Ulishawahi kuwa na mahusiano nje ya ndoa au na mtu mwenye ndoa?

Ulishawahi kuwa na mahusiano nje ya ndoa au na mtu mwenye ndoa?

Umewahi kuwa na mahusiano nje ya ndoa au na mtu mwenye ndoa?

  • NDIO

    Votes: 48 60.0%
  • HAPANA

    Votes: 33 41.3%

  • Total voters
    80
kabla ya ndoa jibu linakuja si zaidi ya watatu,... vidume utawasikia nishakutana na wengi, ila wewe umewazidi wote....(kujifagilia!)

Utakuwa na bahati sana kama atakuambia ni zaidi ya mmoja. Mara nyingi atakwambia mmoja au akikuona zuzu atakwambia hajawahi kuwa nae!

Tatizo kuwa la binaadamu ni kutokuwa tayari kubeba dhamana ya matendo yetu na kuishia ama kudanganya au kusingizia mtu mwingine ana kitu kingine (rejea anguko la Adam na Hawa pale bustani na mazungumzo yao na Mungu...wote Adam na Hawa kwa namna moja ama nyingine walijaribu kukwepa dhamana ya matendo yao).

Hivyo kama walivyosema wengine, kwa tulio wengi pengine ni 'vigumu mno' (sisemi haiwezekani!) kuavoid kabisa kudanganya. Na tatizo kubwa katika kudanganya ni ile ya kuendelea kuutunza uongo na kujikuta unaendelea kudanganya tena na tena ili kutunza uongo ulioufanya awali na uliofuatia (in a long term ni kama nuclear activity hivi!)...waingereza wanasema " Lie and stick to it".

Mara nyingi tunadanganya ili ku manage hali fulani kwa muda fulani. Lakini nadhani cha muhimu ni kuangalia hizo situations ambazo tunataka kuzi manage, je kudanganya ndio nyia sahihi? Ukitizama kwa makini utaona situations nyingi ambazo tunadanganya kama tungejipapa muda kidogo wa kufikiri pengine tungepata suluhisho tofauti.

Hivi ni kweli mara zote ni lazima kutoa kauli? Kwa mfano inawezekana kabisa kuomba muda kwa mwenza wako kabla hujatolea maelezo kadhia fulani. Binafsi kwenye mahusiano yangu nimekuwa nikitumia sana njia hii ya kujipa muda kama nikiona kusema ukweli fulani kwa wakati huo unaweza kumuumiza muhusika.
 
Hapa naona mnachangia wanaumetu ....nitarudi baadae na mchango wangu
 
...pheeeewww, hii ni ahueni sana. Thanks BJ na DC kwa ufafanuzi makini.

Unajua wanandoa/wapenzi wana misemo yao, utawasikia '...ananiamini na namuamini 100%!' ...kumbe hiyo 100% ni kionjo tu! Kudanganya na kudanganywa ni lazima bana... leo hii utadanganya kwa madogo madogo, kesho na keshokutwa unaongezea kauongo kengine,...kidogo kidogo...

No wonder hakuna hata mmoja kwa waliopiga kura ya INAWEZEKANA aliyejitokeza kutetea hoja hapa, LOL!

Believing in 100% is being naive! Wangu anajua kuwa asilimia zangu za kumwamini ni kati ya 75-99% Siwezi kumpatia 100% kwa sababu sibebani naye kila dakika wala sijamwekea CCTV! Pia sitaki yeye anipe hata 98% kwani ikitokea akajua kuwa shetani alinipitia nikacheat au kufanya kitu tofauti ya makubaliano yetu mengine hakika atakufa kwa ugonjwa wa moyo. To be safe, she keeps some percentages and I keep some too!
 
Ka uwongo lazima kaweko bwana.....hiyo 100% probably exists in Utopia.....
 
uongo mtakatifu...lol, nimecheka kweli! uongo unasaidia hata kwenye maisha ya kawaida.
 
....

