Hello Wadau wa JF!
Weekend ipo vipi pande hizo?
Binafsi ipo poa nimeshapata breakfast ya chapati za kusukuma, rosti la maini na kachai ka maziwa pembeni.
Kwa wale wapenzi wa Korean Drama Leo nimerudi 2016 naangalia Shopaholic Luis.
Kwenye 1 2 3 nimekumbuka siku ya sherehe yangu kaka yangu nitampa jina la Steve , wakati wa kutoa zawadi ulipofika na yeye alikuwa miongoni waliotoka mbele kufanya hivyo, basi bwana zamu yake ikafika akachukua MIC pale Kwa mikogo tena alikuwa amejipigilia suti na shades juuπ akatangaza kuwa amenipa zawadi ya kunilipia trip ya kwenda Dubaiπ niliposikia tu hii kitu nikajua hii ni zawadi hewa kabisa Kwa sababu najua fika Kaka Steve yeye mwenyewe Kwa kipindi kile Dubai anaiona Kwa picha za googleπ
Je, wewe ulishawahi kupewa zawadi hewa mbele za watu?
View attachment 2998805