Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Wakati fulani mwaka juzi nikawa na safari ya kikazi Musoma. Sikuwahi kufika Musoma kabla kwa hiyo sikuwa mwenyeji wa maeneo nilitegemea boda.

Nikashuka stend nikamwambia boda nipeleke lodge nzuri nzuri. Baadae nikaona nisichemke ngoja nimshirikishe mwenyeji wangu. Mwenyeji wangu sikuwa nafahamiana naye wala kuonana. Kwa vile alijua ile kazi ni ya kibosi sana akaamini natakiwa kulala hotel yenye hadhi. Akamwelekeza boda pa kunipeleka.

Kufika daaah, nakuta hotel kali ghorofa kadhaa. Nje napokelewa na mabendera ya nchi mbalimbali.

Nikamwambia bodaboda mmenileta cha kike. Muhudumu mrembo kabisa akaja kunipokea nikiwa mchafu vumbi na kabegi mgongoni kama nimetoka kuchimba mitaro.

Nikamwambia boda usiondoke lolote linaweza kutokea. Tayari muhudumu akawa amenihukumu kwamba sina uwezo wa kulala pale. Akaniambia lakini kaka hapa chumba ni kuanzia elfu 50!

Nikamwambia mimi sijauliza bei nimeuliza chumba. Kufika reception kila mtu anaonyesha wasiwasi huyu mteja kapotea. Basi nikamwambia nataka chumba cha juu.

Akanijibu tuangalie tu vya chini kule juu ni kuanzia elfu 70. Nikaona aaaahhhh japo nilitaka chumba cha 20 ila hapa inabidi niweke heshima tu bila kujali chochote.

Nikachukue chumba cha 70. Nikarudi mapokezi kwenye watu wengi walionitilia mashaka. Nikaanza kulipa bills kwa sauti.

Nikawaambia sikilizeni, ninakaa siku 2 nitalipa 140,000 yote, halafu dada chukua buku 10, mlipe boda buku ya nauli na buku 4 ya kunisubiri. Halafu elfu 5 baki nayo umenipokea vizuri nimepenta, lakini mwambie boda naomba namba yake.

Ndugu msomaji yote hayo niliyafanya kulinda heshima dhidi ya wajinga wachache ambao walinihukumu kwa mwonekano.

Lakini pia kujitabiria mambo makubwa mbeleni kwamba ipo siku nitakaa meza moja na wakuu, nitakula na wakuu na nitalala lodge moja na wakuu.

Je, ulishawahi kufanya jeuri ya pesa hata kama huna kingi, ili kulinda heshima yako au kujitabiria ukuu?!!
What an ego trip
 
Kuna restaurant moja katikati ya mji Dar huwa mara kadhaa napenda kunywa chai jioni,sasa baadhi ya wahudumu wakawa wamenizoea na kunichukulia poa, yaani nakaa muda kusubiri mtu wa kunihudumia.

Sasa kukawa na meneja mpya anayewasimamia hao wahudumu akawa anamuelekeza muhudumu aje anisikilize.Kwa mbali nilinote yule muhudumu alichomwambia yule meneja wake kwamba yule ataagiza chai ya rangi tu (siko vibaya ktk kuisoma non verbals),hivyo alivyokuja nikambadililkia nikamwambia nahitaji wali samaki ambao bei yake ni 10,000. Muhudumu akaanza kujichekesha Kwa aibu akiuliza"kwani Leo hunywi chai" ,nikamwambia sihitaji chai.

Kifupi aliabika mbele ya yule aliyemuaminisha kuwa nitaagiza chai tu ,pia nilipoondoka niliacha tip nzuri tu ili kumfunza awe na heshima.
Jamani
 
I have made a covenant with myself, never to spend money on impulse, just to prove a point to any human being. It's just absurd, crude, diabolical and bad economics....

What's there to prove, wakati najua mfuko u hali gani!!! Binafsi nafahamu even if you have all the money in the world, there will be some fools lurking somewhere ready to smack faeces on your good image.

Heri unione bahili, mchoyo au sina pesa, lakini binafsi nafurahia maisha yangu kinoma. Kuna umri ukifika baadhi ya mambo hayakuumizi sana kichwa....
Maana yake huu uzi haukuhusu. Pita hivi 👉 na Kingereza chako.
 
Wakati fulani mwaka juzi nikawa na safari ya kikazi Musoma. Sikuwahi kufika Musoma kabla kwa hiyo sikuwa mwenyeji wa maeneo nilitegemea boda.

Nikashuka stend nikamwambia boda nipeleke lodge nzuri nzuri. Baadae nikaona nisichemke ngoja nimshirikishe mwenyeji wangu. Mwenyeji wangu sikuwa nafahamiana naye wala kuonana. Kwa vile alijua ile kazi ni ya kibosi sana akaamini natakiwa kulala hotel yenye hadhi. Akamwelekeza boda pa kunipeleka.

