Ulishawahi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti mliyeshibana sana?

Nilishawahi kuwa na rafiki,alinimotivate sana vitu vingi,nlikua sipendelei sana kusoma ila alikua ananihimiza mpaka nikawa nafauru pepa balaa.

Alikua na mtu wake i was there,jamaa alikua hanipendi hata kuskia jina,but rafiki yangu huyu alikua haelewi kuhusu mimi.

Kesi ilianza nilipopata mpenzi akaanza kuzuia hata nisipige stori na rafiki yangu,binafsi nilikua upande wa rafiki yangu nikimtetea kwasababu huyu mpenzi kaukuta urafiki

Baadae wakatafutana wakaanza kugombana,yule mpenzi akawa anamtukana rafiki yangu,nikamuonya,but huyu rafiki nae akavuka mstari akawa anamdhalilisha sana yule mpenzi,kiasi cha kutaka mimi nimsapoti kumnanga mpenzi wangu,alipoona sisapoti sana akaanza kunitoa.

Akajaga kwenda chuo,sasa si unajua wengine vyuo vinawabadilisha,bhasi akawa matawi ya juu,full zarau,urafiki ukaiaha like that.

But mchango wake kwenye elimu yangu ni mkubwa sana and namuheshimu mpaka kesho yule dada.
 
Nahisi ni mimi, kujificha huku kwa ID basi tu, ila ni mimi best
 
Daa.. mimi naongea kwa masikitiko makubwa sana kwa sababu, napataga marafiki wa kushibana wa jinsia tofauti na yangu. TATIZO LINAKUJA HAPA, katikati ya urafiki ndio umenoga sasa, tunajikuta tupo kitandani.

Baada ya hapo sasa tunaahidiana hio ni just a one time thing, imetokea tu bahati mbaya. Tukikutana tena mambo yanajirudia, tunabaki kusema tuendelee kukimbiza mwenge ila MARUFUKU KUFALL IN LOVE KWA MWENZAKE.

Sasa, wivu wivu ukianza unajua tayari makubaliano yashavunjwa. Na urafiki unapungua kiivvyo mpaka unatokomea kusikojulikana.
 
Nahisi ni mimi, kujificha huku kwa ID basi tu, ila ni mimi best
Sidhani kama ni wewe boss.
Au unafanana naye??
Nitajie jina nione.

Huwa nipo huru kumwambia changamoto yangu yoyote,na yeye hivyohivyo.
Kuna kipindi mtu unapita,haujitaji pesa Wala vitu..Bali unahitaji faraja tu!
Anajitokeza kukufariji,anakuombea.
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.

Ninao marafiki wengine wengi tu wazuri,
Pengine unaweza kuwa upo miongoni mwao..ila huyu niliyemtaja hapa nadhani ndiye niliyemzoea zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nilikuwa nae ila mwishowe tulibanduana, naikumbuka siku hiyo nilikuwa nimevurugwa home, so akawa amekuja geto hata sijui tulianzaje nilijikuta nipo juu take huku nahema utazani nilikuwa nakimbizwa daah! Ila kwa sasa kaisha olewa huko Morogoro
 
Ulimnyima papu...c .ndo maana akala Kona ukitaka kula lazima uliwe kidogo yakheee!!!
[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu yule Kaka Kama vile alishushwa Toka mbinguni hakuwahi omba tunda, kwanza angeomba nadhani ningepoteza ule Uhuru wa kushare nae Mambo yangu.

Story za mdinyo ilikuwa ananiulizaga vitu gani wanawake wanapenda kufanyiwa in bed ili akampagawishe navyo Dem wake. Halafu akifanya anakuja kunipa mrejesho, urafiki wetu ulifikia kuwa na Uhuru wa dizain hiyo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ongea na watu , na wewe pia wasaidie sio usaidiwe wewe tu wapigie simu ,salimia sio kila siku utafutwe wewe kwani we nani

Acha majivuno uone kama utaendelea kuita watu wanafiki
 
Nimeshakufahamu na mwandiko wako Nimekukumbuka sana tafadhali jibu message yangu hiyo ndefuu urafiki uendelee .
 
Thank you🙏
I also miss you a lot rafiki
 
Duuh na story zote hizo hujawah kumtamani?

Na jamaa hajawahi kuomba tunda

Kuwa na rafiki wa kike so close hivyo ni sawa na kutembelea muwa kama mkongojo lazima utaula tu ...
 
Nilikuwa na binti mmoja mke wa mtu, alinipenda na alikuwa wazi kwangu kuliko hata kwa mume wake kabisa. hata jambo la ndani kitandani ananiambia na ananiomba ushauri, jambo lolote la kimaendeleo kabla hajaenda kujadili na mumewe anakuja kuomba ushauri kwangu kwanza, aliniamini mno na hapo ndio nilijua udhaifu wa wanawake. aliniambia basi tu amenikuta nimeoa, ingekuwa bado na yeye bado angeniloga hata kuniloga ili nimuoe kwasababu mimi ndiye nilikuwa nampa furaha na faraja ya maisha yake, alikuwa anadeka balaa. ajabu yake, sikumlala pamoja na kuwa na urafiki wa miaka mingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…