Ulitegemea nini kwenye ndoa ila baada ya kuingia mambo yakawa tofauti?

Niliplan nikifikisha miaka 30's nioe ila nikisikia au kusoma neno ndoa nasikia maumivu makali moyoni mwangu ni kama mtu anachoma moyo wangu hata upumuaji wangu unabadilika kabisa, yani hapa nasoma huu uzi nipo kwenye hiyo hali, mleta uzi yupo sahihi kabisa low your expectation binadamu anabadilika muda wowote, ni wanawake wachache sana katika 100 wakiolewa wanakuwa wake kweli ila wengi wao wakiolewa tu wanabadilika wanakuwa wajeuri, viburi, wajuaji, wanafiki, hawana siri ya nyumba mostly wao ndo wanajigeuza wanaume ndani ya nyumba yaani ni vurugu tupu, nafikiri kwa vijana wanaotaka kuoa expectation zikiwa kwenye upande negative mtaweza kutoboa maana tayari utakuwa umeshajiandaa ila ingia kwenye ndoa na positive expectation hautoboi kabisa
 

Kijana,

Umenena vyema


Tunapoamua kufanya maisha/kuhusiana na watu tuache nafasi ya wao kuwa binadamu na tusisahau kuacha nafasi ya kupata matokeo tofaut ….hii itakupa control nyakat ngumu
 
Hii ni special kwa waliooa na wenye matarajio ya kuoa kwetu sisi wengne tupite hiv πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kwakuwaza kwaundani, naona kuishi mwenyewe kuna utulivu kuliko ndoa. Nipo mimi kama mimi napanga ratiba zangu halafu nina amani tele ndani ya nyumba. Upweke upo tu, hata aliyeoa anapitia upweke katika kipindi fulani. Ila hii amani kuipoteza kwakweli naona siwezi.
 
Basi kwasababu hii, kulikua hamna haja ya kucertify na kulegalize mahusiano yenu. Kama hiyo ndio ndoa, basi hata mimi siiwezi. Maana mpaka sasa hata kutongoza wanawake watano sijafikisha nanaonaga kupoteza muda tu.
 
M nljua show kila nkitaka napata wee. Hzo kalenda nyie
 
Mhhh sijui hata nachokitrgemea mpaka sasa ngoja nikiingia ndio ntayajua hukohuko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…