Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Mama anatoa michango sana ya harusi
Nilimwambia asiwe anatoa zaidi ya 20k
Akaniambia anachangia ili sendoff yangu achangiwe pia
Nikamwambia sitofanya sherehe ya sendoff wala harusi.

HUo muda ni bora nipelekwe kijijini kwetu nikafundwe😎
Muda ukifika huwezi kukakataa hy kitu..kuna msukumo wa mama na mama wadogo...mashangazi...majirani na marafiki....hasa Kwa nyie Wadada
 
Sina hela
 
Nilijiwekea lengo la kutosumbua watu kwenye michango, na nilifanikiwa
Sawa sawa hii hata mimi ilikua hakuna kitu nilikua sipendi kutuma sms za michango na vikao...hivyo nikaamua kuwa na kamati chache nzito na mimi mwenyewe kusimama kidete ingawa niliumia ila sikusumbua mtu

Na hiyo imenifanya mpk leo mtu ashindwe kunipa kadi ya michango maana mie sikuchangisha
 
Wengine huwaombi mchango lakini ikifika zamu yao lazima wakuletee Kadi ya Mchango πŸ™Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…