Ulishuhudia mama yako akiwa mjamzito?

Ulishuhudia mama yako akiwa mjamzito?

Mi sikushuhudia, ila nilikuta zile story za kununua mtoto...
Umenikumbusha mbali mkuu, mdogo wangu wa mwisho wakati anazaliwa Bi Mkubwa alisema amemnunua dukani.

Nimekuja kujua mtoto anazaliwa baada ya kusoma topic ya Ukuaji kwenye somo la Sayansi darasa la 6.

Kweli Wazee wa Zamani walituweza 🙌
 
Nilishuhudia kwa wadogo zangu wawili wanaonifuatia, ila zaidi ni wa mwisho kabisa ambae muda mwingi nilikuwa karibu na mama kiasi cha kuwa baadhi ya siku mtoto akicheza analifunua tumbo na ananionesha mtoto alivokuwa anachezacheza na alikuwa ananishikisha kabisa. Nilikuwa nina kama miaka 12 au 13 ila that was the best thing mama alichonifanyia kwenye ujauzito wake, ikifuatiwa na za kumuona mtoto wangu mwenyewe anavocheza na zile pilika za kuzunguka tumboni.
 
Niliambiwa ili mtoto apatikane ilibidi mama ale sana mpaka tumbo liwe kubwa halafu likifika size inayohitajika wanakwenda kwenye chumba kimoja cha hospitali ambapo kuna watoto wengi, taa inazimwa. Atakaeshikwa wa kwanza ndio mtoto anaerudi nyumbani.

SIku ya kwenda 'kuchagua' mtoto hospitalli kulizuka tafrani nyumbani maana nilitaka lazima nienda kusaidia kuchagua, sikutaka mtoto awe wa kiume.
 
Mimi nilivyokua mdogo nilijua baba kazaliwa na mama eti😅😃
Pia nilizani neno kufiwa lina maana ya kufi....lwa hivyo wanapunguza ukali wamaneno ili nisijue dah akili za utoto bhana🤔🤔
Kingine pia nilikua naogopa kuku hadi nyama yake yaani mimi nikiona nyama ya kuku natoka mbio🙄🙄
 
×8? Umetisha Mkuu
Wa kwanza anazaliwa.Akifikisha miaka miwili,mama yake ananasa ujauzito wa pili.Yule wa kwanza anakuwa bado hajui ujauzito ni nini.Kwa makadirio,akifika miaka minne hadi mitano na kuendelea ndipo ataanza kujua.Na atajua hasa kupitia maneno ya watu waliowazunguka au udadisi asilia wa watoto.Unaona?🤔
 
Mimi nilivyokua mdogo nilijua baba kazaliwa na mama eti😅😃
Pia nilizani neno kufiwa lina maana ya kufi....lwa hivyo wanapunguza ukali wamaneno ili nisijue dah akili za utoto bhana🤔🤔
Kingine pia nilikua naogopa kuku hadi nyama yake yaani mimi nikiona nyama ya kuku natoka mbio🙄🙄
😂😂😂😂😂Ulikuwa bado unatumia antenna chenga kibao.Hukuwa umefikia viwango vya dish.Usisikitike.
 
Miaka ya nyuma akina mama walipata(kujifungua) watoto hadi kumi+.Kwa hiyo yule wa kwanza kuna uwezekano alimuona ,kwa wastani,mama yake akiwa mjamzito mara nane.🤔
Na inawezekana kabisa wala hakujua kama mama ni mjamzito, zamani watoto hatukuwa smart mama anatoka hosp na mtoto unaambiwa ametoka kununuliwa na hapo mama alikuwa amelazwa siyo kwamba hata alienda na kurudi!
 
Nimelizingatia hilo.Soma komenti #12.
 
Na inawezekana kabisa wala hakujua kama mama ni mjamzito, zamani watoto hatukuwa smart mama anatoka hosp na mtoto unaambiwa ametoka kununuliwa na hapo mama alikuwa amelazwa siyo kwamba hata alienda na kurudi!
Absolutely...yes
 
Mimi mdogo wangu wa mwisho anazaliwa nilikuwa sijui chochote hivo nilishtukia tu mama yupo na mtoto hata kipindi akiwa mjamzito sikutambua chochote

Hapana mimi ni last born Alhamdulillah[emoji1374]
 
Back
Top Bottom