mliverpool
JF-Expert Member
- Jan 6, 2015
- 1,565
- 2,944
Mm nilioa accidentally nikiwa na miaka 29 wife 27, tulikutana kazini mapenzi ya kazini kiutani utani,tumekutana june ndoa november hata sijui ilikuwaje ila sasa tuna miaka 6, watoto wawili nafurahia maisha,kuna muda najiuliza bila yeye sasa hivi ningekuwa wapi,nilichojifunza ktk ndoa,maishw ni hayahaya,hakuna maisha mapya mtafute mtu mmoja unayeelewana naye mjenge maisha,ni fahari sana kuwa na mwenza wako mnaepanga naye mipango ikaenda,Mke wangu amenisaidia vitu vingi sana kunifanya huyu wa leo,na nimegundua ndoa haikuzuii kutimiza ndoto zako zozote zaidizaidi inakusaidia kufika kwa haraka!!