Ulishawahi kupoteza marafiki sababu ulishindwa kutoa mchango wa harusi?

Ulishawahi kupoteza marafiki sababu ulishindwa kutoa mchango wa harusi?

kuna mtu yeye hakunichangia ila alikuja akajumuika anaoa mwez huu ntarajia kwenda kujumuika ajabu ananipigia et mchangovwangu vipi nikamuuliza ulinichangia?? nina kawaida moja kama mtu alinichangia ajue mchango wangu ataupata
Hao ambao hawachangi na wanataka kuchangiwa ndo hawafaiii...!! Mimi binafsi nisipomchangia mtu hata group simuadd au kumpigia simu kuomba mchango
 
Kuna mwamba tulipotezana zaidi ya miaka kumi nyuma, siku amenitafuta, akajitambulisha nikasema poa nafurahi kukusikia tena Mdau. Kesho yake akanipigia kunieleza Jambo lake la kuoa na kuniomba Mchango.

Kwa kweli sikutilia uzito ombi lake nikampotezea pamoja na kunipigia simu pamoja na sms za mara kwa mara kunikumbusha mchango., Akafanya shughuli yake, akamaliza. Leo ni mwaka wa nne toka amemaliza Jambo lake, na hajawahi kunitafuta tena japo kunisalimu Ndugu yake.
Ndugu which[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] kama alivyoheshimu msimamo wako wa kutokuchanga heshimu wake No mawasilianoo...!! Mimi kuna bro alinipigia simu kwa shangwee sana kipindi nilipata tatizo flani kumbe ni gia tu aniombe mchango sijawahi pokea simu zake na pia mimi simtafuti.
 
Wakuu,

Imekuwa kawaida mtu anapokuwa anatarajia kuoa/kuolewa kutoa kadi za michango kwa ndugu, jamaa na marafiki ili wakamilishe jambo lao.

Kimbebe kinakuja pale umepewa kadi halafu kutokana na changamoto mbalimbali ukashindwa kutoa mchango huo. Jamaa huwa hawaelewi na ndio inaweza kuwa chanzo cha mawasiliano yenu kuharibika kuanzia hapo au kuisha siku hiyo hiyo unapomjulisha kwamba umeshindwa kuchangia kwenye harusi yake.

Urafiki wangu na besti yangu uliisha kisa nilikosa elfu 50,000 ya mchango kwenye harusi yake. Na hapo mtu umejipiga kwelikweli kutafuta mchango lakini umekosa!

Vipi wewe, imewahi kutokea ukakosana na rafiki yako kisa kushindwa kutoa mchango wa harusi? Mliweza kuwekana sawa juu ya jambo hilo baadaye au kila mmoja yuko na 50 zake mpaka leo?
KWANZA ni ujinga kumlazimisha mtu akuchangie kiasi Maalum. Kama ni mchango mwache mtu atoe alichonacho, hata kama ni elf 5. Na kmaa hana pia is okay. Na hata kama anacho akikataa kutoa pia kwasbb zake pia ni sawa. Kma huna hela yanini kufanya shereh. Jiandae mwenyew kwa hela zako ufany shuhuli yako kwa uwezo wako ulionao, sio kwa kutegemea michang ya wtu. Ni ujinga nasema ni ujinga wa hali ya juu kulazimisha wtu wakuchangie
 
Mimi rafiki angu sana mwaka Jana aliniharika kwenye harusi ya mdogo wake Mimi kipindi hicho Niko block bhana sikwenda wala kuchanga toka hapo tumekosana ata namba yangu akafuta na Mimi nikafuta [emoji24] namiss sana uwaga namuona insta na FB hila sasa ndo kumuanza kumtafuta siwezi hila namiss namtakia mafanikio uko aliko na kazi iendeleee
Pole sana mkuu, na hapo ndio tatizo lilipo....ikiwa una changamoto huwa hawaelewi
 
Pesa sijui ikoje yaan tunakosana sana na watu ambao tuliamini ni ndugu ama marafiki wa ukweli ila pesa ikikatisha tu hapo kati na undugu unakufa. Hivi mchango ni jambo la kumnunia mtu kweli kama hana je akaibe? Huwa sielewi.
Hapo sasa, tabu kweli kweli
 
Nilistuka kuna ndoa ya sista ake rafiki angu ilifanyika Iringa, MC ni Gara B, eti malipo yake ni 4M, sasa fikiria MC anachukua 4M kwa kazi ya masaa isozidi 6, si upuuzi huu.

