Ulitumia kiasi gani cha fedha ama umepanga kutumia kiasi gani cha fedha kugharamia harusi yako?

Michango Kwa maoni yangu, naona watu wengi hawapendezwi nayo. Wanatoa ile basi tu lakini wengi hawapendi kuchangia hasa Kwa nyakati hizi hali ya Uchumi imekuwa tight Kwa watu wengi
Kuchangia ni jambo zuri sababu tunaonyesha umoja katika furaha na shida ila sasa ni vema watu watumie hoja ya kuchangia kama swala la kulika tu kushiriki shughuli mkazo uwe kwenye kushiriki vikao vya kamati ya maandalizi kama wajumbe na si lazima iwe physically unaweza tumia WhatsApp, clubhouse au closed channels nyingine kama sms za kawaida ambapo wajumbe watashare taarifa na kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia shughuli kufana na kumaliza salama.

Shida watu siku hizi anakutana na demu wake huko, anajikuta kidume kupiga goti avishe pete binti wa watu na tukalio twake utadhani limao za mia mia, kumbe mfukoni ana milioni moja na hana hata vyanzo vya mapato vingine zaidi ya kutegemea michango. Halafu anajitutumua kufanya sherehe ya milioni 30+

Hivi unaijua milioni 30+ mzee?

Halafu hii michango mnaomba kwa watu ambao akiona tu sms yako ya maombi ya mchango na kumuunga group la WhatsApp ana nung'unika na anaitoa kwa maumivu sana ile hali hajaridhia kufanya hivyo, hiyo ndoa itadumu kweli?

Nadhani watu wajifunze kunormolize minimum Budget wedding receptions. Na wanajamii tuache nyooshea vidole na kunanga vijana na mabinti wanaofanya sherehe za gharama nafuu sababu tunawafanya wahisi wameanza maisha na mikosi au kidhaifu jambo ambalo si kweli. Sehemu muhimu ya ndoa ni kuishi pamoja na sio sherehe nzuri na ya kifahari.
 
Nakubaliana na wewe Mkuu.

Vijana waambiwe unaweza kufunga Ndoa ya gharama nafuu ya sherehe na bado ikafana.

Muhimu upangilie vizuri matukio yako.

Jamii pia vyema ikabadirika, ingekuwa hiyo michango tunayochanga Kila Siku wapewe maharusi kwaajili ya kwenda kuanzia maisha if possible.

Badala ya kuchanga kwaajili ya sherehe, tungekuwa tunachanga kwaajili ya kusapotiana ili kujikwamua Kiuchumi
 
Kila kitu kilimalizikia kanisani.

Chakula caterer TZS 3,000,000/-
Vinywaji ( maji, soda, seres juice) TZS 524,000/-

Gari tulitumia letu na niliendesha mwenyewe

Mavazi Mme,Mke na wapambe TZS 2,000,000/-
Kukodi tents na meza za chakula TZS 540,000/-
Picha TZS 150,000/-

Hotelini USD 300 siku tatu, palikua na offer seaview USD 100 per night.

Kwa ufupi iligharim USD 3000.

Hapakua na michango licha ya kamanda wangu mmoja kusisitiza akanipa 150k.

Haya mambo usifuate mkumbo sana, fanya unachoweza ili mradi nyie wahusika mfurahie.

Namie ni kama mleta Uzi, zingatia kuibariki ndoa kanisani...2024

Mambo hayakua mengi, ilipomalizika ibada ya kawaida, tukaitwa mbele zoezi likakamilika kwenye Saa tisa likafuatiwa na chakula hapo hapo kanisani.

Saa mbili tunaangalia taarifa ya habari ITV.
 
Nilinunua mchele kilo 5 na nyama na matunda nikawaagiza wapike kawaida wapo waliopata na wengine wakapata matunda. Maji ilikua katoni 1. Ndoa jioni hivyo niliowaalika walikuja wakiwa washakula japo sikuwaambia. Hapo naona ninahamia kwenye nyumba yangu niliyojenga.
 
Hongera sana Mkuu, ulikuwa na event planner nini?

Hiyo ratiba ilikuwa fupi isiyochosha.

Kama ulivyosema, vyema kufanya sherehe ambayo itawafanya wanandoa kufurahia sio kuondoka na Madeni baada ya tukio
 
Nilinunua mchele kilo 5 na nyama na matunda nikawaagiza wapike kawaida wapo waliopata na wengine wakapata matunda. Maji ilikua katoni 1. Ndoa jioni hivyo niliowaalika walikuja wakiwa washakula japo sikuwaambia. Hapo naona ninahamia kwenye nyumba yangu niliyojenga.
Waliokosa hawakunung'unika kweli?

