Najaribu kufanya Takwimu mazingira haya niliyopo sasa na watu ninaowafahamu naona kama 85 % wanaume wanacheat..15% wanawake wana-cheat ...
Simple logic ni hii: Mwanaume akianza ku-cheat, mke anaanza kutopewa huduma ya ndoa ipasavyo. Mume ataanza kutoa huduma ili mradi kutimiza wajibu na wakati mwingine visingizio vya kuchoka. Mama mwenye uhanga akiguswa kidogo tu lazima aingie kwenye line ya ku-cheat. Kama asilimia kubwa ya wanaume wana cheat kiasi kwamba wanashindwa kuhudumia wake zao ama wanashindwa kuwatosheleza wake zao, hapo ndipo asilimia ya akina mama wanaoingia majaribuni inapoongezeka.
Sijui kwa nini haturidhiki na tulivyonavyo?
Hapa wenye kasheshe ni wanaume, nadhani ndio chanzo cha yote. Wanaume tumeumbwa na tamaa, na wengi wetu tunashindwa kuji-control. Mwanaume hata akiwa na mwanamke mzuri kiasi gani, kama hawezi ku-control tamaa zake za mwili he will end up cheating. Kiwi cha macho!
Wanawake walio wengi huwa wana cheat kwa sababu ya kukosa huduma ndani ya ndoa/mahusiano au kama huduma anayopewa ni hafifu akilinganisha na kule alikowahi kupita na haoni kama kuna uwezekano wa kukaa chini na mwenzi wake ili wajadiliane namna ya ku-improve hiyo huduma.