Ulishawahi kumchukia member wa JF pasipo kumjua

Ulishawahi kumchukia member wa JF pasipo kumjua

Unaweza ukawa unasema kweli, kipindi cha nyuma mkuu hata kama ni utani basi ulikuwa huchagui maneno ya kutumia, mimi binafsi sikuwahi kugongana mahali popote na wewe kwa sababu tu ya kutopenda kujiharibia siku.

Nadhani hata wewe unakumbuka Ban zilivyokuwa zinakuandama, ila siku hizi naona kabisa hata wale wanaokuchokoza unawachunia au kuwajibu vizuri, kitu ambacho kipindi kile ungetegemea kuona matusi.

Nimefuarahi leo kumjua aliyekuwa akinipa BAN. Mwenyezi Mungu akubariki sana kwa kuweza kukiri japo Kidiplomasia zaidi ila wenye upeo uliotukuka tumeshakuelewa.
 
Nimefuarahi leo kumjua aliyekuwa akinipa BAN. Mwenyezi Mungu akubariki sana kwa kuweza kukiri japo Kidiplomasia zaidi ila wenye upeo uliotukuka tumeshakuelewa.

Mkuu mimi siyo Mod.

Wewe ni moja ya watu ninaokubali uelewa wao kwenye nyanja mbalimbali, ukianzia kwenye Muziki wa Zaire/Congo, kwenye Tasnia ya Habari, kwenye michezo hasa ya Simba na Yanga, kwenye baadhi ya issue za kisiasa nk, sasa ilikuwa kila nikifungua profile kuangalia umeandika nini ndo nakuta umepigwa ban.

Na vile ulikuwa humlazii mtu kwa matusi ndo ilikuwa sababu kubwa, siku hizi umebadilika sana, na na kupongeza kwa kubadilika mkuu, kipindi cha nyuma nisingeweza hata kukumention au kuku-quote hata kama ni kwa wema maana akili zako ulikuwa unazijua mwenyewe.
 
Kumchukia mtu sio lazima umuone, labda kama unachukia maumbile yake. Huwa tunachukia 'personality' ya mtu, tabia yake, matendo yake na kauli zake. Jf tunapata kusoma kauli za watu, hivyo si kitu cha kushangaza kumchukia mtu.

Binafsi huwa sichukii mtu bali comment ya mtu. Kutofautiana kimtazamo na majibizano kwa hoja ni jambo la zuri na linajenga. Hili halina maana mtu aandike ujinga kwenye mambo msingi, naweza nikamjibu vibaya halafu nasahau, akiandika kitu cha msingi nampa like yake hata kama ni uzi ule ule.
 
Kuna taarifa kuwa msafara wa timu ya Ruvu shooting umepata ajali mkoani Singida wakati wakirejea nyumbani.
 
umeongea point. kuna baadhi yao humu. naona wanakuwaga na chuki na wenzao. unaweza mquote akakujibu shit balaa
Ni vizuri kupingana kwa hoja na sio kwa matusi! Maana kila anaeamini anachokiongea ana misingi yake Hivyo basi ni jitihada za mtoa hoja kumshawishi anaowaandikia na wao kukubaliana naye au kukubali kutokubaliana nae kwa amani.
 
Mi labda mtu akitukana au kuweka picha mbaya lkn mwisho wa siku akili hazilingani
 
Back
Top Bottom