Kwa bajeti hiyo inaweza kuwa ulitumia less than 500k
 
Mimi harusi au sherehe ya ndoa nilifanya kumfurahisha tu bibi harusi, ndugu zake na ndugu zangu hasa mzazi wa kike aliyelalamika kuwa eti amechangia wengi na yeye achangiwe.

Mimi sikuwahi kuwa na visheni ya kutumia gharama na kusulubisha watu kiuchumi eti kisa naoa.
Mahali nilitoa yote mimi, na kuwaunga mkono waliotaka hiyo sherehe nilitoa milioni 2, shera, suti ya Best waliyenitafutia, na gauni la mke wake.

Kwa sababu sikuwepo kwenye maandalizi ila kwa mujibu wa mwenyekiti wa sherehe ile walitumia kama mil 9. Niliwaongezea na michango ya wadau walionipa kama 2m nyingine
 
Suala la Kuoa ama kuolewa bado litaendelea kuwa ni hitaji muhimu miongoni mwa Jamii ya watu wengi Ulimwenguni.

Kwa Tanzania, tunazo Ndoa za aina mbalimbali ambazo zinatambulika kisheria ambazo ni Ndoa za Kidini, Kimila na Kiserikali.

Mara baada ya kufunga Ndoa, maharusi wengi Kwa kushirikiana na jamii zao, hupenda kufanya sherehe. Sherehe hizo huambatana na michango Kwa walio wengi kupitisha Kadi kwaajili ya kuomba kuchangiwa kufanikisha sherehe za harusi zao.

Japo baadhi hufanya sherehe za harusi zao pasipo kuomba michango Kwa ndugu/jamaa na marafiki. Wao hugharamia Kila kitu wao wenyewe na hao ndugu/jamaa na marafiki hupewa Kadi za mwaliko kuweza kuhudhuria sherehe tu.

Kwa utafiti usio rasmi, sherehe za harusi hupendwa zaidi na Wanawake kuliko Wanaume. Wanaume wako tayari kufunga Ndoa za kimya kimya lakini sio Wanawake.

Je ulitumia fedha kiasi gani kufanikisha harusi yako ama umepanga kutumia fedha kiasi gani kwaajili ya harusi yako na mwenzi wako?

Binafsi, nilitumia kiasi cha shilingi milioni 10 kuweza kufanikisha harusi yangu na Bibi yenu miaka kadhaa iliyopita 🤗🙏

Sikuhitaji kuchangiwa fedha kufanikisha sherehe ile, bali niliweza kujipanga mwenyewe Kwa muda wa miaka 5.

Nilifungua akaunti maalumu Benki (Fixed deposit account) ambayo nilikuwa nina ruhusiwa kuweka fedha pasipo kutoa Kwa muda wa miaka 5 hivi, japo nilikuwa napata interest kidogo za Benki.

Baada ya miaka 4 hivi, nilikwenda kuchungulia fedha nikakuta nina milioni 9.35 so nikaanza maandalizi kujiandaa na harusi Mwaka unaofatia.

Mind you, tayari nilikuwa nina Cheti cha Ndoa ya Serikali na mwenzangu lakini yeye Kiu yake ni lazima tukafunge ile ya Kanisani 🙌

Kuna wakati nilikuwa nafanya biashara ya kununua na kuuza mazao ya nafaka. Nilikuwa naenda Mashambani, nawakopesha fedha Wakulima then wakati wa mavuno nilikuwa naenda kukusanya mazao hasa zao la Mpunga.

Kwahiyo kwenye ile harusi, sikuwa na hofu ya Chakula maana tayari nilikuwa nina stock ya magunia ya kutosha ya Mpunga.

Wanasema harusi ni kula na Kunywa. Kwahiyo nilijiandaa kwenye eneo hili.

Kwenye upande wa Chakula niliandaa wali mweupe,Pilau, chips, mtori, nyama za kukaanga, kachumbali

Vinywaji niliandaa Soda na Maji tu.

Niliandaa Kadi za Mwaliko za watu 300 lakini walifika watu 358 japo hili nilijua lazima lingetokea maana harusi yenyewe niliifanyia Kijijini kwahiyo wengi ni wale watu mnajuana. Kwahiyo niliweka chakula na Vinywaji Kwa zaidi (excess budgeting)

Pamoja na Wageni waalikwa, usiku ule nilikuwa na Mchungaji pamoja na Mwinjilisti ambao walishiriki kuanzia mwanzo wa harusi hadi tunamaliza tukio majira ya saa 9 usiku.

Gharama za mavazi za Wapambe niligharamia mwenyewe kuanzia mavazi ya Kanisani hadi Ukumbini 🙌

Niliamua kukodisha Ma-MC wawili ili kunogesha sherehe 🤗

Pete nilinunua zenye ppt ya dhahabu, kuogopa zisije kupauka.

Mchanganuo wa Bajeti yangu kufanikisha sherehe ile, nimeambatisha kwaajili ya wengine kujifunza.

Kumbukeni, hata kama umeoa bado unaweza kuja kuozesha watoto wako miaka ijayo. Baadhi yetu mnaweza kuwa Wanakamati kwenye harusi za wengine pia

Kwahiyo Harusi zitaendelea kufanyika hata baada ya kufa kwetu maana tutakuwa tumeacha Kizazi chetu kinaendelea Kuoa na kuolewa.
Shukrani Mkuu nimepata mwanga siku ya send off yangu
 
Kila kitu kilimalizikia kanisani.

Chakula caterer TZS 3,000,000/-
Vinywaji ( maji, soda, seres juice) TZS 524,000/-

Gari tulitumia letu na niliendesha mwenyewe

Mavazi Mme,Mke na wapambe TZS 2,000,000/-
Kukodi tents na meza za chakula TZS 540,000/-
Picha TZS 150,000/-

Hotelini USD 300 siku tatu, palikua na offer seaview USD 100 per night.

Kwa ufupi iligharim USD 3000.

Hapakua na michango licha ya kamanda wangu mmoja kusisitiza akanipa 150k.

Haya mambo usifuate mkumbo sana, fanya unachoweza ili mradi nyie wahusika mfurahie.

Namie ni kama mleta Uzi, zingatia kuibariki ndoa kanisani...2024

Mambo hayakua mengi, ilipomalizika ibada ya kawaida, tukaitwa mbele zoezi likakamilika kwenye Saa tisa likafuatiwa na chakula hapo hapo kanisani.

Saa mbili tunaangalia taarifa ya habari ITV.
Kufanya shughuli kwa gharama zako hata ziwe kubwa haina shida.

Shida inakuja unapochangisha watu ili ufanye jambo la gharama kubwa(kifahari), wengi unakuta hawana vipato vikubwa ila wanataka mambo makubwa na kuanza kutegemea kuchangiwa.

Hatukatai kuchangia ila tuchangie kwenye mambo ya msingi. Hivi hapa mjini kuna gharama za Saloon zinazofika hadi 500,000?
 
Mimi harusi au sherehe ya ndoa nilifanya kumfurahisha tu bibi harusi, ndugu zake na ndugu zangu hasa mzazi wa kike aliyelalamika kuwa eti amechangia wengi na yeye achangiwe.

Mimi sikuwahi kuwa na visheni ya kutumia gharama na kusulubisha watu kiuchumi eti kisa naoa.
Mahali nilitoa yote mimi, na kuwaunga mkono waliotaka hiyo sherehe nilitoa milioni 2, shera, suti ya Best waliyenitafutia, na gauni la mke wake.

Kwa sababu sikuwepo kwenye maandalizi ila kwa mujibu wa mwenyekiti wa sherehe ile walitumia kama mil 9. Niliwaongezea na michango ya wadau walionipa kama 2m nyingine
Wanaume wengi sio wapenzi wa sherehe, ni vile tunafanya kuwafurahisha wenzetu tu 🤗
 
Kufanya shughuli kwa gharama zako hata ziwe kubwa haina shida.

Shida inakuja unapochangisha watu ili ufanye jambo la gharama kubwa(kifahari), wengi unakuta hawana vipato vikubwa ila wanataka mambo makubwa na kuanza kutegemea kuchangiwa.

Hatukatai kuchangia ila tuchangie kwenye mambo ya msingi. Hivi hapa mjini kuna gharama za Saloon zinazofika hadi 500,000?
Michango ya ndoa imezidi Kwa kweli, na jamii inalalamika kimya kimya

Maana unakutana na michango mitatu ya 120k ukisema utoe yote unatoboka 360k at once 🙌
 
Niko na kadi tatu hapa ndani zinanipasua kichwa ,kadi ya hela ndogo ni laki na hamsini......nikipiga hesabu karibia laki saba inaenda kuteketea kuchangia ndoa daaah!

Kazi kwelikweli
 
Wanaume wengi sio wapenzi wa sherehe, ni vile tunafanya kuwafurahisha wenzetu tu 🤗
Kweli aisee. Mwenyewe nilitaka kufurahisha tu jamii na walikuwa wamejipanga na walifurahi kwelikweli.
Mara moja moja unaruhusu na wengine wafaudu😃😃
 
Ni kweli Mkuu, Siku hiyo hakikisha Jamii inakula wali hadi wabebe kwenye Mashati ( Prof Jay - Zali la Mentali) 🤗
 
Niko na kadi tatu hapa ndani zinanipasua kichwa ,kadi ya hela ndogo ni laki na hamsini......nikipiga hesabu karibia laki saba inaenda kuteketea kuchangia ndoa daaah!

Kazi kwelikweli
Mkuu hiyo michango ukiiendekeza unaweza kutoboka mifuko.

Kama unaletewa michango ya 700k si balaa hilo 🙌
 
Back
Top Bottom