Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Binafsi nimewasiliana na wanachama wengi humu ndani (ME + KE), lakini mbali na kuleteana masikhara na kudanganyana kule PM sijawahi kabisa kutaka kufahamiana na mtu humu ndani. Naamini kuna waliokuwa na nia njema na wako Genuine, lakini waovu, wauaji, watekaji, mamluki na matapeli wako wengi sana mitandaoni. Hivyo wale watu wema wanisamehe tu.........

Nashauri vijana, hata kama umependa na kuvutiwa na mwandiko wa mtu, fahamu kwamba huku kwenye mitandao kila mtu huonekana ni malaika japo uhalisia hauko hivyo. Nawafahamu watu ambao wameshaumizwa na kuvurugwa kisa haya mawasiliano ya humu JF, Twitter na Instagram. Binafsi nimewahi kutumiwa links za mitego na E-Mails nyingi huko PM.

Wengine wanaanzia mbali kwa kujenga urafiki mimi nawachora tu nasema Hiiiiiiiiiiiiiiiii. Huko PM nimepewa ofa kubwa za kufa mtu, wengine wanasema wananipenda sana (wanajaribu kunijaza Sweet-Nothing) , wengine wananiletea vitisho,wengine wanataka ushauri, wengine wananiletea umbeya na majungu, wengine wanakuja kunimwagia misifa. Sasa kama ukiwa na kichwa kibovu itakula kwako. There's No Free Lunch in the World: You Eat the Devil's Food, You Pay the Devil's Bill....

Ila kama umempenda mtu wewe jilipue at your own risk, lakini kaa ukikumbuka kwamba waliomo humu ndiyo haohao wa mtaani kwako. Tanzania ya leo imejaa watu waovu wengi mno, tumefika pabaya sana, kuwa makini (Be vigilant and don't have unrealistic expectations).....

Una nakosea ndugu Mgonga Like ???
 
Binafsi nimewasiliana na wanachama wengi humu ndani (ME + KE), lakini mbali na kuleteana masikhara na kudanganyana kule PM sijawahi kabisa kutaka kufahamiana na mtu humu ndani. Naamini kuna waliokuwa na nia njema na wako Genuine, lakini waovu, wauaji, watekaji, mamluki na matapeli wako wengi sana mitandaoni. Hivyo wale watu wema wanisamehe tu.........

Nashauri vijana, hata kama umependa na kuvutiwa na mwandiko wa mtu fahamu kwamba huku kwenye mitandao kila mtu huonekana ni malaika japo uhalisia hauko hivyo. Nawafahamu watu ambao wameshaumizwa na kuvurugwa kisa haya mawasiliano ya humu JF, Twitter na Instagram. Binafsi nimewahi kutumiwa links za mitego na E-Mails nyingi huko PM.

Ila kama umempenda mtu wewe jilipue at your own risk, lakini kaa ukikumbuka kwamba waliomo humu ndiyo haohao wa mtaani kwako. Tanzania ya leo imejaa watu waovu wengi mno, tumefika pabaya sana, hivyo kuwa makini (Be vigilant)......

Una nakosea ndugu Mgonga Like ???
Kabisa aiseh
 
Kumbe ndio huyu? Basi atakuwa ujumbe ashaupata. Ila tayari aliemtaja anaongeza upinzani hahaha.
Aiseh huyo masta ni spesho kesi😁😁

Hapana sio RRONDO ingawa ninamkubali sana pamoja na CONTROLA bahati mbaya hawa ninaowataja wameshatajwa😁😁

Mama yangu mwanamke nilisema sitokuja kufanya akajua humu ndani.
 
Shida ni kwamba hivi twudemu tunaovipenda ni wengi alaf wao ni wachache na wengi wanaonekana ni wabaya kwa muonekano ingawa kuna member mmoja nlishawah kutana nae sijui humu ID yake ni ipi ila alivokua mzur pozi zake nna imani ni moja wa active member humu
 
Back
Top Bottom