SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,889
kabla ya ndoa jibu linakuja si zaidi ya watatu,... vidume utawasikia nishakutana na wengi, ila wewe umewazidi wote....(kujifagilia!)
Utakuwa na bahati sana kama atakuambia ni zaidi ya mmoja. Mara nyingi atakwambia mmoja au akikuona zuzu atakwambia hajawahi kuwa nae!
Tatizo kuwa la binaadamu ni kutokuwa tayari kubeba dhamana ya matendo yetu na kuishia ama kudanganya au kusingizia mtu mwingine ana kitu kingine (rejea anguko la Adam na Hawa pale bustani na mazungumzo yao na Mungu...wote Adam na Hawa kwa namna moja ama nyingine walijaribu kukwepa dhamana ya matendo yao).
Hivyo kama walivyosema wengine, kwa tulio wengi pengine ni 'vigumu mno' (sisemi haiwezekani!) kuavoid kabisa kudanganya. Na tatizo kubwa katika kudanganya ni ile ya kuendelea kuutunza uongo na kujikuta unaendelea kudanganya tena na tena ili kutunza uongo ulioufanya awali na uliofuatia (in a long term ni kama nuclear activity hivi!)...waingereza wanasema " Lie and stick to it".
Mara nyingi tunadanganya ili ku manage hali fulani kwa muda fulani. Lakini nadhani cha muhimu ni kuangalia hizo situations ambazo tunataka kuzi manage, je kudanganya ndio nyia sahihi? Ukitizama kwa makini utaona situations nyingi ambazo tunadanganya kama tungejipapa muda kidogo wa kufikiri pengine tungepata suluhisho tofauti.
Hivi ni kweli mara zote ni lazima kutoa kauli? Kwa mfano inawezekana kabisa kuomba muda kwa mwenza wako kabla hujatolea maelezo kadhia fulani. Binafsi kwenye mahusiano yangu nimekuwa nikitumia sana njia hii ya kujipa muda kama nikiona kusema ukweli fulani kwa wakati huo unaweza kumuumiza muhusika.