1. Mtu amewahi kukosea kutuma kwenye lipa namba 140,000, akaripoti voda. Voda wakanipigia nikawa sipatikani, siku ya pili wakanitafuta kwenye namba nyingine, nikatoa ushirikiano hela ikarudi.
2. Kuna wakala aliweka 2000 kwenye mpesa yangu. Nikasubiri kama nitapigiwa simu, sikupigiwa. Siku ya pili nikabetia, nikala 18,000.
Nikakaa kama wiki kimya, nikawapigia voda kuwa kuna wakala alikosea kuweka 2000 kwangu kama vipi wairudishe. Wakasema hawawezi kurudisha kama yeye hajaripoti. Nikasema kwa hiyo nitumie hela! Wakasema nisitumie.
3. Kuna mwalimu aliazima laini yangu ya voda aweke hela MPESA Atumie intaneti, akaenda kwa wakala kuweka pesa.
Dakika chache nikaona ticha anarudi anahema anasema hebu tuongee pembeni kwanza.
Kumsikiliza akasema wakala kakosea, badala ya kuweka 2000 kaweka 20,000 kwa hiyo tugawane. Nilivyoanza kupinga hilo swala kwa sababu ni mfanyakazi wa wakala ndio kakosea, jamaa akasema tutakufa masikini.
Ikabidi nimtoe 9,000 yaishe. Ile pesa nilipanga kumrudishia dogo lakini ndio hivyo tena