Ulishawahi kumsaidia mtu kupata kazi lakini malipo yake yakawa kukuumiza?

I have bad experience japo sikuwa nimejariwa .Nilikuwa najishkiza kwenye kibanda cha mpesa kipindi nipo likzo fulani ya chuo mwaka jana. Yule niliyeomba aletwe tusaidiane naye alichonifanyia hakika simpingi mtu anayemnyima mtu mchongo. Nilitamani nilipize kisasi ila nikikumbuka mkono wa dola ni mrefu nikawa najifariji na msemo wa life is full of misfortunes ,forgive and forget
 
Ilikuwaje kwako?
 
Ili usiumie siku nyingine ukiamua kumsaidia mtu saidia kwa kuwa upo au ulikuwa katika nafasi ya kumsaidia na usitegemee postive yoyote kwake, hapo hautaumia na utaishi kwa amani tatzo wengi mnasaidia kama investment, ndio maana mnaishia pabaya na watu wenu
 
Ulitaka akupe Mshahara wake wa Mwezi mmoja?
 

Ilikuwaje kwako?
Kale kabinti kalikuwa kanachepusha hela kwa kuhonga wanaume asee af msala ukanigeukia mimi. Maana kila tukifunga hesabu naona kuna shoti za kutosha daily .Yeye kumbe alikuwa na mipango yake anatuma miamala kwa mabwana zake halafu hata ukimwelewesha baadhi ya vitu akawa hataki kwa kujifanya much know. Siku moja katuma muamala kwa mteja kupitia nmb . Sasa network ikawa inazingua kwenye vile vimashine haikuleta response yoyote . Kwamba muamala failed au successed yeye akaamua kumrudishia mteja zile milion 5 plus zote akasepa akiamini hela haijaenda na ni kitu anajua nishamweleza. Baada ya kuja kukagua miamala mikubwa ilofanyika halafu nikilinganisha na keshi ni vitu viwil tofauti. Nikaona nishapigwa. Ikabidi niwapandie nmb customer hewani. Baada ya kujieleza wakasema muamala ule ulikuwa successed ikabidi niwaombe wauzuie. Kufupisha ni kwamba ile hela kuja kurudi ilinigharimu sana kwa upande wangu na ilichukua mwezi . hiyo haitoshi siku moja nikamwambia mteja anayetaka umeme wa kuanzia milioni moja usinunue. sa sikumoja kaja mama staff wa wizara fulani ambayo ipo hapo dom akitaka umeme wa luku wa 3.9m wa ofisi. yeye kwakuwa anapenda masifa si akanunua. tena hili la umeme nilishawahi leta thread humu. token hazikutoka na hela ikakatwa. kupiga tena simu benki customer kuelezea scenario wakasema tatizo haliko kwao lipo kwa upande wa tanesco. ikabidi nianze mchakato wa kufuatilia na kuandikishwa mabarua n.K. Nachoshukuru hela ilirudi pasipo kuletewa token. Mambo yakawa mengi maana mwenye mpesa aliniangushia msala .Na hako kademu wala kakawa hakawazi. Kabisa. Hilo moja kati ya 100. Mambo yalikuwa ni mengi sana. Nikaja kuhitimisha kwamba. 1. Mwenye mpesa alikuwa anakabandua kale kamform five dropout.2. Mabwana alokuwa anawahonga walikuwa wanamtumia tu . Maana kuna laki 5 mpaka leo hii alimpa muhuni wake haijawahi rudi. 3.Kutokana na ka exposure kadogo ka uelewa wa mambo mengi nilokuwa nao, ikatokea kukubalika na watu wengi nikajengewa chuki kubwa sana kiasi kwamba imenifanya niwe na roho ya kisasi sana.Ila nikaona ya nini kufa kisa hela za watu ikabidi niyaage mashindano.
 
Msaada ni huu, yupo humu naasome nenda kwa mchungaji kaombewe ili akutokee katika maisha yako, jingine mpenzi maisha sio yakuyachezea kuwa makini sana nawatu wanaokuzunguka . Au ukiwa ni unaona bora kule basi nenda huko akusahau
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…