Hivi ni kweli mara zote ni lazima kutoa kauli? Kwa mfano inawezekana kabisa kuomba muda kwa mwenza wako kabla hujatolea maelezo kadhia fulani. Binafsi kwenye mahusiano yangu nimekuwa nikitumia sana njia hii ya kujipa muda kama nikiona kusema ukweli fulani kwa wakati huo unaweza kumuumiza muhusika.

Siyo lazima lakini wakati mwingine huwezi kukwepa. Yaani wafe akuulize umechelewa wapi au mbona pesa zimepungua kwenye account wewe umwambie kuwa unaomba muda ili umpatie majibu? Huyo mke wako naona ni aina fulani ya malaika. Wa kwangu anataka majibu ya papo kwa papo na macho yake wakati huo yanakuwa nyuzi 90 kwenye yangu. Hatafuni wala hamung'unyi. Katika mazingira kama hayo sijui kama kuna muda wa kutafuta jibu. Kwanza inahitaji akili ya kuzaliwa tena ya hali ya juu kupata jibu la kumpa!

uongo mtakatifu...lol, nimecheka kweli! uongo unasaidia hata kwenye maisha ya kawaida.

Mbona kuna vitu vingi viberikiwa? Mfano wine kidogo inakubalika..! Kwangu mimi amani ya mwili na roho ni kipaumbele katika maisha yangu na wale niwapendao. Kama kuna uongo kidogo unaweza kunisaidia kufikia adhima hiyo basi huo umebarikiwa!
 
Wa kwangu anataka majibu ya papo kwa papo na macho yake wakati huo yanakuwa nyuzi 90 kwenye yangu
hehehe!
daaki site menifurahisha sana yani!mkeo anataka majibu ya papo kwa hapo kwani we umekuwa mizengo pinda bungeni alhamisi asubuhi na yeye amekuwa MUHISHIMIWA MBUNGE?:bounce:
 
Siyo lazima lakini wakati mwingine huwezi kukwepa.

Dark City,
Nikweli kuna mambo/maswali mengine huwezi kuomba muda. Tatizo langu ni pale tunapodanganya hata kwa situations ambazo sio lazima kudanganya endapo tunaweza kutumia vizuri advantage ya muda. Na kama nilivyosema hapo juu, uongo mmoja unaanzisha uongo mwingine! Na kuna wakati unapelekea hata marafiki zako pia kusaidia katika kudanganya.
 
hehehe!
daaki site menifurahisha sana yani!mkeo anataka majibu ya papo kwa hapo kwani we umekuwa mizengo pinda bungeni alhamisi asubuhi na yeye amekuwa MUHISHIMIWA MBUNGE?:bounce:

Mkuu masuala ya ndoa waachie wenye nazo. Ndoa nzuri ni ya mwezio na mke mzuri hunaye ndani ya nyumba. Kuna watu wana hali ngumu na huwezi kuamini kama kweli watamaliza life expectancy ya Mtanzania (45yrs). Hayo maswali ya Pinda Bungeni ni cha mtoto. Sema tu wengi tumeshajua jinsi ya ku-deal na hayo mambo ndo maana unaona tuna amani. Lakini katika hako ka mchakato, ule uongo wetu uliobarikiwa na bwana unasaidia kama 60%.
 
Dark City,
Nikweli kuna mambo/maswali mengine huwezi kuomba muda. Tatizo langu ni pale tunapodanganya hata kwa situations ambazo sio lazima kudanganya endapo tunaweza kutumia vizuri advantage ya muda. Na kama nilivyosema hapo juu, uongo mmoja unaanzisha uongo mwingine! Na kuna wakati unapelekea hata marafiki zako pia kusaidia katika kudanganya.

