Ulishawahi kumchukia member wa JF pasipo kumjua

Ulishawahi kumchukia member wa JF pasipo kumjua

Kwa nn nisichukie hasa mtu anapotetea utumbo,mtu anaongea njegele dagaabichi tena nshachukia hata aliyetoa mada asa anataka kila mtu akibaliane na mtazamo..kwanza anayeleft ni uoga huna jibu wala ujasiri wa kutetea mawazo ya unachoamini mwenyewe wakuyumbishwa tu
 
Mara nyingi chuki huambatana na WIVU.Sasa unapomchukia mtu ambae hata hujamuona ni dalili ya kupungukiwa na baadhi ya vitu vinavyokamilisha kichwa cha mwanadamu
Si kweli, Hitler hatukumuona, lakini tunamchukia kwa matendo yake, kauli zake TULIZOAMBIWA!
 
Sijawaha na naomba isitokee kwa sababu kwanza tulio wengi hatufahamiani kisura na makazi yetu. Ila, tofauti ktk fikra ni kitu cha kawaida na huo ndio ubinadamu.
 
Mambozzz
.
Ivi ulishawahi kumchukia members yeyote wa jf. Kutokana na mijadala,mabishano yanayoendelea humu.mimi binafsi sijawahi mchukia members yoyote humu jf. Hata anikashifu vipi.
Ila.
Ulivyoandika Ila Nikawaza Kwanza Kinachofuata
 
Humu kuna full chuki live tena balaa. Ma haters wapo kibao hata wanao kimbilia kuandika opposite ni ma haters pia. Kuna wengine (majina kapuni) ukipinga mijadala yao unaanza kuwaona wanakagua profile yako, wakikupata sijui itakuaje

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nitakuwa mnafiki kusema hakuna watu nawachukia humu:

Kuna watu humu ni wagomvi au wanapenda kutukana tukana hovyo, ili nisimjibu au kuendelea kukereka na issue za mtu huyo huwa naenda kwenye kitufe cha ignore nakibonyeza mchezo umekwisha.

Mfano, zamani GENTAMYCINE alikuwa ni mkorofi sana na anatukana ovyo, nikamwignore, siku hizi jamaa kabadilika sana na hata akitukanwa anajibu vizuri tu, so hayuko tena kwenye ignore list yangu.

Hii ni list yangu ya watu ambao wako kwenye ignore list kwa sababu zangu mwenyewe:

View attachment 512005
Hahahahaha
 
Pole kwa kunifikiria vibaya hapo mwanzoni ila pongezi pia kwa kutambua umuhimu wa GENTAMYCINE Mkuu.

Unaweza ukawa unasema kweli, kipindi cha nyuma mkuu hata kama ni utani basi ulikuwa huchagui maneno ya kutumia, mimi binafsi sikuwahi kugongana mahali popote na wewe kwa sababu tu ya kutopenda kujiharibia siku.

Nadhani hata wewe unakumbuka Ban zilivyokuwa zinakuandama, ila siku hizi naona kabisa hata wale wanaokuchokoza unawachunia au kuwajibu vizuri, kitu ambacho kipindi kile ungetegemea kuona matusi.
 
Teh teh teh Mimi yupoo namjua kwa picha kbsaaa lbd ukute alinitumia ya uwongo yani simpendi mpk shetani wanajua simpendiii.......
..najua anajijuaaaa[emoji57] [emoji57]
 
Teh teh teh Mimi yupoo namjua kwa picha kbsaaa lbd ukute alinitumia ya uwongo yani simpendi mpk shetani wanajua simpendiii.......
..najua anajijuaaaa[emoji57] [emoji57]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hebu ning'ate sikio nani huyo nikamuamshie popo.
 
Ukijikuta unamchukia mtu alafu hujawahi kuonana nae face to face ,ujuwe na wewe unajichukia ,coz haileti sense umchukie mtu uliyejuana nae through mitandao ,but kuna some species wako hvyo wanachukia tu bila reasons behind asee,inabidi waache hyo tabia ,unanchukia mtu Leo hujaonana nae then kesho unakutana nae yeye ndo anakuwa msaada kwako tena

Sent from my TECNO-Y4 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom