Intelligent businessman
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 31,913
- 65,514
Ndo uta elewa Sasa 🤓🤣, kingine mi ni future b so wekeza 🤓Kwan tupo zama za mawe kaka 😂
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo uta elewa Sasa 🤓🤣, kingine mi ni future b so wekeza 🤓Kwan tupo zama za mawe kaka 😂
Sawaa future Billionaire😃Ndo uta elewa Sasa 🤓🤣, kingine mi ni future b so wekeza 🤓
Naam NaamSawaa future Billionaire😃
mkuu wana kamati wanapigaje kama hutojali unisaniue mapema ninatarajia mwezi wa sita kubariki ndoa.Nakumbuka tu nilipigwa vibaya mno na kamati.
mkuu nipe A,B,C za kudhibiti wanakamati kama C.A.G natarajia kufanya hii shughuli siku sio nyingi.Kamati usipokuwa makini zinapiga hela ndefu tu
Mimi nilishtuka, nikawa naenda mwenyewe front japo Wanakamati walimind 😅
Wazo zuri sana! Sio wadada wa siku hizi,unapewa budget hadi unataka kulia:....... Washikaji unawabana kwenye michango hadi uswahiba unakufaSitofanya sherehe ya harusi...
Gauni langu nataka liwe zuri sanaaa... nipige picha za ukumbusho nikitoka kanisani
Baada ya kanisani kila mtu akale kwao!
Bajeti iwe shirikishi lakini Kila manunuzi uhusike mwenyewe, Kwa maana yasifanyike manunuzi bila wewe mwenyewe kuhusishwa na ujiridhishe kabisamkuu nipe A,B,C za kudhibiti wanakamati kama C.A.G natarajia kufanya hii shughuli siku sio nyingi.
Nimependa ulivyofanya bajeti rahisi, hutaki baada ya harusi mbaki na Madeni 🤗Harusi ml 9 zanini??
Mie mume wangu namvalisha zile nguo za kiafrika 150k wapo wawli laki 3 . Gari zinakuwa 3 tu bwana harusi na bwana harusi , na wasimamizi , .
tunapewa na marafiki ,
ingine kanisani tunaomba wanakwaya na wazee arusha, baba na mama wa upande wa mzee, mama na dada upande wangu, mwanasheria wangu, na mkewe . Kwao pia baadhi wawe 4 waheshima.
Ukumbi hakuna tunaomba meza kadhaa kwa ajili ya chakula baada ya harusi, bufee 6 tu ndio tutalipia yenye vyakula mablimbali na vinywaji kama shampaigne na keki , basi tunakula .
Gharama ni honeymoon basi. hakuna cha send off . Wala kitchen party namuaga nani waste of time.
BAjeti yangu ya harusi 2 ml . Ukitoa gauni na kupambwa 1 ml basi maana gauni langu litakuwa simpe tu . Pete hiyo sasa ndio siri yetu. So total balance ya harusi ni 3ml kwa mahitaji yote toa pete
Ndioo madeni na hali hii ni mbaya sanaNimependa ulivyofanya bajeti rahisi, hutaki baada ya harusi mbaki na Madeni 🤗
Mnakuwa na harusi simple tu 🥂
Halafu harusi kubwa mnajishaua tu watu hawapendi sio kila mtu anapenda unaolewa etiUtakuwa umefanya vizuri Mjukuu
Jitahidi umsaidie mwenzako kwenye hilo🤗
Ni kweli sio wote wanapenda harusi kubwa but ni ukweli kwamba Wanawake mnapenda sana harusi kubwa.Halafu harusi kubwa mnajishaua tu watu hawapendi sio kila mtu anapenda unaolewa eti
Sipendagi kujionyeshaNi kweli sio wote wanapenda harusi kubwa but ni ukweli kwamba Wanawake mnapenda sana harusi kubwa.
Harusi zenye bajeti kubwa, hadi baada ya harusi unakuta Bwana harusi ana madeni ya 10M na zaidi 🙌
Kama wewe sio mmoja wapo, tukupe hongera zako Mjukuu 🤗
HahahaSuala la Kuoa ama kuolewa bado litaendelea kuwa ni hitaji muhimu miongoni mwa Jamii ya watu wengi Ulimwenguni.