Mkuu hapo inategemea na intention ya kusema huo uongo. Kuna uongo unaotumiwa kama excuse ambao mimi siuafiki. Mfano umesahau kununua kitu cha muhimu nyumbani (ambacho umeahidi kukipitia dukani wakati wa kurudi home) then unaanza kusema uongo. Huo ni upuuzi. Lakini kuna mambo ambayo ni vigumu kumweleza mke wako kila kitu akakuelewa. Mfano una mshikaji wako hana kazi na wewe unampatia pesa mara kwa mara. Je kama mke wako hapendi utoe misaada ya namna hiyo utamweleza?
 
Ambaye hajawahi kumdanganya mwenziwe na awe wa kwanza kunibishia hapa. Nina uhakika hakuna hata mmojawenu ambaye hajawahi kumdanganya mwenzie. Nikiwemo mimi.
 
Ambaye hajawahi kumdanganya mwenziwe na awe wa kwanza kunibishia hapa. Nina uhakika hakuna hata mmojawenu ambaye hajawahi kumdanganya mwenzie. Nikiwemo mimi.

Hata mimi nitafurahi kupata ushuhuda wa mtu kama huyo. Huyo anaweza kuwa Malaika Gabriel.
 
Mkuu masuala ya ndoa waachie wenye nazo. Ndoa nzuri ni ya mwezio na mke mzuri hunaye ndani ya nyumba. Kuna watu wana hali ngumu na huwezi kuamini kama kweli watamaliza life expectancy ya Mtanzania (45yrs). Hayo maswali ya Pinda Bungeni ni cha mtoto. Sema tu wengi tumeshajua jinsi ya ku-deal na hayo mambo ndo maana unaona tuna amani. Lakini katika hako ka mchakato, ule uongo wetu uliobarikiwa na bwana unasaidia kama 60%.

kweli huo ni uongo mtakatifu, pia mie uongo umenisaidia bwana mana natakiwa nitoe majibu pacpo kituo, sasa kuweka mambo sawa tuweze maliza cku vizuri ni bora ni mix....50-50
 
kweli huo ni uongo mtakatifu, pia mie uongo umenisaidia bwana mana natakiwa nitoe majibu pacpo kituo, sasa kuweka mambo sawa tuweze maliza cku vizuri ni bora ni mix....50-50

Huo ndo ukweli wa maisha dada. Hebu angalia hiyo list ya Mbu, yaani yoote ukiyafanya kwa nia nzuri ni matakatifu kabisa

kudanganya unapochelewa kurudi nyumbani?
kudanganya mapato na matumizi yako?
kudanganya kuridhishwa kimapenzi japo unatoka kapa?
kudanganya hakuna alilokuudhi ili yaishe?
unexpected mobile calls, ukajidai humsikii mpigaji?
kudanganya mambo unayojua yatamuudhi ukimwambia ukweli?
kumdanganya mahusiano yako na marafiki asiowapenda?
nk,...nk...?
 
We danganya tu hata musa alidanganya kwamba mke wake ni dada yake ili apate hifadhi na mke hakuudhika! ije kuwa miaka hiiiii......Danganya tu ila jua baba wa waongo ni SHETANI
 
We danganya tu hata musa alidanganya kwamba mke wake ni dada yake ili apate hifadhi na mke hakuudhika! ije kuwa miaka hiiiii......Danganya tu ila jua baba wa waongo ni SHETANI

Kimbweka,

Unaongelea realities au ideal life? Tupe basi upande wako. Wengine tunaongelea yale tunayokutana nayo kila siku. Binafsi nitafurahi sana kusikia upande wako usio na chembe ya nguvu za shetani!
 
Yaani kila nikiisoma hii mada, moyoni najiskia mkosaji.
binafsi huwa nadanganya sana mara nyingi lengo huwa ni kunusuru uhusiano wangu.
lakini huwa sipendi iwe hivyo.
Inaniuma sana.
 
Yaani kila nikiisoma hii mada, moyoni najiskia mkosaji.
binafsi huwa nadanganya sana mara nyingi lengo huwa ni kunusuru uhusiano wangu.
lakini huwa sipendi iwe hivyo.
Inaniuma sana
.

Karibu Mama wa Mtajiju!
 
Back
Top Bottom