Ulishawahi kuona malaika?

Ulishawahi kuona malaika?

Mimi Kuna kijana nilikutana nae kwenye basi la gongo la mboto nakumbuka nilipandia mawasiliano(simu200)tulikaa sit ya mwisho kabisa kulia,nakumbuka aliniambia anasoma UDSM,kama si sociology ni Bcom.
Alinisalimia vizuri nikamwitikia marahaba. nakumbuka nilikua vyombo sana,Baada ya Salam akaweka poz kidogo baadae akaniambia nimejisikia Kuomba na wewe,nikamwambia all is well let's pray,nakumbuka alinisalisha Sala ya Toba na akasali Kwa kitambo kidogo.Mwisho wa siku nikashuka majumba sita,aisee nilikoswakoswa kugongwa na DCM,nikajiambia moyoni hakika yule kijana alikua Malaika wangu.
Kama Yupo huku tafadhali naomba uni PM.
Ungekaidi kusali ungekipata. Mungu anatuwekea ulinzi kwa njia ngingi sana
 
Hahahaha baada ya kusoma ule Uzi Wa Jamaa anazungumzia Mungu Wa walokole akagusia habari za malaika

Ili nipa hamasa sana ya kutaka kuona malaika

Sasa wakati nipo kwenye maombi ya jioni siku ya alhamisi wakati nimezama kwenye maombi ile story ya Jamaa ikanijia kichwani
Nikaona hapa hapa kwenye wingu la kuzama niombe Neema ya Mungu nione malaika

Ninapoanza kutamka tu nikajikuta nashukuru na kusema asante Mungu Kwa ajili ya uwepo Wa malaika wako mahali hapa

Gafla hali ya hewa ilibadirika kukawa na hali ya ukungu hivi aise ilishuka nguvu ya roho mtakatifu nijazama jumla hapo nikinena Kwa lugha

Kwa raha ya uwepo ule Wa nguvu za Mungu hata sikuwaza tena kuhusu malaika

So nikajua hata malaika niwaone haitakuwa na faida kwangu zaidi ya kujitafutia majivuno tu

Ninachohitaji nikudumisha ushirika wangu na Mungu wakati wote maana ushirika huo ndio unaosababisha malaika wanihudumie
Ilikua ni nguvu ya roho mtakatifu imekushukia
 
Imeandikwa;
Yohana 14:14
[14]Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
If ye shall ask any thing in my name, I will do it.
Yakobo 4:3
[3]Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
Ye ask, and receive not, because ye ask amiss, that ye may consume it upon your lusts.

Zingatia .
Niambie labda akili zangu fupi ubaya wa ombi langu uko wapi? Sinamatumizi nalo mabaya
1. Mwaka fulani nilikuwa nasoma nchi fulani ya mbali, nikaamua kusafiri toka mji mmoja kwenda mji mwingine, ilikuwa ni safari ndefu sana kwa treni hizi ninyi mnasema za mwendo kasi unasafiri kama masaa 8, ni kama kutoka DSM hadi Bukoba hivi. Ule mji umejengeka sana, una barabara nyingi sana, magari mengi, majengo kila unaloliona yanafanana, mitaa unaona kama ni ile ile, hawaongei kiingereza (kwa uchache sana utakuta kiingereza airport, train station, bus stations n.k kwenye screens tu, hata polisi ukimwuliza hajui kimombo), watu wanasafiri kwa kuangalia ramani za hardcopy au google map. na mimi ni mgeni kabisa ndio mwezi mmoja tu nimetoka Tanzania kwenye analojia. huwezi amini, kuna mtu aliingia kwenye treni akakaa nilipokaa, alipokaa nami tu nikajisikia raha sana na uwepo wake, alikuwa mwanamke, nimefika njiani nikalala usingizi, naamka yupo pale ni kama ananilinda na kunijali, safari ndefu magoti yanauma kwasababu viti vilikuwa vinatazamana akachukua miguu yangu akaipakata ili inyooke. ile natua final destination, akahakikisha nimepita sehemu zote korofi naelekea sehemu ambayo sitapotea hadi pale nilipokuwa nafikia, akaniaga akaondoka. alipoondoka tu ndio nikahisi kabisa kuwa huyu hakuwa mtu wa kawaida kwasababu alipokuwepo hali ya hewa ilikuwa nyingine na alipoondoka ile hali ya hewa nzuri ikapotea. siwezi kusema moja kwa moja alikuwa malaika, ila najua hakuwa mtu wa kawaida, na kwa ulaya mtu kukujali vile sio rahisi.

2. kuna siku moja nililala usingizi, nikaona maono, Malaika wengi kweli wamekizunguka kiti cha enzi, wanaimba nyimbo nzuri, nyimbo ya kumsifu Mungu wakisema tumpe sifa yeye tu na kwamba hakuna kama yeye mwingine, ni miaka kama 20 imepita, lakini ule wimbo naukumbuka na kuuimba wote hadi sasaivi na picha yote naikumbuka, note za wimbo zote nazikumbuka, na sikujifunza niliona maono naimba tu na malaika wengi na wanaimba vizuri sana sana. wimbo ni kama uliniambukiza upako fulani ambao unaufanya ule wmbo haufutiki kabisa moyoni, wote. kuna mambo nimeyafanay miaka 2 au 5 iliyopita ambayo nimeyasahau, ila wimbo niliouona kwenye maoni miaka 20 iliyopita hadi leo hii upo verse zilezile zote moyoni siwezi kuusahau umepigwa mhuri moyoni mwangu. hapo tusemeje?

