Ulitumia njia gani kuishi kwa mtu bila kukuchoka?

Me nilikuwa naamka mapema mtoto wa kiume nawapikia chapat za maji watoto na wazazi walikuwa wanazipenda balaa plus naziweza kupika na viungo vyote.... Nikimaliza napika tena sup wakiamka wanakuta supu tayari wanakunywa na chapat juu...
 
Maisha yako unaishi kama unajimudu sasa unaishije maisha yako wakati umejipeleka kuomba msaada kwenye maisha ya watu wengine. Uwepo wako pale ushawabadilishia mfumo wao wa maisha so na wa kwako lazima uadjust mwende sawa.
Ni kwel kma yupo kwa mtu inabdi awe mbwa tu
 
Hiyo uliyofanya wewe ni mgeni njoo mwenyeji apone.

Sehemu yeyote kinachofanya mtu achokwe ni kujipweteka na kuongezea wenyeji mzigo.

Huna uwezo pesa basi jitoe hata kusaidia shughuli za nyumbani. Unakuta jitu lipo ugenini linaweka miguu juu kuangalia tv asubuhi mpaka jioni. Likila hata kutoa vyombo haliwezi. Sasa jitu kama hilo usilichoke kwanini.
 
Kuishi kwa mtu au kwa watu sio poa nishalala pale mbagala bus terminal mara kibao nilikuwa nafanya kazi za shift sasa ikifika ile shift ya kutoka usiku nikifika nimefungiwa mlango nyumba ina geti huwezi kuruka narudi mbagala rangi tatu mpaka asubuh ndio naenda nilikuja kuhama nikatafuta chumba changu baada ya mda maana nilikuwa ndio nimeanza kazi sikuwa na hela za kulipia siwezi sahau nilivyopata hela kitu cha kwanza nikanunua kiwanja.
 
Anataka ahudumiwe sawa na mume wa nyumba,binafsi nimewazoesha watoto kuondoa sahani wanapomaliza kula,hata baba yao hukuti kala kaachwa sahani mezani..nkapata mgeni kiazi hatoi sahani wala kikombe alicholia hata kama kala peke yake mezani,baada ya kuona hata fadha Hausi anabeba chombo alicholia kupeleka jikoni alikuwa akimaliza Kula anshkilia kikombe mkononi hadi umpokelee.. hawa ndo wageni mizigo wanapewa chumba banda la uani still anataka afanyiwe usafi chumbani kwake mpaka choo chake peke yake..uzwazwa kabisa huu
 
Jichanganye Sasa vile umetoka ukirudi tu unawakuta wanaongea Ile umefika tu wewe wakikuona tu wote wanakaa kimya... Hata kuanza kuondoka eneo lile au sebuleni mmoja mmoja...
Hapo Ndugu yangu ondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…