1. Mwaka fulani nilikuwa nasoma nchi fulani ya mbali, nikaamua kusafiri toka mji mmoja kwenda mji mwingine, ilikuwa ni safari ndefu sana kwa treni hizi ninyi mnasema za mwendo kasi unasafiri kama masaa 8, ni kama kutoka DSM hadi Bukoba hivi. Ule mji umejengeka sana, una barabara nyingi sana, magari mengi, majengo kila unaloliona yanafanana, mitaa unaona kama ni ile ile, hawaongei kiingereza (kwa uchache sana utakuta kiingereza airport, train station, bus stations n.k kwenye screens tu, hata polisi ukimwuliza hajui kimombo), watu wanasafiri kwa kuangalia ramani za hardcopy au google map. na mimi ni mgeni kabisa ndio mwezi mmoja tu nimetoka Tanzania kwenye analojia. huwezi amini, kuna mtu aliingia kwenye treni akakaa nilipokaa, alipokaa nami tu nikajisikia raha sana na uwepo wake, alikuwa mwanamke, nimefika njiani nikalala usingizi, naamka yupo pale ni kama ananilinda na kunijali, safari ndefu magoti yanauma kwasababu viti vilikuwa vinatazamana akachukua miguu yangu akaipakata ili inyooke. ile natua final destination, akahakikisha nimepita sehemu zote korofi naelekea sehemu ambayo sitapotea hadi pale nilipokuwa nafikia, akaniaga akaondoka. alipoondoka tu ndio nikahisi kabisa kuwa huyu hakuwa mtu wa kawaida kwasababu alipokuwepo hali ya hewa ilikuwa nyingine na alipoondoka ile hali ya hewa nzuri ikapotea. siwezi kusema moja kwa moja alikuwa malaika, ila najua hakuwa mtu wa kawaida, na kwa ulaya mtu kukujali vile sio rahisi.
2. kuna siku moja nililala usingizi, nikaona maono, Malaika wengi kweli wamekizunguka kiti cha enzi, wanaimba nyimbo nzuri, nyimbo ya kumsifu Mungu wakisema tumpe sifa yeye tu na kwamba hakuna kama yeye mwingine, ni miaka kama 20 imepita, lakini ule wimbo naukumbuka na kuuimba wote hadi sasaivi na picha yote naikumbuka, note za wimbo zote nazikumbuka, na sikujifunza niliona maono naimba tu na malaika wengi na wanaimba vizuri sana sana. wimbo ni kama uliniambukiza upako fulani ambao unaufanya ule wmbo haufutiki kabisa moyoni, wote. kuna mambo nimeyafanay miaka 2 au 5 iliyopita ambayo nimeyasahau, ila wimbo niliouona kwenye maoni miaka 20 iliyopita hadi leo hii upo verse zilezile zote moyoni siwezi kuusahau umepigwa mhuri moyoni mwangu. hapo tusemeje?
3. mengine kadhaa naomba nisiyaseme hapa, code zangu zitafunguka kwasababu nilishashuhudiaga kwa watu.