Ulikuwa na umri gani ulipotengeneza milioni yako ya kwanza?

Nyafwili

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2023
Posts
4,240
Reaction score
10,561
• Habari wana JamiiForums na wafanyabiashara wenzangu, nataka nitengeneze milioni yangu ya kwanza mapema mwaka huu. Hata hivyo, Maana nimekuwa kila nikitafuta hela nashindwa kufikisha million , nataka kujua ni umri gani nyie mlitengeneza milioni ya kwanza na jinsi mlivyofanya au uwekezaji mliofanya mpaka mkapata hiyo million.

• Ndiyo! uchumi si wa kutabasamu kwa sasa, Lakini hii inaweza tumika kama motisha kwa ndugu, jamaa na marafiki, ambao bado wapo kwenye ajira ndogo ndogo na Wanataka kujiajiri au wapo kwenye hatua ya kudunduliza mitaji.

• Tuambie ni lini ulitengeneza milioni yako ya kwanza na kwa njia gani?

Your browser is not able to display this video.
 
Iko poa hii mkuu, ulifanyaje mpaka ukavuna milioni 8-9 ukiwa upo chuo, kuna biashara yeyote ulikuwa unafanya?
 
27 July 2022 Ndio milioni yangu ya kwanza kutimia, na mpaka leo niko nayo imeongezeka mana naiwekaiweka kuna jambo la kufanya mwaka huu 😎
Hongera sana mkuu, hiyo million yako ya kwanza, umeiweka Bank,?, kwenye kibubu au ipo kwenye mzunguko,. Tuambie ratiba yako niipi kwenye hiyo million.
 
Iko poa hii mkuu, ulifanyaje mpaka ukavuna milioni 8-9 ukiwa upo chuo, kuna biashara yeyote ulikuwa unafanya?
Nilikuwa nafanya forex miaka ile na broker templer halafu nilitemana nayo kabisa ,pia nilikuwa nafundisha watu nikila kipigo sokoni nahost event naleta kelele nyingi nakula sitting allowance ...Baadae niliona biashara ya kiduanzi unajiexpose sana kama umefanikiwa nikatemana nayo.

Nina rafiki yangu mpaka leo afanya hana lolote kazi kukodi magari anakaa sinza huko ,ila alishapiga mpaka million 100 ...Ujinga bata kwa sana na wanawake kutwa yupo Zanzibar ...Ana nyumba lakini huko Mbweni.
 
Wewe umri wako mbona hujataja?
 
• Ulijitahidi sana mkuu, maana naskia walio ingia forex, kwa sasa ni mafukara wakutupwa,

• Mkuu unatushauri nini sisi ambao hatujafikisha milioni ? Wapi tujirekebishe?
 
55
 
• Zuri hii sana hii mkuu, Je bado unaendelea na ufugaji wa kuku? Na walikuwa wa kienyeji au kisasa.

• Ipi changamoto uliipata wakati wa ufugaji wa kuku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…