Ulipokwenda ugenini, tabia gani za watoto zilikushangaza?

Ulipokwenda ugenini, tabia gani za watoto zilikushangaza?

Kuna nyumba nilienda watoto wale walinishangaza sana, imagine mtoto anaangalia katuni mtu mzima ukiingia anatoa katuni na kuweka channel ya kawaida na remote anaweka mezani. Nilibaki mdomo wazi 😁😁
Ndiyo maana kwangu nilipiga vita TV kuwa Sebuleni. Naamini mgeni anakuja nyumbani kwangu kwa mazungumzo si kutizama TV
 
Huo ujinga sio wa kuuchekea yaani nyumba yangu halafu jitu linifungie kwa nje? Hapana rangi wangeacha kuona

Nilienda kwenye nyumba moja huko mbezi beach kwa washua watoto wakitoka shule wanatupa tu mabegi sebuleni wanawasha TV na kuanza kuangalia tamthilia ikifika saa mbili wanaoga wanakula na kulala, ile wanaamka asubuhi ndio wanakumbuka kumbe walipewa homework wanaanza kujiliza hapo wasaidiwe ndio waje kukugongea mlango chumbani anko anko mama amesema utusaidie homework, nikavumilia siku ya kwanza mpaka wiki inaishia nikawatolea uvivu siku hiyo nilitaka kuangalia taarifa ya habari muhimu wanang'ang'ania rimoti nilichukua stiki walichezea mbele ya mama yao, nikawaamrisha kuchukua daftari na kufanya homework kuanzia siku hiyo huo ujinga haukuwepo hata wakitaka kuangalia tamthilia wanakuja kuomba ruhusa kwangu baba na mama wapo
 
Nipo Ugenini huku Mikoa ya Kaskazini, nimekuta kwenye hii familia watoto wana tabia ambayo imenishangaza sana na wazazi wanachukulia poa tu,

Jana tulikwenda sehemu wakanitembeze nione miazingira wakati tunataka kwenda watoto walitaka kwenda nasi, wazazi wakasema wababi wafanye kazi za shule wao watawatoa siku za weekend, watoto hawakuridhia wakabaki wanalia japo kiumri wanaonekana si wa kulia kwa kuachwa.

Kasheshe lilianza tuliporudi, Watoto wakagoma kufungua mlango wa nyuma wanasema tulale nje kwa kuwa tuliwaacha, geti tulifungua kwa funguo ambayo baba mwenye nyumba alikuwa nayo ila ya ndani ndiyo hana, tulikaa nje zaidi ya saa moja na nusu wazazi wakibembeleza watoto wafungune na watoto wanasema hawafungui mpaka Mama akaanza kumwambia mumewe wampigie fundi wavunje.

Baadae Dada wa kazi akarudi ambaye alikuwa kaenda kusuka akawaambia anawaomba wamfungulie ndipo walipofungua na sisi tukaingia.

Cha ajabu wazazi wakasema mnajua kujifungia ndani sio jambo zuri mtakuja kupata madhara, kwanza mmeoga, hebu nendeni muoge mje tule na kesi ikawa imeishia hapo.
Ulitaka wasulubishwe au mtoto sio kila kosa ni kumbonda
 
Back
Top Bottom