Hapo anategemeaa watu wachange ndo walipee kwa MC lol
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
😂 😂 😂 kama mtu huwezi kusimamia harusi yako mwanzo mwisho ni bora utulie tu, sio kusumbua watu wengine ambao hujui hali zao zikoje kwa wakati huo
 
Huu upuuzi naona nikiuendekeza sitafanya lolote la maendeleo nina kadi 5 zote nimewekwa mwanakamati kiwango cha mwisho 100000 hivi watu wanajielewa kweli? Nitatoa mchango wangu kwa ndugu yangu wa karibu basi wengine waninue tu hakuna namna.
😅😅😅
 
Wakuu,

Imekuwa kawaida mtu anapokuwa anatarajia kuoa/kuolewa kutoa kadi za michango kwa ndugu, jamaa na marafiki ili wakamilishe jambo lao.

Kimbebe kinakuja pale umepewa kadi halafu kutokana na changamoto mbalimbali ukashindwa kutoa mchango huo. Jamaa huwa hawaelewi na ndio inaweza kuwa chanzo cha mawasiliano yenu kuharibika kuanzia hapo au kuisha siku hiyo hiyo unapomjulisha kwamba umeshindwa kuchangia kwenye harusi yake.

Urafiki wangu na besti yangu uliisha kisa nilikosa elfu 50,000 ya mchango kwenye harusi yake. Na hapo mtu umejipiga kwelikweli kutafuta mchango lakini umekosa!

Vipi wewe, imewahi kutokea ukakosana na rafiki yako kisa kushindwa kutoa mchango wa harusi? Mliweza kuwekana sawa juu ya jambo hilo baadaye au kila mmoja yuko na 50 zake mpaka leo?
Mimi sio mchango wa harusi

Tulikwazana na rafiki angu wa karibu sana kwakua tu nilikataa kujiunga Qnet kama sehemu ya team yake

Mpaka leo hatuzungumzi
 
Tafuteni Hela Mtoe Michango Bila Manung’uniko.

Daah, Kweli Tupo Tofauti.

Mimi michango ya ndugu na jamaa flan flan lakini huwa naikumbatia vibaya mnoo na nachanga bila hiyana yoyote.

Binafsi kuna kitu na gain from such friendships na kuwa social than just kujumuika na watu na kusherekea.

Wachache Watanielewa. Yani sijai pewa card na mtu naemjua nikaacha kuchanga…tofauti ni kwamba tu intensity ya ule mchango unaendana na ukaribu nlionao na hao wahusika.

Sijai changa chini ya laki 1 toka nianze kujitegemea na kula jasho langu mwenyewe

Naombeni mnielewe kitu kimoja watu hupenda kufanya biashara au kushirikiana na watu wanao wapenda. So kwenye maisha jitahdi sana ku build genuine relations. Moja ya mbinu yangu katika hili ni kuchangia na ku participate shughuli za watu…so not just everyone ila kuna watu kabisa unaona hapa gains zipo tena sana.

Lazima uwe na jicho la kujenga relations zenye tija. Binafsi zimenilipa sanaa. Mi hata liquor store sioni shida kumlipia mtu beer 3 mpaka 5 hata wawe mtu 3 instantly if naona kabisa mwamba ana madini huyu. Sijui kama mnanipata lakini.

Add value to ur circle, know the art of winning and influencing the right people thru serving them. Unamkuta mtu liquor store masaki. How tha fxxxk huyo mtu ni njaa ?? Lazima ana information itakayokusogeza mbele sio lazima mtu akupe hela.