Kufika daaah, nakuta hotel kali ghorofa kadhaa. Nje napokelewa na mabendera ya nchi mbalimbali.

Nikamwambia bodaboda mmenileta cha kike. Muhudumu mrembo kabisa akaja kunipokea nikiwa mchafu vumbi na kabegi mgongoni kama nimetoka kuchimba mitaro.

Nikamwambia boda usiondoke lolote linaweza kutokea. Tayari muhudumu akawa amenihukumu kwamba sina uwezo wa kulala pale. Akaniambia lakini kaka hapa chumba ni kuanzia elfu 50!

Nikamwambia mimi sijauliza bei nimeuliza chumba. Kufika reception kila mtu anaonyesha wasiwasi huyu mteja kapotea. Basi nikamwambia nataka chumba cha juu.

Akanijibu tuangalie tu vya chini kule juu ni kuanzia elfu 70. Nikaona aaaahhhh japo nilitaka chumba cha 20 ila hapa inabidi niweke heshima tu bila kujali chochote.

Nikachukue chumba cha 70. Nikarudi mapokezi kwenye watu wengi walionitilia mashaka. Nikaanza kulipa bills kwa sauti.

Nikawaambia sikilizeni, ninakaa siku 2 nitalipa 140,000 yote, halafu dada chukua buku 10, mlipe boda buku ya nauli na buku 4 ya kunisubiri. Halafu elfu 5 baki nayo umenipokea vizuri nimepenta, lakini mwambie boda naomba namba yake.

Ndugu msomaji yote hayo niliyafanya kulinda heshima dhidi ya wajinga wachache ambao walinihukumu kwa mwonekano.

Lakini pia kujitabiria mambo makubwa mbeleni kwamba ipo siku nitakaa meza moja na wakuu, nitakula na wakuu na nitalala lodge moja na wakuu.

Je, ulishawahi kufanya jeuri ya pesa hata kama huna kingi, ili kulinda heshima yako au kujitabiria ukuu?!!
🤣🤣🤣Nilikaa ya elfu 90 kwa siku kumbe na mimi ni tajiri eeh
 
Okay mwaka fulan nimeenda kule kariakoo nimefanya biashara na mshikaji mmoja nikapata kama 2.8m, million 2 nikadeposit bank, nikapita msimbazi pale meridian nikakandamiza mkeka wa laki mbili odd ya 10, nikabaki na laki sita, sijakaa vizuri jamaa kanipigia simu njoo 5N nipo na kina lisa na huyo lisa nilikuwa namuwinda kweli nikaenda pale nikakuta kama wanasua sua, shusha sana monde, tukahamia samaki samaki ya mliman kula sana magae, laki sita nlikuwa nimeifunga kwenye rubber band na rubber band ilikuwa imekaza, nachokumbuka ni kwamba kuna muda niliingiza mkono mfukoni nikakuta ma rubber band yamepwaya yan ela zipo kivyake rubber band zipo kivyake daah noma sana, kuja kuhesabu pesa imebaki 185000 mida mibovu nna laki kamili roho ilikuwa inauma kilichofanya isiume sana nilikula ule mkeka bila vile ningetukana sana matusi aisee...
Nimecheka na niko kwenye daladala
 
Mimi ilikuwa sio kuleta heshima ila ilikuwa sifa.iko hivi nilienda dodoma kwenye harusi ya sista nilikaa meza moja na pisi kali 2 ukafika muda wa kuchangia bibi harusi kulikuwa na phase mbili,phase ya kwanza ilikuwa kikapu kinapita kwenye kila meza yoyote anaweka alichonacho'muda ule nilikuwa nipo tungi balaa kutaka kuonyesha sifa mfukoni nilikuwa na laki 8 nikawa naweka narusha rusha elfu 10 kwenye kapu mpaka laki 8 yote ikaisha.
Baadae wale wadada wakaniambia weee kaka pesa zote umetoa wapi mbona umechangia hela nyingi hivyo!! Nikawaambia kawaida kisha nikawapotezea.
Ikaja phase 2 kwenda kumtunza bibi harusi pale mbele ili kuonesha sifa nikaenda ATM nikatoa mil 1.5 pisi kali moja ikanishauri sana nisiende kuchangia tena pesa nilizotoa awali zinatosha.
Baada ya harusi kuisha asubuhi nikajikuta nipo room yenye muonekano kama hostel kumbe yule sista nilivyozima alinikokota mpaka chuoni kwao alikuwa ni mwanafunzi wa udaktari md5 akanikabidhi pesa yangu 1.5mil alizitunza coz nilikuwa tungi sana..kifupi huyo dada ndio mke wangu hivi sasa..sifa zilinisaidia kupata mke bora aliyekuwa yupo sealed
Wow
 
We uko kama Mimi Tu,unajua wakati mwingine ili kuondoa aibu ndogo ndogo ni Bora ujue bei mapema kuliko kuja kutukanwa baadae,kuna sehemu soda 1,000 kwengine 6,000 na 8,000 haya ndo umejichanganya kwenye buku 8 hlf huna hiyo hela si aibu hiyo?

