Mimi ilikuwa hivi,
Ilikuwa kama ajali tu. Mimi nilikuwa nasali nae kanisani mume wake engineer kuwepo nyumbani ngumu mtu wa kusafiri safiri kwa hiyo ili mke asiwe mpweke nilikuwa kama namsaidia maana mimi sio mchoyo akija anaendeleza 🤣🤣 akitoka namfanya mke wake asitoke kwa wengine ila Mimi tu.
Baadaye nilipata mchongo mkoa ikabidi nihame mawasiliano yakaanza kupungua siku hadi siku si unajua tena fimbo ya mbali haiui nyoka 🤣🤣.
mimi nilikua kama wewe, ila ilifika kipindi nikarudi kwa Mungu, nilitubu dhambi hizo sio tu kwa Mungu, na kwa mke wangu. nilipiga magoti, nikatubu kwa mke wangu kwa kukiri dhambi nilizomfanyie (uchepukaji) kabisa, baada ya kumalizana na mke wangu, nikaenda kwa Mungu, nikatubu, hapo ndipo nikapata amani ya moyo, na wokovu ukawa umeingia maishani mwangu. nilibadilika kabisa, amani ile niliyoipata, uwepo ule nilioupata, nilithibitisha kabisa kwamba mimi sio yulee wa zamani, nimebadilishwa, nimeokolewa, nimekombolewa toka utumwani. Biblia inasema,
MITHALI 28:13,
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
TENA SIO KUUNGAMA TU, BALI NA KUZIACHA, ukiungama bila kuacha toba yako sifuri.
kumbe pamoja na kutubu kwa Mungu, tunatakiwa kwenda kwa wale tuliowakosea na kuungama mbele yao, kwamba nimekukosea naomba unisamehe, nimekutendea mabaya naomba unisamehe, na pia uende kwa Mungu. awali, niliamini unatakiwa kwenda kwa Mungu kimya kimya omba akusamehe, imeisha hiyo. nilifanya hivyo sikupata amani, hadi kwa wale niliowakosea nilipoenda kutengeneza nao wanisamehe. Mke wangu ni mmoja wa watu niliowaomba msamaha, nilikubali adhabu yeyote ila roho yangu ipone, alikasirika sana, almanusura nivuruge ndoa ila kwa ajili ya roho yangu ilibidi iwe.
baadaye alikuja kuona niko serious, na nimebadilika, akageuka na kuwa mke mwema zaidi, yote yamebaki historia. ukichepuka sio tu umemkosea Mungu, umekosea na mke wako pia, kwasabab wewe na yeye ni mwili mmoja na kuna viapo mliapiana/agano kwamba mtakuwa waaminifu, ukivunja agano unatakiwa ukatubu kwake, mwambie nimechepuka nisamehe sitarudia tena. zamani nilidhani wazungu wajinga, kumbe ni desturi waliyokuwa nayo kutokana na ukristo wao wa zamani, mzungu ukichepuka na mke wa mtu jua its just a a matter of time, kuna siku atamwambia tu mumewe "kuna kitu nataka nikuambie", akikitapika tu ndio atapata amani. hekima ya Mungu ikuelekeze, wake wengine utawaambia na watadondoka kwa pressure utauwa, kama mazingira yanaruhusu mpe details kabisa, kama hayaruhusu mwambie tu maishani mwangu nilishakukosea sana naomba unisamehe, Mungu awaongoze.
wengi watasoma hapa na kuamini mimi nilichukua njia isiyo bora, ila kwa njia hii ndio nilitoka kifungo cha uzinzi na dhambi kibao, nilikuwa naishia kutubu kila wakati, unatubu leo wiki ijayo umeshazini tena, hadi nilipokuja kumwaibisha shetani, nikazitubu dhambi na wote niliowakosea, hata wale niliozini nao niliwaomba msamaha kwamba sikutakiwa kuzini, Mungu alibadilisha maisha yangu kabisa, akayaponya na magonjwa yangu, sasaivi sihitaji kitu kingine chochote hapa duniani ila kuendelea kuishi kwenye uwepo wa Mungu, hayo ya dunia yanakuja kwa ziada kama marupurupu tu, ila sitegemei kuacha njia ya msalaba, sitegemei na ninamwomba Mungu anisaidie.