Ulitumia muda gani kupata mtaji wa milioni 3 kwa kutumia mshahara wako?

Ulitumia muda gani kupata mtaji wa milioni 3 kwa kutumia mshahara wako?

Niliingia kwenye mchezo wa kupeana pesa sh 300000 kwa mwezi tulikuwa 5 ..mzunguko wa kwanza nlikuwa mtu wa mwisho kupokea..mzunguko wa 2 nikawa wa kwanza kupokea hivyo nkawa nimeipata ndani ya miezi 6..nlifungua biashara ambayo bado naendelea nayo kwa zaidi y miaka 5 sasa imenisaidia sana.
 
Usiwaze ivyo hapa utapigwa chenga Kun Wana wanaipata zaidi ya hyo kwa mkupuo sema Bata lake usiwaze kinaanza ijumaa ..Bongo hapa vijana wanapataga sana kila mwezi zaidi ya mil 3 Sema labda saving maana hapo Kuna mafuta gari unakuta harrier na inazunguka siku Saba zote ukiachana na tano za kazini mbili wanaenda vijana wakifika mfano bagamoyo anakodisha hotel,,Kuna Wana wako Moro ila Bata zao zipo dar wanakuja kama wako mtaani tu ijumaa wako hapa jumapili wako Moro kupiga kazi.

Kusave na kupata tofauti kwa kupata watu wengi wanaipata ila kusave ndo balaa lingine. Kuna familia ishu kusomesha kodi ya mexa daily ,mke nae matunzo nguo mara kusuka vilaki laki vinakutoka
 
Naam tuachane na ile mambo ya kukopa. Tuchukulie ile akiba kidogo inayoweka kutokana na mshahara wako tu unaolipwa kama umeajiriwa.

Uliweza kutumia miezi, miaka ama decade ngapi kupata mtaji wa Tshs. Milioni 3?

Mjadala huu utasaidia waajiriwa wengi kujijua wapo kwenye hali gani kulingana na mishahara yao.

Haya karibuni.
Uzi wa kiwaki maana mishahara haifanani sijui unataka kujua nn, Kuna watu hiyo 3m anai save kwa mwezi mmoja
 
Uzi wa kiwaki maana mishahara haifanani sijui unataka kujua nn, Kuna watu hiyo 3m anai save kwa mwezi mmoja
Sawa una gross ya 4m

Statutory deduction? Mikopo? Madeni? Wategemezi? Bata zako?

Point yake iko sawa tu
 
Hii saving ni nzuri sana maana mimi nilipima nikajiuliza kama nakopa lakini maisha yanenda kwa nini nisijiwekee tabia ya kusave kiasi sawa na makato ya bank

Ila unatakiwa ufungue account tofauti na ile ya mshahara ambayo masharuti yake ni kama ifuatavyo.

1. Mshahara ukitoka kabla ya kufanya chochote toa pesa moja kwa moja kwa wakala unaiweka kwenye hiyo saving account yako.

2. Simu banking iwe ya kupata taarifa pesa imeingia au kutoka tu. Pia hiyo sms ikiingia ifute ili usiwe unajiwekea kumbukumbu ya pesa ulioyonayo .

3. ATM card ifungie kabisa kwenye kabati ili usije kupata dharura kubwa ukataka kuitoa .

4. Ukiwa na shida usije fikiria hata siku moja kuwa una pesa kwenye account tumia account yako kama unakomba pesa chota yote.

5. Usijiwekee mawazo kuwa utasave Mshahara tu hata ukipata pesa yoyote tenga kiasi kidogo angalau kuanzia asilia 10.

6. Usiwe unaiwazia hiyo pesa kwa kitu chochote.

Mimi nimeanza toka mwaka jana matokeo nimeyaona na nikajilaumu sana kwa kuwapa mabenki pesa .

Mwisho uwe na moyo wa uvumilivu sana

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Safi sana mkuu, sema km umeweza kufuata hayo masharti yote uliyoandika basi upo vizuri sana
 
Niliingia kwenye mchezo wa kupeana pesa sh 300000 kwa mwezi tulikuwa 5 ..mzunguko wa kwanza nlikuwa mtu wa mwisho kupokea..mzunguko wa 2 nikawa wa kwanza kupokea hivyo nkawa nimeipata ndani ya miezi 6..nlifungua biashara ambayo bado naendelea nayo kwa zaidi y miaka 5 sasa imenisaidia sana.
Wow
 
Back
Top Bottom