3. mengine kadhaa naomba nisiyaseme hapa, code zangu zitafunguka kwasababu nilishashuhudiaga kwa watu.
Tupe verse na wanaonekanaje
[emoji23][emoji23]maybe ,maybe not , mkuu unaweza kuta ulipatana na mtu choka mbaya akakuomba msaada wa kitu unakiweza ukapuuza kumbe ndo malaika huyo .wengi tunangoja kiumbe na mabawa ,
Nikupe kisa kingine cha pili ...
2019 kabla corona tu nlikuwa nimesua kiuchumi sana kuna rafiki wa dhati alinitapeli hela kubwa sana nikiitamka utaona nadanganya.
Sasa banae njiani nkitoka kusini kulikuwa kunanyesha nlipatana na majamaa wawili barabara ya mwitu kona kuu .
Wakanisimamisha wakiomba lift , nlihofia ila nkaskia sauti flani hivi siwezi ielezea ikaniambia hao usiwapite niwema.
Nikawapa lift almost kilomita 70 hvi wakashuka ,njiani tulipiga gumzo sana kuhusu uchumi n.k. walishuka wakiniombea baraka nyingi kwa usaidizi .
Waliposhuka tu kumbuka ni usiku na mataa ya gari yapo on na tulikuwa mbali na mijengo kama mita 400 hvi kugeuka nipige mlango wa nyuma lock nikiangalia mbele hawapo ,nkajiambia yaani sekunde 3 napiga lock wamefika kwa yale majengo ila nkapuuza .
Mwezi ule mkuu hela ilinikimbiza kweli kweli , inshort ile gap ya pesa sikuimaliza ila ilibakia kiasi ambacho kule kusua kuliisha .
Malaika anakuja kwa njia nyingi kukupima imani ,wengi tunafeli mitihani midogo sana
Duuh hatari
Wanaonekana mbona physically, ukitafuta baadhi ya video pitia YouTube utaona zipo zimenaswa pitia surveillance camera zimekua zikuonesha
Hao wa mchongo
 
Niambie labda akili zangu fupi ubaya wa ombi langu uko wapi? Sinamatumizi nalo mabaya

Tupe verse na wanaonekanaje

Duuh hatari

Hao wa mchongo
Yakobo 5:16-18
[16]Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Confess your faults one to another, and pray one for another, that ye may be healed. The effectual fervent prayer of a righteous man availeth much.
[17]Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Elias was a man subject to like passions as we are, and he prayed earnestly that it might not rain: and it rained not on the earth by the space of three years and six months.
[18]Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
And he prayed again, and the heaven gave rain, and the earth brought forth her fruit.
 
Sawa mkuu nimekuelewa
Yakobo 5:16-18
[16]Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Confess your faults one to another, and pray one for another, that ye may be healed. The effectual fervent prayer of a righteous man availeth much.
[17]Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Elias was a man subject to like passions as we are, and he prayed earnestly that it might not rain: and it rained not on the earth by the space of three years and six months.
[18]Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.
And he prayed again, and the heaven gave rain, and the earth brought forth her fruit.
 
Mara ya kwanza nilikuwa chuo enzi hizo ndo nlikuwa ushamba unanitoka na nlikuwa napenda betting japo sikuwa na hela ya kubet sana. Sasa ada ilikata kabisa mzee ,nyumbani wakadai hawana pesa nlikuwa nahitaji laki saba hivi nikamilishe madeni .
Siku hyo nimekaa nawaza nirudi nyumbani kwa kuwa bila hela exam sifanyi kukaja jamaa wa kawaida sana hatujuani alinipa kikaratasi kimeandikwa mechi kadhaa akadai nikabet yy hana hela .
Nikaiangalia nikajiambia what the heck ,nlienda cyber nikaweka buku kwa account ,nkabakiza buku 9 mfukoni ,jioni nkaenda kucheki mechi ya arsenal ,kitu saa nne usiku naona message ya congratulations 830k , nlikimbia nje kama mwendawazimu siku hio ,ada nliclear last minute chenji nkajipanga nayo ,yule jama hatukupishana tena mpaka leo nlimtafuta sana .
Mpaka leo naamini yule alikuwa malaika ,leo hii sibet kabisa ila baada ya pale sijawai shinda tena mpaka kuacha kwangu
Huku mnasema kamari ni dhambi, halafu Malaika akakuletea mkeka ukawin! Qmmmk acha niendelee kutokuamini tu huu upuuzi wenu
 
Dah! Mwezi wa 7 nimekula mtoto mkali kimasihara,alikuja ofisini kwangu anajichekesha....nikatake opportunity.

Aaisee ni age ya 24 hivii amejaaa...seee kunawadada wanamwagilia bustanii balaaa...kha! Meza yotee chapachapa. Dah! Akina Neema watamu sana.
 
Kwa ufupi malaika ni wajumbe wa Mungu wa Biblia! Kuna malaika wasiokuwa na miili wanaokuja kwa mission maalum na malaika ambao ni Walokole (hapa naongelea walokole wa ukweli sio wale wanaojitafuta) kibiblia wanaitwa "malaika", katika kitabu cha Ufunuo "kwa malaika wa makanisa yale saba", hao malaika wanaotajwa ni "walokole"! Mungu wa Biblia anaweza kuwatumia walokole walioko hapa duniani kufanyakazi kama "malaika" wasiokuwa na miili!
Huna akili
 
Back
Top Bottom