Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Kumbe tunapoona washikaji wanatusua sana Bar wanachafua meza kumbe kesho yake huwa wanaamka na homa.😅😅😅
 
Ngojaa na mie niweke Kamkasa ila yangu ipo tofauti kdg

Kuna Manzi nilimkubali sana (Ktk WhatsApp status) nikaomba namba Nikapewa.

Nikaanza Urafiki nae tu huku nikijifanya sina kazi wala sina mishe yoyote town., Manzi ni mtu wa bata sana nikaw namchora tuu basi bhana

Mwezi wa 12 Siku ya Mkesha wa Mwaka mpya, nikamchek ile kumuuliza anasema yupo Wavuvi Camp.. Mie nikasema huko sipawezi nipo maeneo ya Kino kama utaweza njoo tuonane.

Basi.. Time ikasonga mishale ya saa 8usiku Manzi kanivutia waya upo wap? Nikatuma location dk 15 Manzi kafika na mwenzie mmoja.. Nikaona sio kesi nikawaambia agizeni (muda huo napiga zangu Krest ya buku) rafik yake akaagiza Jack daniels sijakaa saw ikaagizwa Absolute Vodka.. Sijakaa sawa ikapigwa simu Manzi anawapokea rafik zake wengine aliokuw nao kule..

Jumla wakaja kama 6 hivi na mie wa 7 nikaagiza Redblue wale wengine wakagoma kinywaji wakataka Shisha.. Nikavuta shisha mbili 20-20.. Kuchek saa naona saa 10 na bado wanaagiza tu vitu hovyo hovyo.

Basi.. Mie sikutaka mambo mengi nikamuita waiter aje na Bill na Mashine ya kulipa kwa card, nikalipa almost 350k within 2hrs.

Basi after kulipa nikaomba ruhusa niwahi home maana nina Mishe ya muhim asubuh sana., Manzi hakutegemea kama ningekuw na uwezo ule, hakutegemea physical appearance yangu, maana sikuwah mtumia picha. Hakutegemea the way nilivyo humble.. Mwisho nikatoka nje akanisindikiza akaona na Chuma nachosukuma ndio akawa hoi.

Tukaagana pale mie nikajipindua..

Mpk leo sijahangaika nae kuomba Papuchi san san analazimisha yeye nimle lkn mwamba walaaa sina time. Na mwendo ni ule Ule wa kujishusha..
 
Hapo Zamani Nalikua na Utaratibu Nikikutana na Mwanamke amevaa hayo Majuba yenu nakomaa nae hata iwe kavaa kininja nalikua Nacheza Bahati Nasibu, Na kwa Bahati Iliyo njema sijawahi Kukutana na mbaya [emoji3][emoji3]
Muone[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],una roho ngumu
 
Kwenye ATM ukatoa 1.5m. ATM ya bank gani hiyo?
 
dakika 90 hazijaisha 250K imeisha.... Punguzeni chai madogo
 
Hebu msinikumbushe machungu mimi😪😪kwa kawaida mwanaume kamili anakua na kile kiburi cha asili sasa kujimwambafai kupo humo humo kwenye kiburi cha asili, nilipata pisi moja ya kisukuma balaa imepanda hewani trako hiloo jicho kama anacum hivi balaa yani basi nilienda na swaga za kinyonge sana demu akaingia kingi tatizo likawa ni shoga yake na yule demu ananipondea balaa balaa yani khah!! Basi siku hiyo nina ka laki mbili na nusu kangu mfukoni wakataka niwatoe outs kwa mtego tu nami nikavimba kuwapeleka bagamoyo maaaayooooweeee😂😂😂 ndani ya masaa matatu kahela kameisha mpaka nikaomba msaada kwa mwana akanitumia mia mbili tena,hapo yule rafiki yake demu wangu haamini mpaka aibu anaona jinsi ninavyochana wallet kuuumbee,basi nikala mzigo swafi ila kesho yake niliumwa kichwa kwa mawazo helq zaanguuuu uuuwiii
 
Safi sana. This was worth it
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Nimecheka saaaaana
 
Kweli ninyi wote ni wife
 
Jana nimeingia salon moja kali sana, ikabidi niulize bei ya kunyoa nikaambiwa 7,000/-. Nilitaka kukimbia ila nilipoangalia zile pisi mle ndani ikabidi nivimbe Nika nikanyoa nikalipa 7000 nikabakiwa na 3000/- siku ikaisha.
Hizi saloon ukiendekeza mabinti mmm

Sinza Nishawahi lipishwa 35,000

Kunyoa ni 5,000 tu alafu

Ila kale kachumba kaliniduwaza na vihuduma vya ajabu ajabu nikaacha hela wakati nilikuwa nimefulia weekend hiyo na kubaki na 5000 tu mfukoni


Sahizi nkiona jina barbershop siingii nikiona Saloon ndio naingia😹

Alafu wanampa jukumu mdada ndio akudai hela zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…