Na hii nilijifunza hata Kwa wazungu huwa wanauliza bei Sana,siku moja tulitoka nao out Yani wanauliza bei fresh Tu, kwahiyo ndio nikazidi kupata hamasa ya kuuliza kabla ya huduma
Miss u
 
Ilinitokea miaka hiyo nikiwa sekondari, siku moja asubuhi(mimi na ndugu yangu) tumetoka kwa sista. Sista alikua na safari ya nairobi kwahiyo ikatulazimu turudi nyumbani mkoani kwakua alihofia kutuacha wenyewe. Tukapewa nauli na baada ya kuona hela tukaona hatuna muda wa kupoteza tukaaga mbio mbio hata chakula hatukula tuliona kitatuchelewesha.

Tukafika town tukashauriana tuingie mahali tuchambe koo na juice plus kuku kidogo then tuamshe. Tulifika na kupokelewa na pisi moja ya kimbulu kali sana(huu ndio ugonjwa wa huyu ndugu yangu mpaka kesho alafu ni mbishi akitaka jambo lake lazima liwe). Nikamnong'oneza ndugu yangu hapa bei zao sio size yetu tumevamia kambi tutafute sehemu nyingine, mwamba akagoma akasema pesa si ipo leta vitu. Nikaagiza juice, inakuja juice naona na misahani shazi, nikauliza kiuwoga nikajibiwa huwa wanauza special package(hapa tulipigwa plus ushamba). Tukaulizwa turudishe au mtakula? Ndugu yangu akaropoka tutakula mbona ni jambo dogo sana, basi tukala tukamaliza bili inakuja hatukubaki hata na nauli, tulivyotoka hapo nilikua kama bubu kimya tulitembea hadi kwa dada tulivyofika tukamwambia asijali sisi tutabaki tu hamna shida, alituelewa [emoji23][emoji23] sitosahau hiyo siku niligongwa na mvua sana.
Si wewe tu ,kuna siku mimi nikaingia hoteli fulani nikaagiza chipsi kavu na juice,bili ikaja elfu 24,yani ile chipsi kavu ya 1500 na juisi ya 1000 nikauziwa elfu 24[emoji57]
 
Si wewe tu ,kuna siku mimi nikaingia hoteli fulani nikaagiza chipsi kavu na juice,bili ikaja elfu 24,yani ile chipsi kavu ya 1500 na juisi ya 1000 nikauziwa elfu 24[emoji57]
Kwamba hukusoma MENU?
 
Ni ngumu sana kujua binadamu mwengine anafikiria nini, iwe kwake au juu yako. Kitu ambacho kila mtu anasahau ni kwamba kila mtu anajifikiria yeye mwenyewe na anafikiria jinsi gani wewe unamfikiria yeye. Na wala hakuna anayejali kuhusu wewe au unachopitia wakati huo. Ego ni ile hali ya umimi, kila kitu kinahusu mimi, kila mtu anafikiria kuhusu mimi, mimi ndio main character nk. Lakini kila mtu ana ego na ego ndio ime take over kila akili ya binadamu. Expectations za juu na kujipa thamani kubwa kwa watu yote ni sababu ya Ego.

Hivyo ulichofanya sio kwamba umebadilisha mawazo yao juu yako, bali umebadilisha mawazo yako juu ya unachodhani wao wanachofikiria juu yako, umeiridhisha Ego yako. Kwenye maisha wewe sio main character wa movie na kila mtu anakuangalia wewe bali kila mtu ni main character wa maisha yake, wewe ni side character tu ambaye yupo kwenye background, mpita njia tu kwenye movie zao. Kugundua WEWE SIO MUHIMU kwenye maisha ya wengine ni zawadi kubwa sana na level kubwa ya kujitambua itakayokufanya kuwa free maishani.

Ndio kitu kitatokea kila mtu atakiona lakini baada ya sekunde 30 kila mtu anarudi kwenye movie ya maisha yake na anaendelea kujifikiria yeye. Hivyo ni kupoteza muda na resources kujali na kujaribu kubadilisha mitazamo ya wengine.

Irony ni kwamba hata mimi nasumbuliwa na hili tatizo la ego vilevile, and its huge than usual but I'm working on it.

The power of NOW.
 
Back
Top Bottom