Ulishawahi kuwa addicted?

Ulishawahi kuwa addicted?

Addiction yangu mpira wa miguu tuu, achilia mbali Manchester united timu ninayoishabikia ila imefika mahala naangalia ligi yoyote inshort nikigundua Kuna mechi yoyote inachezwa iwe ligi ya Italy, uholanzi, ufaransa au Spain nimo.

Hapa Kama leo imefika ijumaa nikiingia ndani ni mpira tuu mpaka j3 kazi yangu kubadili tu stations za mipira, hii addiction Wala sijutii inanisave na mengi ya walimwengu ingawa mahusiano yangu ya mwisho yalikufa kutokana na mwenzangu kushindwa kutokana na mpenzi yangu mpira yaliyopitiliza mipaka.

Napoongelea mpira wa miguu namaanisha kuangalia mpira, kubishana kuhusu mpira nipo kwenye groups kama 4 hivi za soccer, mavazi yangu ya kushindia nyumbani na mishemishe za hapa na pale kwa kiasi kikubwa ni jezi za mpira, marafiki wangu wengi wamebase kwenye mpira, Mimi sio muongeaji asili yangu Kama sio kubishana mpira basi tunaeza kukaa kimya hata masaa mawili usiponiongelesha, kwa vijana wa Sasa wapenda mpira Kuna kitu kinaitwa FPL ( Fantasy premeir league) humo namo nimo hii ndio imenishika kabisa.

Hiii addiction inaenda sambamba na muziki simu yangu ina application ya Spotify nikiweka earphones masikioni nisahau kabisa ukipiga simu sipokei hata awe ya boss.
Huwa nadhani niko peke yangu. Naweza nikasahau nilipokuwa naenda nikikuta mpira hata wa timu ambazo sizifahamu.
Sasa kimbembe ni pale Man United anapokuwa uwanjani, hata mke wangu aniambie njoo namwambia asubiri mpira uishe.
 
music-addict.jpg
i think im musicoholic
 
Nimeshindwa kuacha kuvuta unga toka mwana 98


Na kucheza video games mpk kesho mm bado nacheza game tena sasa hivi mwanangu akifunga shule ndio tunapiga game mpk saa 8 usiku


na umeoa? duh !mkeo anajua unavuta unga ? ila nyie wanaume nyie jaman !
 
kupika kupika kupikaa do ba
Nimeshindwa kuacha kuvuta unga toka mwana 98


Na kucheza video games mpk kesho mm bado nacheza game tena sasa hivi mwanangu akifunga shule ndio tunapiga game mpk saa 8 usiku
hivi alosto haikupati..mazee acha bora bangi kuliko unga doh
 
Facebook kuna mchezo unaitwa Farmville, kuna wakati nilikuwa addicted kabisa, nilikuwa ninapanda mazao kuhakikisha baada ya masaa matatu yatakuwa ni ya kuvuna, nitaharakisha kila ninachofanya ili niwe free baada ya masaa matatu. Kuna wakati nilikuwa ninaamka katikati ya usingizi ili nivune mazao yasioze. Hapo ndipo nilipogundua nina tatizo, nilijitoa. Siku hizi FB ninakwenda kuchungulia tu.

Uliwezaje kuacha addiction yako?
Duh madam kuna wakati nikiwa mvulana niliwah kumpenda Bhooke mpenzi wangu hadi nikipishana na mwanamke mwingine njiani alomzidi sura najishtaki kwake...siku hizi ni ex wangu na huwa namtumia happybirthday sms mara moja kwa mwaka!
 
Back
Top Bottom