princess ariana
JF-Expert Member
- Aug 19, 2016
- 9,245
- 18,347
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa machozi yalikutokaje sasa? Hukuona umuhimu wa kunywa bia?Siku 3 kabla ya tangazo la Kifo chake.
Nilipitishwa ktk(ulimwengu wa roho)
Nilimuona JPM akiwa na mpambe wake.
Jpm Alionekana akiwa na huzuni saana,
Kuna briefcase ya flan ya Rais yule mpambe wa Rais alimkabidhi mtu flan(Ambae alikua kivuri sikumtambua sura wala jinsia).
Shortly Nilikuja kuelewa na kukumbuka maono hy usiku ule baada ya tangazo la msiba.
Taarfa za msiba.
Nilikua nimelala wakaja madogo,(walienda kucheki mechi bandani)
Wanaongea kwa sauti ya juu mpk nikashtuka nikaamka.
Ile kufungua mlango nikaskia "Jamani Magufuli kafariki"
Nikamuuliza we umejuaj?
Akaanza kuelezea.
"Si tulikua tunaangalia mpira ghagla akasimama juu muhuni mmoja, akasema kwa sauti kubwa...JAMAAAANI EEEH TAYARI!!!...wakasema kaachini acha ujinga,tyr nini..
Aksema TAYARI MAGU KAVUTA..
KAMA HAMUAMINI WEKENI TBC 1..
Ikawekwa tukamwona Samia Anahutubia kwa huzuni"
Hatujaendelea na mpra wote tumetawanyika"
Aisee tukawasha tv na redio tukakuta nyimbo za misiba zinapigwa .
Nilichoooka nilisikitika niliporudi kitandani ndo nikakumbuka siku 3 nyuma yale maono niliyoyaona kumbee yalikua na maana hyo.
Nilitokwa machooozi.
Ulikosea kuwapenda wote,huyo demu na huyu mwamba,Daah kabla ya tarehe 17 tarehe 9 majaliwa anaenda njombe tarehe 12samia ana ziara tanga siku tatu kabla ya hizo tarehe malaika alikua akizungumza na mimi katika roho.
Nilimuota magufuli mara tatu ni baaada ya kuhutubia mbezi pale alinionyesha mungu magufuli amekufa nilipatwa na roho ya kuomba na kujinyenyekeza mbele za bwana kitu ninacho amini magufuli alikufa tarehe 8 mwezi wa tatu.
Nilimpenda huyu mtu kwa mara ya kwanza namuona magufuli nilikua nampelekea demu wangu zawadi katika siku yake ya kuzaliwa alikua anasoma baobab girls bahati mbaya siku ile ilinyesha mvua daraja la ruvu chini lilikatika mawasiliano ya barabara kutoka msata kuja dar kupitia bagamoyo road hayakuwa yanapitika.
ndipo mwamba alipofika na kurekebisha hali nikamuona niliwaza moyoni huyu anafaa kuwa raisi wa nchi na kweli ikawa nilimpenda sana huyu mwamba toka moyoni sijipiga kura tena nilianza kwake utamadun wa kupiga kura na umeishia kwake kibaya na kinachoniuma demu niliyempenda kaniacha na mwamba amelala milele ninamaumivu two side ni hayo
NothingBinafsi niliumia sana siku hiyo hakuna wimbo uliokuwa ukiniumiza kila nikiusikia kama ule wa Msechu- UMETUACHA salama. Taarifa za kifo nilizipata mida ya saa sita usiku nikiwa kwenye basi la fikoshi Iringa to Mwanza. Jamaa alikuwa mwamba!!!
Utakuwa ulifaidi utawala wakeMimi nikiri sikuwa sawa tangu tetesi za kuumwa kwake nlikuwa naomba Sana kimoyo moyo isiwe kweli yaani.badi bhana siku yenyewe nilikuwa nimetoka kazini ile nalumzika kidogo baada ya kuoga kabla ya Kula nikapitia pitia jf Kwanza ili nilale, ile naenda bafuni kirudi wife ananiambia angalia itv huku analia aisee...kwa mara ya Kwanza nikaonja uchungu wa msiba tangu nizaliwe inauma Kama nini.nilikaa Kama siku mbili sielewi elewi mpaka sasa bado kwa mbali sielewi Mimi.
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
SawaSIKU hiyo nilichelewa kulala nikawa busy nacheki movie, baadae nikasema goja niingie online kidg ndipo mfanyakazi mwenzangu Kwenye group ikaingia sms kasema pumzika mwamba kisha kaweka emoji za kulia nikshtuka nikampigia akanambia Magufuli kafa [emoji24][emoji24][emoji24] sikuamini asee.
