Ulipokwenda ugenini, tabia gani za watoto zilikushangaza?

Ulipokwenda ugenini, tabia gani za watoto zilikushangaza?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Nipo Ugenini huku Mikoa ya Kaskazini, nimekuta kwenye hii familia watoto wana tabia ambayo imenishangaza sana na wazazi wanachukulia poa tu,

Jana tulikwenda sehemu wakanitembeze nione miazingira wakati tunataka kwenda watoto walitaka kwenda nasi, wazazi wakasema wababi wafanye kazi za shule wao watawatoa siku za weekend, watoto hawakuridhia wakabaki wanalia japo kiumri wanaonekana si wa kulia kwa kuachwa.

Kasheshe lilianza tuliporudi, Watoto wakagoma kufungua mlango wa nyuma wanasema tulale nje kwa kuwa tuliwaacha, geti tulifungua kwa funguo ambayo baba mwenye nyumba alikuwa nayo ila ya ndani ndiyo hana, tulikaa nje zaidi ya saa moja na nusu wazazi wakibembeleza watoto wafungune na watoto wanasema hawafungui mpaka Mama akaanza kumwambia mumewe wampigie fundi wavunje.

Baadae Dada wa kazi akarudi ambaye alikuwa kaenda kusuka akawaambia anawaomba wamfungulie ndipo walipofungua na sisi tukaingia.

Cha ajabu wazazi wakasema mnajua kujifungia ndani sio jambo zuri mtakuja kupata madhara, kwanza mmeoga, hebu nendeni muoge mje tule na kesi ikawa imeishia hapo.
 
Watoto wa kibongo hasa wale wa familia za kati wana tabia ya kuvizia chakula cha mgeni, mtoto anaacha chakula chake anakuja kukaa mbele yako wewe mgeni anakukodolea macho mpaka unalazimika kula naye tu.
 
Kuna nyumba nilienda watoto wale walinishangaza sana, imagine mtoto anaangalia katuni mtu mzima ukiingia anatoa katuni na kuweka channel ya kawaida na remote anaweka mezani. Nilibaki mdomo wazi 😁😁
 
Mimi kwa sasa nimeamua kulea na kukemea wa kwangu tu maana ukijifanya kukemea unaonekana una kiherehere.Ila ki ujumla kuna wazazi wanalea watoto kimama mama sana ww unaenda sehem mtoto hajui hata kusalimia tu.
Kwa hiyo mtoto wako atajioa ? Si atakuja kuoa na utapata mkwe asiye na staha kama usipochukua hatua sasa hivi?
It takes a village to raise a child!
 
Back
Top Bottom