Ulishawahi kupoteza marafiki sababu ulishindwa kutoa mchango wa harusi?

kuna mtu yeye hakunichangia ila alikuja akajumuika anaoa mwez huu ntarajia kwenda kujumuika ajabu ananipigia et mchangovwangu vipi nikamuuliza ulinichangia?? nina kawaida moja kama mtu alinichangia ajue mchango wangu ataupata
Hao ambao hawachangi na wanataka kuchangiwa ndo hawafaiii...!! Mimi binafsi nisipomchangia mtu hata group simuadd au kumpigia simu kuomba mchango
 
Ndugu which[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] kama alivyoheshimu msimamo wako wa kutokuchanga heshimu wake No mawasilianoo...!! Mimi kuna bro alinipigia simu kwa shangwee sana kipindi nilipata tatizo flani kumbe ni gia tu aniombe mchango sijawahi pokea simu zake na pia mimi simtafuti.
 
KWANZA ni ujinga kumlazimisha mtu akuchangie kiasi Maalum. Kama ni mchango mwache mtu atoe alichonacho, hata kama ni elf 5. Na kmaa hana pia is okay. Na hata kama anacho akikataa kutoa pia kwasbb zake pia ni sawa. Kma huna hela yanini kufanya shereh. Jiandae mwenyew kwa hela zako ufany shuhuli yako kwa uwezo wako ulionao, sio kwa kutegemea michang ya wtu. Ni ujinga nasema ni ujinga wa hali ya juu kulazimisha wtu wakuchangie
 
Pole sana mkuu, na hapo ndio tatizo lilipo....ikiwa una changamoto huwa hawaelewi
 
Pesa sijui ikoje yaan tunakosana sana na watu ambao tuliamini ni ndugu ama marafiki wa ukweli ila pesa ikikatisha tu hapo kati na undugu unakufa. Hivi mchango ni jambo la kumnunia mtu kweli kama hana je akaibe? Huwa sielewi.
Hapo sasa, tabu kweli kweli
 
😂 😂 😂 kama mtu huwezi kusimamia harusi yako mwanzo mwisho ni bora utulie tu, sio kusumbua watu wengine ambao hujui hali zao zikoje kwa wakati huo
 
Huu upuuzi naona nikiuendekeza sitafanya lolote la maendeleo nina kadi 5 zote nimewekwa mwanakamati kiwango cha mwisho 100000 hivi watu wanajielewa kweli? Nitatoa mchango wangu kwa ndugu yangu wa karibu basi wengine waninue tu hakuna namna.
😅😅😅
 
Mimi sio mchango wa harusi

Tulikwazana na rafiki angu wa karibu sana kwakua tu nilikataa kujiunga Qnet kama sehemu ya team yake

Mpaka leo hatuzungumzi
 
Shida sio kutoa michango, shida ni pale unatakiwa kutoa mchango lakini uko vibaya kiuchumi na unapitia changamoto kadhaa ambazo zinakufanya ushindwe kutoa mchango huo... na ikitokea umeshindwa kutoa mchango huo wanaotarajia kuoa/kuolewa hawakuelewi na kuvunja urafiki wenu mazima
 
We mbona ulipewa nyama ya ngamia kwa expense ya wengine?!#%&(!!!!. Vipi nyama ya ngamia bado ipo au ilishaisha na ulishainya? Kwahiyo uliuza utu wako kwa vipande 30 vya nyama ya ngamia?
Haahaaaa ile nilipewa sadaka imeshaisha [emoji1787]
 
Yani Mimi namtaja kabisa anaitwa TAJI ni MPUMBAVU ana akili za kikahaba.
MCHANGO nimechanga 100,000/=
Wife ameshiriki vikao vyote vya kina mama vya harusi
Siku ya harusi tukashiriki hatua zote....ukumbini sikufanikiwa kwenda kwa sababu ya dharura ofisini...ila familia niliipeleka ukumbini

JAMAA AMENUNA HATA SALAMU TU HATOI NA NI JIRANI YANGU....

haya yapo yanatokea sana
 
Mimi ilishatokea mara nyingi tu,unakuta ananinunia kwa muda flani na mimi huwa nampotezea,ila baada ya muda naona akishaanza kuona kuwa kumbe hakuna cha ajabu na yeye sio wa kwanza kuoa,na mwingine hata moto unamuakia kabisa utaona anaanza kujichekesha chekesha,unajua hapa tayari,unamasamehe tu kwakuwa alikuwa hajui alitendalo...
 

Mtu anaongea masaa sita tu. Analipwa milioni nne.

Kweli maisha ni kuji Brand tu

Enzi Gara B anafundisha shule ya kata hiyo milion 4 ilikuwa ndio net ya mshahara wake wa miezi nane.
 
Kama ni rafiki yako Kwa nn hukumwambia hali yako?ukimya wako akajua umedharau tu na uwezo unao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…