Kwa Tanzania, tunazo Ndoa za aina mbalimbali ambazo zinatambulika kisheria ambazo ni Ndoa za Kidini, Kimila na Kiserikali.
Mara baada ya kufunga Ndoa, maharusi wengi Kwa kushirikiana na jamii zao, hupenda kufanya sherehe. Sherehe hizo huambatana na michango Kwa walio wengi kupitisha Kadi kwaajili ya kuomba kuchangiwa kufanikisha sherehe za harusi zao.
Japo baadhi hufanya sherehe za harusi zao pasipo kuomba michango Kwa ndugu/jamaa na marafiki. Wao hugharamia Kila kitu wao wenyewe na hao ndugu/jamaa na marafiki hupewa Kadi za mwaliko kuweza kuhudhuria sherehe tu.
Kwa utafiti usio rasmi, sherehe za harusi hupendwa zaidi na Wanawake kuliko Wanaume. Wanaume wako tayari kufunga Ndoa za kimya kimya lakini sio Wanawake.
Je, ulitumia fedha kiasi gani kufanikisha harusi yako ama umepanga kutumia fedha kiasi gani kwaajili ya harusi yako na mwenzi wako?
Binafsi, nilitumia kiasi cha shilingi milioni 10 kuweza kufanikisha harusi yangu na Bibi yenu miaka kadhaa iliyopita 🤗🙏
Sikuhitaji kuchangiwa fedha kufanikisha sherehe ile, bali niliweza kujipanga mwenyewe Kwa muda wa miaka 5.
Nilifungua akaunti maalumu Benki (Fixed deposit account) ambayo nilikuwa nina ruhusiwa kuweka fedha pasipo kutoa Kwa muda wa miaka 5 hivi, japo nilikuwa napata interest kidogo za Benki.
Baada ya miaka 4 hivi, nilikwenda kuchungulia fedha nikakuta nina milioni 9.35 so nikaanza maandalizi kujiandaa na harusi Mwaka unaofatia.
Mind you, tayari nilikuwa nina Cheti cha Ndoa ya Serikali na mwenzangu lakini yeye Kiu yake ni lazima tukafunge ile ya Kanisani 🙌
Kuna wakati nilikuwa nafanya biashara ya kununua na kuuza mazao ya nafaka. Nilikuwa naenda Mashambani, nawakopesha fedha Wakulima then wakati wa mavuno nilikuwa naenda kukusanya mazao hasa zao la Mpunga.
Kwahiyo kwenye ile harusi, sikuwa na hofu ya Chakula maana tayari nilikuwa nina stock ya magunia ya kutosha ya Mpunga.
Wanasema harusi ni kula na Kunywa. Kwahiyo nilijiandaa kwenye eneo hili.
Kwenye upande wa Chakula niliandaa wali mweupe,Pilau, chips, mtori, nyama za kukaanga, kachumbali
Vinywaji niliandaa Soda na Maji tu.
Niliandaa Kadi za Mwaliko za watu 300 lakini walifika watu 358 japo hili nilijua lazima lingetokea maana harusi yenyewe niliifanyia Kijijini kwahiyo wengi ni wale watu mnajuana. Kwahiyo niliweka chakula na Vinywaji Kwa zaidi (excess budgeting)
Pamoja na Wageni waalikwa, usiku ule nilikuwa na Mchungaji pamoja na Mwinjilisti ambao walishiriki kuanzia mwanzo wa harusi hadi tunamaliza tukio majira ya saa 9 usiku.
Gharama za mavazi za Wapambe niligharamia mwenyewe kuanzia mavazi ya Kanisani hadi Ukumbini 🙌
Niliamua kukodisha Ma-MC wawili ili kunogesha sherehe 🤗
Pete nilinunua zenye ppt ya dhahabu, kuogopa zisije kupauka.
Mchanganuo wa Bajeti yangu kufanikisha sherehe ile, nimeambatisha kwaajili ya wengine kujifunza.
Kumbukeni, hata kama umeoa bado unaweza kuja kuozesha watoto wako miaka ijayo. Baadhi yetu mnaweza kuwa Wanakamati kwenye harusi za wengine pia
Kwahiyo Harusi zitaendelea kufanyika hata baada ya kufa kwetu maana tutakuwa tumeacha Kizazi chetu kinaendelea Kuoa na kuolewa.