Nililia siku mzee anaagwa Mwanza baada ya clip moja kuiona anasaidia mama kipofu kule Mara nililia sana.
RIP. mzee
SawaTaarifa za kifo chake nilizipata trh 9 kutoka kwa mtu ambae hawezi kudanganya ila nikajua uzushi tu.
Tetesi zikaendelea mitandaoni, sasa siku ya trh 17 saa 11 alfajiri nilikosa usingizi nikaingia jf nikakuta mtu kaweka uzi akisema " si watangaze tu raisi wa nchi yupo kwenye fridge wiki nzima si watangaze"
Yesuuuu, moyo ulidunda mbio nikatoka kitanda nikashika biblia sikuifungua nikapiga magoti nikasema Mungu nakuomba hiki nikachokihisi nikilinganisha na tetesi za mitandaoni mungu naomba isiwe ni kweli.
Yaani nilihisi naumivu ila nikajisemea hapana hizi hisia mbaya nikajiandaa nikaenda kazini.
Nikiwa ofisin kuna kijana mmoja kaingia akicheka kweli akasema "jiwe lazima lidondoke" nilimjibu magufuli hafi leo tukaishia hapo.
Nyumbani nilifika saa 3 nikajilaza kwenye sofa nikapitiwa usingizi, sasa nikiona simu ya mama inaita najua ni saa 4 usiku, nikampokea usingizini tukasalimiana mwisho akaniambia eti " dada nimesikia jpm kafa? Nikasema mama hao waongo.
Nilienda chumbani nikalala mida kama ya saa 6 kasoro naona shoga yangu wa moro ananipigia, bila hata salama nikasikia, " wewe unalala hovyo wakati raisi kafa? Yesuuuuuuu, usingizi ukikata nikamjibu, wewe ni uzushi uko mitandaoni, akasema washa tv samia anatangaza.
Fasta nikaingia insta nikakuta samata kapost yesuuuuu nilipiga kelele, na ninavyoishi mwenyewe, nikaanza kupigia watu nikiuliza.
Nikaona haitoshi, kuna ndugu yake jpm namjua nikampigia alivyopokea simu kwa muda ule nilijua tiyari, nilibaki tu napiga ukunga, kila ninaempigia yupo hewani watu wanalia aiseee.
Nakili magufuli nilikuwa namkubali kawaida tu ila sijui baada ya kusikia kifo chake yale maumivu yalitoka wapi yaan utadhani mimi ndugu yake. Nililia sana.
Kuna fala mmoja akanipigia najua hampendaji jpm, nikapokea nikasikia kicheko nikakata simu nikamblock. Siku mbili baadae akanitafuta kwa no nyingine nilimchamba hakuamini. Akinipigia siku hizi lazima awe na adabu sina hasara hata asipokuwa rafiki yangu.
Magufuli ulijua kuniumiza jamani.
RIP JPM.
Acha kufokea watu sio wote walimpendaFunga domo lako usinisababishie nafungiwa jf, funga bakuli lako hujui watu tumeumia kiasi gani.
Mimi ni mtu wa kawaida kuna watu humu tunajuana face to face. We mjinga ungekuwa karibu yangu ningekudunda mbaya kwa hasira nilizo nazo.
Mamilion wanalia kwa ajili ya jpm wewe unaongea ujinga, hivi unajua jpm alikuwa muhimu kiasi gani?
Unajua nini maana ya uongozi wewe?
Akili kisoda wewe.
Mimi mmoja wapo nilimpenda mno,nilitamani hata utokee muujiza aamke.Kwa waliompenda walimpenda kweli kweli na kwa waliomchukia walimchukia kwelikweli, kwahiyo inategemeana upo upande gani.
Kabla hujaniambia nafoka soma comments za niliemjibu anavyonitukana, umesoma alichokiandika?Acha kufokea watu sio wote walimpenda
🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌🙌 Potelea mbali we elezea tu mambo yasiwe mengi mzee alikuwa katili sana yule.Nikielezea yangu naweza onekana mdogo wake shetani bure.
Kwanza tangu nione Kigogo anaongelea hilo twitter, nilianza kuwa mtazamaji mzuri wa TBC.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119] Potelea mbali we elezea tu mambo yasiwe mengi mzee alikuwa katili sana yule.
wenye akili ni jiwe basiWewe huna akili
i dont blame you , i blame your low IQHiki kiswahili cha wapi