Ulishawahi kumsaidia mtu kupata kazi lakini malipo yake yakawa kukuumiza?

Tenda wema nenda zako
Wema ukigeuka machungu basi sio wema tena.

Kwa hali hiyo tutarudi kwenye kauli ya "Fikiri kabla ya kutenda" au kwa kimajuu/kimalkia "Risk assessment" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kauli hiyo itakupatia majibu haya:

Ukigundua kitendo hicho(kumpa connection) kitaleta madhara hasi, usifanye au ukifanye ukiwa unajua jinsi ya kuja kukabiliana nacho.

Kama kitaleta madhara chanya, kifanye kiroho safi.
 
Kuna jamaa ni mwana JF mwenzetu ila ID siijui yake na yeye naamini hajui yangu. Kulikuwa na nafasi ofisini kwake. Kuna jamaa fulani mpe jina X, alikuwa katika msoto baada ya kupunguzwa kazi. Kwa vile hao jamaa wanatoka sehemu moja, jamaa wa JF akaona amchukue ili afanye kazi katika shirika lao.

Baada ya miaka kama mitatu, ikaanza zogo kazini kwa jama wa JF (alikuwa ni MD), katika kuchunguza akakuta X ndiye chanzo na ni kiongozi wa kupiga majungu ili MD abadilishwe. Jamaa alikasirika sana akamuita na kumuonya asitishe hayo majungu yake la sivyo njia iliyomleta itatumika kumuondoa kabla yeye hajabadilishwa. X alikuwa ngangari, na jamaa hakusita kuhakikisha kibarua cha X kinaota majani. Siku hizi ni paka na panya
 
Pole sana uncle.. Kuna watu ni wanyama kwenye sura ya binadamu, na hawa ndio mabingwa wa kuwaumiza watu wema kama wewe anko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sumu ya mwanamke ni mwanamke mwenzie.

Dawa ya mwanamke ni mwanamke mwenzie.
Pole dada...wanawake hawawezi kaa chumba kimoja wakamaliza mwezi.
Lakini mwanaume wanaweza kaa Geto moja mpaka wakatoboa.
 
Wengi nimewapa michongo baadae wanajikuta matawi ya juu, ila hua sijali kikubwa wanapata rizki na kusaidia familia zao.
Unapomsaidia mtu jambo basi kazi yako inaishia hapo,hakuna haja ya kuanza kumfuatilia tena mpaka uone kua eti anajikuta matawi ya juu,au siku hizi anaringa,

Hapa tatizo lako ni kua,unamsaidia mtu kisha unasubiri reaction yake kwako kwa msaada uliompa,ndio hapo inakuja issue kua,jamaa anaringa,siku hizi hanisalimii,kumsaidia mtu haimaanishi kua awe mtumwa kwako ili kulipa fadhila,

Kila mtu amewahi kusaidiwa kwa njia moja au nyingine katika safari yake ya maisha,kulipwa wema wako sio jambo la lazima,uliyemsaidia nae anatakiwa amsaidie mwingine mwenye shida,kulipa wema kwako ni sawa na kukulipa malipo kwa wema wako kwake.
 
Sijakurupuka kusema "matawi ya juu" nilifupisha tu ila maana yangu ni zile dharau na kuanza kukupiga majungu, nina visa vingi sana ila sijawahi kuchoka kusaidia watu pale wanapohitaji msaada sababu naangalia familia zao hata mimi nasaidiwa tena sana tu.
 
Ni Basi tuu uko mbali,,,ungekuwa karibu yangu na umempumzika upande wa mkono wa Kuume ningekwambia ya kuwa achaneni na mahaba huko makazini mtauana shauri yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…