Ulishawahi kukosea muamala wa kiasi gani kwenye simu yako?

Safi sana, haukuwa na mapepe.
 
Vipi mkuu hiyo hela ya huyo mwanamke ingekuwa mzigo mrefu ungemrudishia?😁
 
mi niliwahi kukosea ,nilikuw namtumia jamaa mmoja ivi tulifanya biashara ikaenda poa akanichia namba kwamba nusu nitachukua nusu nyingne,

nikajifanya bingwa nikamtumia huku nakula vyombo fasta fasta nikathibitisha ,

kesho asubuh nachek hela imeenda kwngne ,af yule aliyepokea nikampigia akanijibu "bro pole nipo naitumbua nikutakie masikitiko mema byee" akakata cm.


hii ya pili

manzi yangu (mtu wa ibada sana) aliwah pokea m1.2 kimakosa zaid ya siku mbil hakuna aliyepiga cm kuulizia ,akaamua kumtafuta mhusika ,jamaa aliyekosea ndo kushtuka kumbe alimtumia mtu ambaye alikuw anamdai kumbe kafariki kama jana yake na hakujua,

jamaa alishukuru sana akampoza elfu 10 afu manz et akanipa hiyo ten daaaaaa nadhan toka siku hyo hatuna maelewano mazuri kabsa.

ya mwsho kuna aliwah kosea m5 ikaingia kwangu kimakosa daaaaaa najaribu kutoa fasta kumbe kashapiga cm na wameizuia,siku hyo nililala na stress.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Wewe ni Mimi mtupu
 
Kweli kabisa upo sahihi mkuu, hasa ukiona mpaka aliyekosea anakupigia simu kukubembeleza, ujue hiyo hela ilikuwa inaenda sehemu muhimu sana.
 
1. Mtu amewahi kukosea kutuma kwenye lipa namba 140,000, akaripoti voda. Voda wakanipigia nikawa sipatikani, siku ya pili wakanitafuta kwenye namba nyingine, nikatoa ushirikiano hela ikarudi.

2. Kuna wakala aliweka 2000 kwenye mpesa yangu. Nikasubiri kama nitapigiwa simu, sikupigiwa. Siku ya pili nikabetia, nikala 18,000.
Nikakaa kama wiki kimya, nikawapigia voda kuwa kuna wakala alikosea kuweka 2000 kwangu kama vipi wairudishe. Wakasema hawawezi kurudisha kama yeye hajaripoti. Nikasema kwa hiyo nitumie hela! Wakasema nisitumie.

3. Kuna mwalimu aliazima laini yangu ya voda aweke hela MPESA Atumie intaneti, akaenda kwa wakala kuweka pesa.
Dakika chache nikaona ticha anarudi anahema anasema hebu tuongee pembeni kwanza.

Kumsikiliza akasema wakala kakosea, badala ya kuweka 2000 kaweka 20,000 kwa hiyo tugawane. Nilivyoanza kupinga hilo swala kwa sababu ni mfanyakazi wa wakala ndio kakosea, jamaa akasema tutakufa masikini.
Ikabidi nimtoe 9,000 yaishe. Ile pesa nilipanga kumrudishia dogo lakini ndio hivyo tena
 
Aiseee nimecheka sana hapo Kwa huyo mwalimu aliyekuambia mtakufa maskini kwasababu ya 20000
 
Huyo teacher anaonekana alikuwa na njaa sana.
Jamaa zake Mpwayungu Village
 
Jioni ya leo nimeenda kutuma pesa kwa wakala,mama kanituma

195,000,,,,,imeenda siko,sasa narudi nimwambie mimi tayari,. Kupiga kwa mpokeaji anasema hajaona,

Kurudi kwa wakala jioni hivi, kupiga kwa namba aliyotuma pesa anapokea mbaba anasema ampigie baadae yupo kwenye makelele,

Hapa sielewi kwanza,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…