Ulitumia muda gani kupata mtaji wa milioni 3 kwa kutumia mshahara wako?

Ulitumia muda gani kupata mtaji wa milioni 3 kwa kutumia mshahara wako?

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Naam tuachane na ile mambo ya kukopa. Tuchukulie ile akiba kidogo inayoweka kutokana na mshahara wako tu unaolipwa kama umeajiriwa.

Uliweza kutumia miezi, miaka ama decade ngapi kupata mtaji wa Tshs. Milioni 3?

Mjadala huu utasaidia waajiriwa wengi kujijua wapo kwenye hali gani kulingana na mishahara yao.

Haya karibuni.
 
Hii saving ni nzuri sana maana mimi nilipima nikajiuliza kama nakopa lakini maisha yanenda kwa nini nisijiwekee tabia ya kusave kiasi sawa na makato ya bank

Ila unatakiwa ufungue account tofauti na ile ya mshahara ambayo masharuti yake ni kama ifuatavyo.

1. Mshahara ukitoka kabla ya kufanya chochote toa pesa moja kwa moja kwa wakala unaiweka kwenye hiyo saving account yako.

2. Simu banking iwe ya kupata taarifa pesa imeingia au kutoka tu. Pia hiyo sms ikiingia ifute ili usiwe unajiwekea kumbukumbu ya pesa ulioyonayo .

3. ATM card ifungie kabisa kwenye kabati ili usije kupata dharura kubwa ukataka kuitoa .

4. Ukiwa na shida usije fikiria hata siku moja kuwa una pesa kwenye account tumia account yako kama unakomba pesa chota yote.

5. Usijiwekee mawazo kuwa utasave Mshahara tu hata ukipata pesa yoyote tenga kiasi kidogo angalau kuanzia asilia 10.

6. Usiwe unaiwazia hiyo pesa kwa kitu chochote.

Mimi nimeanza toka mwaka jana matokeo nimeyaona na nikajilaumu sana kwa kuwapa mabenki pesa .

Mwisho uwe na moyo wa uvumilivu sana

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom