Ulishawahi kumpoteza mwenza kwa sababu ya utofauti wa kidini?

Ulishawahi kumpoteza mwenza kwa sababu ya utofauti wa kidini?

Kuna mdada mmoja alijaribu kunivutia kule wanaosali jmosi kisa tu nilitaka oa,nikasepa!
Ukikubali kubadilishwa dini utabadilishwa mpk na kabila, utakuwa wakugeuzwa tu....
Upo sahihi mkuu mke una mbadilisha dini wewe sio yeye akubadilishe dini
 
Mdogo wangu usitafute Mke wa kuoa kwa sababu ya Ubikra wake, au usmart wake hapo chuoni iwe usmart wa mavazi au Akili.
Ukitaka kupata Mke Tafuta Mke
1. mwenye Hofu ya Mungu.
2. Mwenye Heshma na Utii, awe na Adabu kwako na kwa wengine.
3. Familia yao iwe walau na Ahueni ya Shekels isiwe kununua friji au Tv ukaonekana mkwe wetu ni Tajiri.
4. Uzuri, hiki sio kigezo cha muhimu sana, maana unaweza kumpenda kwa uzuri baadae akapata ajali uzuri ukatoweka.

NB: ktk vigezo vyote hivyo kigezo cha muhimu ni hicho namba 1 hapo juu.
 
Mimi binafsi nachukia mtu kuoa au kuolewa na mtu wa dini nyingine!
Kwa mfano nikisikia Mkristo ameolewa na Muislamu nachukia kabisa. Hata nikisikia Mkristo ameoa Muislam nachukia kabisa hapo najua hiyo ndoa itaishia kwenye matatizo tu.Itavurugwa na Majini.
 
Hiyo ni imani yako.

Ndoa nyingi za waislamu kwa wakristo zinadumu na ziko vizuri kuliko za dini moja.
 
mi muhimu aamini uwepo wa Mungu baaasii.
 
Mbona mimi hawa ninaowapata wote wanakuwa wapo tayari kubadili dini na kunifuata?!

Wengine mnakwama wapi aisee 😎
 
Back
Top Bottom