto wa, Afrika, sherehe ilifanyika UDSM, Nkrumah, nilivutiwa na nikasema, lqzima nifike chuo, nikiwa, form one, nikasema, lazima niwe engineer, nilipokuwa chuo, nikasema, nataka kuwa engineer lakini ndani ya, jwtz!
Siku, nimeenda kufatilia nafasi, pale jkt karibu na kawe, kwanza mapokezi, wakaniuliza, kabila langu! Nikawauliza kabila LA nini? Wakasema litanisaidia, kupata, kazi, kiurahisi,nikapiga chini, nimejaribu Mara nne nafasi ya jeshi, natoswa!
Nikarudi, chuo, ongeza, elimu, niwe muhandisi, nafurahi nimefanikiwa kuwa muhandisi,
Ila bongo fulsa ni chache,kuna watu wana uwezo, makubwa, lakini hawa patients nafasi
Hongera kwa kutokukata tamaa na kufikia ndoto yako japo siyo kule ulikusudia kabisa lakini 90% umefanikiwa.... hiko kipande cha kabila hapo, mbona wanafanya kama ka ubaguzi fulani hivi? Kwamba kuna baadhi wanakuwa wazembe sababu tu ni kabila fulani?
 
Nilitamani kuwa Lawyer, Sababu Babu alikua ananipa vitabu vyake na kesi nyingi nyingi nilizipenda sana kusoma, akawa ananiambia nimsindikize hadi mahakamani 🤣 🤣 Mwisho wa siku nimeangukia kwenye makalai🤣🤣
Bado unaweza kufikia huko Mkuu usikate tamaa. Pascal Mayalla aje akupe chachu ya kukamilisha hilo😀😀
 
Nilitamani sana kuwa mwanajeshi, sijakata tamaa bado umri unaruhusu.
 
Back
Top Bottom