Ulikuwa na ndoto za kuwa nani utakapokuwa mkubwa? Umeiishi ndoto yako au maisha yamekupeleka kwingine?

Nilikuwa na ndoto ya kuwa mwanajeshi wa wagner group ila nilifanikiwa kushiriki vita ya ukraine
 
Mbona hata ubuyu uuletao hapa ni uandishi wa habari pia. πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜„πŸ˜πŸ˜†
Anajinoa hapa ila hajawa serious tu, kuna shindano la Stories of Change anaweza kushiriki pia akatoa mawe hawezi jua nani anasoma akatoboa au akaibuka moja ya mshindi ndio akachomokea hapo, kuna wakati pia Mkuu Maxence Melo aliwahi kusema kwenye interview kama mara mbili hivi kama sijakosea (kwa nyakati tofauti) kuwa JF inawalipa watu wanaoandika maudhui/content zenye tija humu, achangamkie fursa... anaweza kutoboa kupitia humu humu JF
 
Not in such a way, ni kwamba iwe taaluma rasmi.
Umenichekesha.
Kuna watu wa kukupa muongozo humu humu Mkuu watumie hao kupiga hatua, kuna shindano la stories of change tumia fursa likianza, unaweza hata kuanza kuandika makala zenye tija hapa hapa-mambo ambayo yanagusa jamii na kupitia wewe yanaweza kupatiwa ufumbuzi, sehemu unayoishi kuna changamoto gani kwa mfano? Anza kutumia hizo hizo kama sehemu ya kujinoa na kama stepping stone kuelekea kutimiza ndoto yako. Mambo ambayo tunaona ni madogo na hayana maana yanaweza kuleta impact kubwa kwenye safari yako.
 
As long as bado unapumua Mkuu hakuna kinachoshindikana, miaka 40+ sio mwisho usikate tamaa
 
Namshukuru Mungu nina mwalimu bora kabisa anayeijua taaluma hiyo vyema, Asante.
 
Randomly,sijawahi kuchagua wala kutamani nafasi ya mtu mimi niliacha hali iende inavyotaka litakakowakia huko huko nasonga namshukuru Mungu kwa nilipo.

Wala simshauri mtu aanze kuishi ndoto zisizowezekana huko ni kujichosha akili na mwili hizo waachie wanaokuta tayari kuna watu walishatengeneza njia ya mafanikio kama wewe maskini kuna namna asili huamua ukapata kinachokustahili.
 
Hata sijui nilitamani nini na sasa nipo kwny kitu naona kinanifaa maisha ni vyenye Mungu umeshakuchorea kwa mkono wake..ukiona unaenda mule mule jua basi ndo kusudio lake...ukiona unapigwa ngwara na kuibukia kwingine ujue ndo huko wapaswa kua so urelaaaxx na kufanya
 
Hakuna kitu kilikua kinanukwaza kama nikiota nakojoa, then nikiamka asubuhi nakuta nimelimwaga kweli....🀣
Sasa mawazo yalikua yananipata nikitoka nje nitaimbiwa ile kikojoozi...eehhh....
Ama hapa mnaseme ndoto zipi kwani mkuu...πŸ€”πŸ™„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…