Ulioa au kuolewa ukiwa na umri gani?

Ulioa au kuolewa ukiwa na umri gani?

Watu wote JF wameoa na kuolewa Uzur watu wa JF wanaendana na Uzi wako unavotaka, ukileta Uzi wa utajir watu wote JF n matajir ukirud kweny ndiga humu wote wana ndinga

Yan thread inavoenda ndo watu wanaend nayo ivo ivo [emoji23]
 
Kukutana kwa Mara ya kwanza 2011…tukiwa chuo kikuu kimojawapo Moro town. Ndoa 2015 October. Miaka 27 & 26 respectively! Mwaka huu tunafunga 8 years strong with 2 kids along the way, God is good!
Bigup safii

Marriage is good.
 
28 yrz wife 25 tupo mwaka wa kumi with 3 kids,tuna jumla ya miaka 18 ya kimahusiano.humo mna miaka ya uvulana na usichana na miaka ya mahusiano serious kisha kumi ya ndoa na familia,namshukuru Mungu kwa hili.

Juzi weekend nilikuwa namtania wife namwambia tumeshatoboa sisi ni wa kufa na kuzikana alifurahi sana maana yeye ndiye aliyetengeneza mazingira ya ndoa sikuwa tayari wakati huo but leo (japo sijawahi kumwambia na sitakaa nimwambie kwa sababu zangu binafsi) namshukuru kama siyo yeye kuna vitu naona kabisa nisingekuwa navyo.

Vijana oeni,maisha ni haya haya kila mtu ameandikiwa kikombe chake cha mwenzako hutakinywa na yeye chako hatakinywa msi-copy matukio ya ndoa mkayafananisha huko ni kudanganyana.
Inapendeza sana
 
Kweli ni hekaheka tupu ila ni hekaheka zaidi ukioa/kuolewa na vijana wa karne ya sasa, utaona kila rangi, ambao wameoa au kuolewa siyo kwamba kuna kitu wanafaidi ni vile tu mmoja amekubali yaishe na awe mpumbavu ili maisha yaendelee.

Si shauri kuingia katika ndoa ukiwa hujajipanga kiakili, kiuchumi, kimwili, kiroho na kikubwa zaidi kuliko yote kisaikolojia.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
Ufafanuzi kidgo paragraph ya mwisho hiyo mkuu..!
 
Back
Top Bottom