Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Hiyo lazima ilikuwa classic and simple

Kuna watu wanataka harusi za milioni 20 alafu wao Wana kianzio cha laki 5 🙌
Ilikuwa simple sana, tulifanyia kijijini miaka hiyo kwa hela hiyo watu walikula wali nyama (hasa watoto wa mtaa) na soda ,kuimba nyimbo,kucheza na kufurahi.

Mke wangu nakumbuka alichangia laki mbili na sabini elfu, kiasi kilichobaki nilitoa hela yangu maana hatukuchangisha mtu zaidi ya kuwasafirisha wazazi tu (baba na mama)
 
Hongera Mkuu, Shemeji anaonekana alikuwa mwelewa.

Ukifanyia Kijijini inakuwa ni kama unarejesha shukrani Kwa jamii yako.

Na ukiwa Mpenzi wa Siasa inakuwa njia ya kuelekea Dodoma hiyo 😅
 
Hata kama babu. Nyie babu na bibi zetu ndo mnaotusukuma vijana kwenda siko. Anyways wenye hela waserebuke...wasio nazo wahenderee kuiga mpk wakufe...😅😅😅😅😅
Eti Wahenderee😅 🙌

Sherehe zinakula sana Uchumi wetu, Kuna wengine hadi huenda Benki kukopa ili kufanikisha sherehe 😜

Wazee sherehe zetu zilikuwa za kimya kimya tu 😜
 
🤣🤣🤣🤣 babu mbona na nyie mnatusevu dada muuza parachichi
Hahaha..........hiyo ni Kwa Vijana wa hovyo, ila sisi Wazee lazima tusevu Majina mazuri mazuri ili kumpa changamoto Bibi yenu.

Unakuta nimekusevu "Malikia Elizabeth" nikiulizwa namwambia Bibi yenu, hivi unakumbuka Mwaka 47 nilifanya kazi na Malikia Elizabeth pale Tanganyika, bado nina namba yake ya Simu 😜🙌🏃🏃🏃
 
Back
Top Bottom