macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Mimi nadhani ni dhamira kuu ni kutisha wananchi na kuwateka kimawazo ili waone taasisi ya urais ni kama ukuu ambao una nguvu kuu na hauchezewi. Tuna tuna watawala na siyo viongozi, na ni kawaida sana kwa watawala kutaka kujionyesha ni watu wenye uwezo na mamlaka kuu!Hapo uwanja wa ndege kulikuwa na umati mkubwa?
Watu wasio na upeo wakiona picha na video kama hizi hutishika na kumwona rais kama mungu mdogo asiyehojiwa bali anatakiwa kuogopwa. Nasema hivi kwa sababu kwa hali ya kawaida kama kuna adui anayetaka kumdhuru hilo la kushika bunduki kama wapo tayari kufyatua halisadii chochote bali linatoa mwanya wa kuwashambulia!