Ulishawahi kupoteza marafiki sababu ulishindwa kutoa mchango wa harusi?

Ulishawahi kupoteza marafiki sababu ulishindwa kutoa mchango wa harusi?

Mi shoga angu alinipa mchango wa 35k au 30k sasa kipindi yeye anaolewa nilikua napitia kipindi kigumu sana mi na mume wangu jamani nilijikakamua nikamtumia 15k kaninunia hadi leo na namba angu kafuta
Umejikaza kweli kweli afu unakuja kuambulia block au namba kufutwa....sio poa kabisa
 
Nimetoka kuzungumza na mtu Leo hichi kitu, Nina rafiki yangu sikumchangia pia na wakati alikuwa anashuhudia michango mingine nilikuwa natoa kama kawaida, (tupo group moja),

akaninunia kabisa kabisa, asichojua ni kuwa wakati huo yeye anawaza harusi Mimi nina struggle vibaya mno na maisha yamebana balaa,

Hivi, huwa haiwezekani baada ya kufunga ndoa watu wakawa tu na family dinner kisha kama wataenda honeymoon waende maisha mengine yaendelee..? Why tuna-force kuwa na mambo makubwa ambayo pengine hatuna hata uwezo nayo..?
 
Wakuu,

Imekuwa kawaida mtu anapokuwa anatarajia kuoa/kuolewa kutoa kadi za michango kwa ndugu, jamaa na marafiki ili wakamilishe jambo lao.

Kimbebe kinakuja pale umepewa kadi halafu kutokana na changamoto mbalimbali ukashindwa kutoa mchango huo. Jamaa huwa hawaelewi na ndio inaweza kuwa chanzo cha mawasiliano yenu kuharibika kuanzia hapo au kuisha siku hiyo hiyo unapomjulisha kwamba umeshindwa kuchangia kwenye harusi yake.

Urafiki wangu na besti yangu uliisha kisa nilikosa elfu 50,000 ya mchango kwenye harusi yake. Na hapo mtu umejipiga kwelikweli kutafuta mchango lakini umekosa!

Vipi wewe, imewahi kutokea ukakosana na rafiki yako kisa kushindwa kutoa mchango wa harusi? Mliweza kuwekana sawa juu ya jambo hilo baadaye au kila mmoja yuko na 50 zake mpaka leo?
Too much expectations kills!!!!

Mm Huwa sinaga over expectations so ukifanya au usifanye ni sawa TRUE usipende kuweka matarajio makubwa Kwa watu kama unaogopa disappointment 😔😔
 
Mimi rafiki angu sana mwaka Jana aliniharika kwenye harusi ya mdogo wake Mimi kipindi hicho Niko block bhana sikwenda wala kuchanga toka hapo tumekosana ata namba yangu akafuta na Mimi nikafuta [emoji24] namiss sana uwaga namuona insta na FB hila sasa ndo kumuanza kumtafuta siwezi hila namiss namtakia mafanikio uko aliko na kazi iendeleee
 
Huwa hawaelewi kabisa, na hapo unakuta hata umeelezea sababu ila shingo inashupazwa kuwa umedhamiria
Nilikua nimemuambia week 1 kabla ya shughuri, yeye alitegemea kupewa vikubwa, ko hata nisipo kuwepo haina shida, sasa alipokuja kuona tofauti ndo ikawa mzozo zaidi.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Miye nashangaa sana hivi unajua sherehe ya harusi wanufaika ni mc, watu wa mapambo, watu wa chakula, na watu watu wa vinywaji na ujinga mwingine MC ndio anamua mkae ukumbini mda gani mc akiwa mhuni masaa matatu anamaliza sherehe yani mmekaa vikao miezi mitatu mc anawaweka ukumbini masaa matatu

Sikia wewe bibi harusi mtalajiwa na baba harusi kafunge ndoa rudi nyumbani kula chakula na wana ndugu na jamaa vizuri , jioni amua sasa unasherekea hapo hapo nyumbani au nje ya nyumbani kama nyumbani funga mziki mzuri dj mzuri kiamshe kuleni hapo wa kunywa wanywe uone itakavyochangamka kwanza hakuna limit ya mda mnajimwaga mnavyoweza.
Harusi za vijijini hizi huwa zinanogaa balaa, changanyikenii tyuuh.
 
Nimetoka kuzungumza na mtu Leo hichi kitu, Nina rafiki yangu sikumchangia pia na wakati alikuwa anashuhudia michango mingine nilikuwa natoa kama kawaida, (tupo group moja),

akaninunia kabisa kabisa, asichojua ni kuwa wakati huo yeye anawaza harusi Mimi nina struggle vibaya mno na maisha yamebana balaa,

Hivi, huwa haiwezekani baada ya kufunga ndoa watu wakawa tu na family dinner kisha kama wataenda honeymoon waende maisha mengine yaendelee..? Why tuna-force kuwa na mambo makubwa ambayo pengine hatuna hata uwezo nayo..?
Mbna vijijini shuguri wana andaa wahusika, hakuna kukomoanaa
Tatizo mjini, kinacho kwamishaa ni kamatii, afu pia, ukumbi, MC, etc.

Aaaah wee
 
Pesa sijui ikoje yaan tunakosana sana na watu ambao tuliamini ni ndugu ama marafiki wa ukweli ila pesa ikikatisha tu hapo kati na undugu unakufa. Hivi mchango ni jambo la kumnunia mtu kweli kama hana je akaibe? Huwa sielewi.
 
Mbna vijijini shuguri wana andaa wahusika, hakuna kukomoanaa
Tatizo mjini, kinacho kwamishaa ni kamatii, afu pia, ukumbi, MC, etc.

Aaaah wee
Tatizo mjini tunataka mambo makubwa alafu pesa tunategemea za michango ndio chanzo cha kununiana.
 
Mbna vijijini shuguri wana andaa wahusika, hakuna kukomoanaa
Tatizo mjini, kinacho kwamishaa ni kamatii, afu pia, ukumbi, MC, etc.

Aaaah wee
Eti jamani, kakitu kadogo tu classic basii, cha msingi jambo lenye umuhimu 'kufunga Ndoa' limefanyika, hizi mbwembwe zingine tuachane nazo..!!
 
Tatizo mjini tunataka mambo makubwa alafu pesa tunategemea za michango ndio chanzo cha kununiana.
Wanune tu kiukweli, I can't force myself kufanya kitu kiko nje ya uwezo wangu..!!
If it's the matter of life and death then hapo hata ukijifinya hata ukope ni sawa..!!
 
Huu upuuzi naona nikiuendekeza sitafanya lolote la maendeleo nina kadi 5 zote nimewekwa mwanakamati kiwango cha mwisho 100000 hivi watu wanajielewa kweli? Nitatoa mchango wangu kwa ndugu yangu wa karibu basi wengine waninue tu hakuna namna.
 
Eti jamani, kakitu kadogo tu classic basii, cha msingi jambo lenye umuhimu 'kufunga Ndoa' limefanyika, hizi mbwembwe zingine tuachane nazo..!!
Nilistuka kuna ndoa ya sista ake rafiki angu ilifanyika Iringa, MC ni Gara B, eti malipo yake ni 4M, sasa fikiria MC anachukua 4M kwa kazi ya masaa isozidi 6, si upuuzi huu.

Hapo anategemeaa watu wachange ndo walipee kwa MC lol
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom