Uliwahi ku-date na mtu wa aina hii?

Good Father

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
10,321
Reaction score
18,574
Kwa ufupi sana, niliwahi kudate na mwanamke flani miaka ya nyuma mkoa flani sitautaja.

Tukapotezana kwa maana ya kuonana, ila mawasiliano yalikuwepo kwa simu. Juzi kati amekuja mjini kwa biashara zake, kaniahidi tutaonana kweli kafika tukaonana ilikuwa jioni sana.

Tukapata msosi tukaelekea location, sasa katika mazungumzo nikamwambia siwezi kufanya chochote kwa sababu ni muda kidogo hatujaonana.

Hata kama tutatumia kinga lakini ni vema tujue afya zetu kwa sababu kuna emergencies za kinga kupasuka, kinga kuvaliwa vibaya bila kujua au wakati wa kutoa kinga bahati mbaya ukawa contaminated.

Hapo ndio nilitonesha kidonda kilichoanza kupona, mjumbe kanikatalia katukatu hawezi kupima, niliona kama utani vile alivyokuwa akinikomalia kuonana namimi nikajisemea atalegeza tu, mpaka inafika 2 usiku kakaza, nikamwambia sili mzigo bila kipimo basi tumelala hadi asubuhi sijamgusa hakuamini kama fisi anaweza kulala na mbuzi buchani.

Asubuhi ya leo nimemwambia business iishe, huwezi kuamini ameunga mkono hoja.

Moral of the story: Uhai ni muhimu sana usibweteke na starehe ya sekunde moja


 
Hiyo inaitwa escape from Sorbibor, wako wa hivyo,inawezekana hana ila anataka apate utamu bila kuwazia madhara yake au inawezekana ameathirika hivyo haoni sababu ya kuendelea kukosa utamu, kwahiyo hajali hata wewe akikuambukiza.Kifupi tuache zinaa kwani haijawahi kumuacha mtu salama.
 
Bila shaka baada ya kuachana na wewe yupo kwenye relationship na mtu mwingine.
Kama mtu yupo kwenye relationship hata kama umejitunza ni ngumu kuamini kwamba na partner wako anajitunza. Kitendo cha kuwa kwenye mahusiano basi uhakika na afya yako ni mdogo sana.

Halafu atakuwa amewaza, akipima ikitokea majibu yakiwa mabaya, bado hamta-sex na bado utakuwa unaijua siri yake. Na itamuumiza sana ,akaona basi bora aache, na nyie sio wapenzi tena.

Lakini yeye kukataa kupima haimaanishi anaumwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…