Ulitumia mbinu gani kumfanya Mtoto wako aache kulala chumbani kwako?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Hebu naomba mnisaidie hapa jaman ili niweze kuwahamisha hawa Watoto chumbani kwangu (Miaka 4&2). Imekuwa vita ya muda mrefu sana hawataki kulala kwenye Chumba chao, wanalazimisha kuendelea kulala kwangu

Hata nikisubiri walale halafu niwahamishe wakishtuka kwenye zoezi la kuhamishwa mtanange unaanza upya, walalia kama ndio wanakufa siku hiyo πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Wenzangu mlifanyaje kwenye hili?
 
Baba yao iko wapi?
 
Mnawadekeza sana watoto.
Ni kuwakunjia tu sura na kuwaambia ni marufuku kulala chumbani kwangu. Watoto wanaelewa.
Huyo wa miaka minne akielewa basi na mdogo wake ataelewa taratibu.
 
Lala nao chumbani kwao, wakisinzia toka nenda kwako
 
Mtoto wa miaka 4 alitakiwa awe ameshazoea, kisha wa miaka 2 kama ameacha kunyonya unakuwa unampeleka kwa mwenzie akipata usingizi..

Mtoto wa miaka 4 anapaswa uwe umeshamfundisha kwamba kile ndo chumba chake na kitanda chake, awe anajua muda wa kulala, ukimpa maelekezo kalale aende willingly.

Mtoto anafundishwa akiwa bado mdogo, ila haujachelewa anza sasa.

Siku za kwanza kwanza atalia sana, lkn ndo kukua kwenyewe, mzazi unapaswa uweke boundary kwa mtoto, ukisema no mtoto ajue hapa kimeumana, siyo kuwadekeza dekeza tu kwa kuogopa kuwaliza.
 
Sisi wengine hatuna ushauri maana hicho chumba cha pili hakipogo
 
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…