(No bragg but ni ukweli / facts)
Shida sio kutoa michango, shida ni pale unatakiwa kutoa mchango lakini uko vibaya kiuchumi na unapitia changamoto kadhaa ambazo zinakufanya ushindwe kutoa mchango huo... na ikitokea umeshindwa kutoa mchango huo wanaotarajia kuoa/kuolewa hawakuelewi na kuvunja urafiki wenu mazima
 
We mbona ulipewa nyama ya ngamia kwa expense ya wengine?!#%&(!!!!. Vipi nyama ya ngamia bado ipo au ilishaisha na ulishainya? Kwahiyo uliuza utu wako kwa vipande 30 vya nyama ya ngamia?
Haahaaaa ile nilipewa sadaka imeshaisha [emoji1787]
 
Yani Mimi namtaja kabisa anaitwa TAJI ni MPUMBAVU ana akili za kikahaba.
MCHANGO nimechanga 100,000/=
Wife ameshiriki vikao vyote vya kina mama vya harusi
Siku ya harusi tukashiriki hatua zote....ukumbini sikufanikiwa kwenda kwa sababu ya dharura ofisini...ila familia niliipeleka ukumbini

JAMAA AMENUNA HATA SALAMU TU HATOI NA NI JIRANI YANGU....

haya yapo yanatokea sana
 
Wakuu,

Imekuwa kawaida mtu anapokuwa anatarajia kuoa/kuolewa kutoa kadi za michango kwa ndugu, jamaa na marafiki ili wakamilishe jambo lao.

Kimbebe kinakuja pale umepewa kadi halafu kutokana na changamoto mbalimbali ukashindwa kutoa mchango huo. Jamaa huwa hawaelewi na ndio inaweza kuwa chanzo cha mawasiliano yenu kuharibika kuanzia hapo au kuisha siku hiyo hiyo unapomjulisha kwamba umeshindwa kuchangia kwenye harusi yake.

Urafiki wangu na besti yangu uliisha kisa nilikosa elfu 50,000 ya mchango kwenye harusi yake. Na hapo mtu umejipiga kwelikweli kutafuta mchango lakini umekosa!

Vipi wewe, imewahi kutokea ukakosana na rafiki yako kisa kushindwa kutoa mchango wa harusi? Mliweza kuwekana sawa juu ya jambo hilo baadaye au kila mmoja yuko na 50 zake mpaka leo?
Mimi ilishatokea mara nyingi tu,unakuta ananinunia kwa muda flani na mimi huwa nampotezea,ila baada ya muda naona akishaanza kuona kuwa kumbe hakuna cha ajabu na yeye sio wa kwanza kuoa,na mwingine hata moto unamuakia kabisa utaona anaanza kujichekesha chekesha,unajua hapa tayari,unamasamehe tu kwakuwa alikuwa hajui alitendalo...
 
Nilistuka kuna ndoa ya sista ake rafiki angu ilifanyika Iringa, MC ni Gara B, eti malipo yake ni 4M, sasa fikiria MC anachukua 4M kwa kazi ya masaa isozidi 6, si upuuzi huu.

Hapo anategemeaa watu wachange ndo walipee kwa MC lol
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mtu anaongea masaa sita tu. Analipwa milioni nne.

Kweli maisha ni kuji Brand tu

Enzi Gara B anafundisha shule ya kata hiyo milion 4 ilikuwa ndio net ya mshahara wake wa miezi nane.
 
Mimi rafiki angu sana mwaka Jana aliniharika kwenye harusi ya mdogo wake Mimi kipindi hicho Niko block bhana sikwenda wala kuchanga toka hapo tumekosana ata namba yangu akafuta na Mimi nikafuta [emoji24] namiss sana uwaga namuona insta na FB hila sasa ndo kumuanza kumtafuta siwezi hila namiss namtakia mafanikio uko aliko na kazi iendeleee
Kama ni rafiki yako Kwa nn hukumwambia hali yako?ukimya wako akajua umedharau tu na uwezo unao.
 
Back
Top Bottom