Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Ulishawahi kumpenda usiyemfahamu kwa sura?

Kuna mtu nilimpendaga humu jf. Jamani alinitesa sana..namuwaza 24/7. Aliniteka vibaya mno na nilikuwa tayari kwa lolote...ila akawa na moods za ajabu ajabu tukaachana ila nilimpenda for real.
Nasoma comments zake zote na avatar yake matata sana ni picha yake halisi.
.
.
Tuliachana bila kuonana. Utakaposoma hii comment jua kwamba ni kweli nilikupenda na mipango yote niliyowaza juu yako ilikuwa ya kweli.
Nimeshamove on, na Jana ndo nimefuta namba yako wakati napitia contacts kwenye phone book.
Aisee. Pole rafiki
 
mimi nilipendana na mwana jf mmoja....siku tulivyokutana physically tuliongea baada ya kuachana akaniblock....i know sikumvutia coz nina sura mbaya sana (Najijua) na wala simlaumu hata mimi ningekua yy lazima ningeblock......




Sio kupenda kwangu lakini[emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25]

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
@Evelyn Salt itakuwa ni wewe [emoji23]
 
Miaka ya nyuma kidogo enzi hizo secondary school, ndo facebook imeanza basi, nishapataga friend request kutoka kwa mdada mmoja anaitwa Patricia,basi nami sikua na iyana nilikubali na kuanza kuchati mambo ya kawaida kuhusiana na maisha.

Jinsi siku zilivyokuwa zinasonga ukaribu ulizidi kuongezeka na ikabidi tufahamiane zaid, huyu mwenzangu alikua all the way from Congo democratic Republic, lakini alikua akiishi Bulawayo Zimbabwe mambo yalizidi kunoga hadi tukajikuta tayari tuko kwenye penzi zito na wakati hatujawahi kuonana zaidi ya kuchat na kutumiana picha.

Ilifikia kipindi tukaanza kuwasiliana kwa normal calls maana kwake ilikua sio shida coz alikua yuko vizuri economically ( kwa muonekano wa maisha aliokua akiishi) so mapenzi mubashara yaliendelea na kukolea na si unajua wanaume wa bongo kwa swagga, mtoto akanitambulisha mpaka kwa family member baadhi na ahadi kede kede,

Mapenzi mubashara yaliendelea hadi Patricia akaja bongo kujiendeleza kielimu hapo UDSM kwa influence kubwa kutoka kwangu,(mtoto all the way from Bulawayo to Dar es salaam). By that time nilimwambia sitoweza kumuona juu ya sababu za mbalimbali ikiwemo kubanwa na shule na tulikubaliana kwamba afunge safar aje to my home city Mwanza na alikubali, safar ilipangwa na kweli tulionana na sikuamini nilichokiona mkuu.

She was the priests woman to stand beside me kwa kipindi chote kwa wakati ule na alikua classic kinouma alikaa mwanza kwa siku tatu na baadae kurudi Dar.

Wakuu baada ya kuona kua Patricia ni zaidi ya nilivyofikiria na alinizidi kila kitu yaani kuanzia umri, uchumi, na hata elimu hapo ndipo mwanaume nikaona yule manzi si type yangu tena.

Kifupi nilimuogopa but sikumbwambia ukweli na tuliachana kimasihara na ahadi zote ziliyeyuka. But nlikuja kufaidi penzi la mdogo wake aliyekuwa akiitwa grolia tulikuwa same age na alikua kwenye the same proffesional field kama yangu na alikuja kujiendeleza pale UDSM

Kifupi wakuu haya mambo yapo na mara nyingi mapenzi ya namna hii huyayuka punde tu mnapoonana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alivokuja mwanza mlibanjuana??

Au uliishia kumsalimia tu[emoji1]
 
Habari za wakati huu wakuu.

Wakuu hadi naandika hapa binafsi huwa natokewa na hali hii for instance, kupitia mitandao ya kijamii mfano, hapa JF kupitia mada au comment za mtu unaweza jikuta unampenda mtu usiemfahamu.

Mara kadhaa hali hii huwatokea watu na ushahidi anao kila aliewahi kutokewa na hali hii. Note: sio lazima umpende kimapenzi japo inatokea kuna wengine anapenda tu japo aone comments zako au kila anapoingia online lazima apitie profile kwako au timeline yako.

Mbaya zaidi sasa, watu wanaogopana sana humu ndani kiasi kwamba hata ukivutiwa nae au amevutiwa na wewe unapata/anapata shida anaanzanje/unaanzaje kumuaminisha kuwa wewe ni mtu mwema kwake na huna nia ovu.

Mkijitahidi sana mtachat PM akiona niaje niaje anakupiga block kimasihara. Offcoz nafahamu wapo wengi wenye mgongano wa aina hii ya kuvutiwa na baadhi ya watu hususani humu ndani watatoa ushuhuda hapa.

Ninae mpenda akisoma hii thread atajijuwa. Na naomba usione soo mama njoo PM niambie nitakupokea kwa mikono miwili. Huwezi juwa huwenda mimi ndo fungu lako!

Au nasema uongo ndugu zangu?
You're user name is exactly birthday month and date
 
Oooh nishakumbuka, usiache kunipenda lakini
Unatuhumiwa kwa kosa la unyanyasaji wa Kimapenzi.
Umemsababishia binadamu mwenzako maumivu na mateso ya roho na mwili,umemfanya aishi bila furaha na kwa unyonge kwa muda mrefu.

Adhabu.
Mrudishie furaha kwa kumuuliza anataka umfanyie Nini,akikutajia tekeleza.

Usirudie Tena kutesa binadamu wenzio.
 
Back
Top Bottom