Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Duh ila ndugu wa mume jamani kuishi nao yataka moyo.nimekuja kugundua kwanini watu wengi wanaishi na ndugu zao kuliko ndugu wa mume.nikiishi na mdogo wangu namtuma nitakavyo hata nguo zangu nampa anifulie hutomsikia kunung'unika, ndugu wa mume mtume hata mara moja ukoo wao mzima watajua . Nako hapa naishi na wifi yangu kaachika kwa mume wake yaani ni kero jamani nyumba imekuwa kama na wanawake wawili mimi napanga kipikwe hiki yeye anapika kile mavyakula anapika mengi anaishia kumwaga yaani ilimradi fujo.hapa napanga na mimi niondoke niende kuishi kwa kakaangu
Hahahah kwahio unamkomesha wifi yako 🤣
 
Nilienda kusoma tuition nikiwa A Level, kwa kweli nikiri wazi mwanaume hakuwa na shida kabisa [emoji1787][emoji1787] lakini mwanamke alipiga stop kupewa chakula mchana lakini kisiri siri bila mme wake kujua, alisababisha nikasitisha tuition na kurudi nyumbani tu na sikurudi tena huko..
Mara nyingi wanawake ndio wana roho za choyo. Na hawapendi kujulikana hivyo kwa waume zao.
 
Mwaka 2008 kuna jamaa kama watano walikuja dar kumtembelea jamaa yao. Wawili kati yao walikuja na wake zao na mmoja alikuwa na mtoto mchanga. Jamaa aliwaribisha vizuri ila wakati wa msosi akaenda nao kwenye mgahawa wale yeye akaagiza wali magarage wageni wakaagiza wali kuku ugali mbuzi nk ilipokuja bili akalipa sh mia nane tu ya wali alio kula wageni libidi walipie walichokula baada ya hapo wakarudi tena kwa jamaa na jamaa akawa anawapigisha tu story za kuwauliza mambo ya kijijini etc ilipo fika usiku akawapeleka gesti ya bei nafuu na kuwaambia watalipia hela asubuhi.. kesho jamaa waliondoka bila kuaga. Jamaa alikuwa kauzu zaidi ya dagaa
Huyo kweli alikuwa mwamba 🤣
 
Vijana wanataka waishi kifalme waamke saa 4 Asubuhi wakute chai mezani wanywe kisha house girl atoe vyombo, wakishamaliza kunywa chai warudi chumbani kuchati wakisubiri chakula cha mchana waje waitwe na dada wa kazi.
Hahahah hii ndio sababu kuishi kwa mtu ni taabu. Sasa hapo kuna ubaya gani? Mfanyakazi si yupo we unataka mie kijana wa makamo nikija kwako nianze kuosha na vyombo🤣?

Staki kabisa habari za kukaa kwa mtu hata nikitembelea ndugu ni aheri kulala gesti tu. Unasalimia na kuondoka.
 
Sijui kama umenielewa, huyu wifi yangu katoka kwa mume wake kaja hapa kwa kaka yake kuishi.ishu inayokuja kwa mfano hapa kwangu nina ratiba ya chakula asubuhi mchana na jioni,asa utakuta ratiba yangu jioni ni kupika hiki yeye atapika kile,hafu maagizo yote hela huwa namuachia binti wa kazi lakini ukirudi ulicho tegemea kukuta sicho kuuliza ooh aunt kasema tupike hiki. Kwahiyo ni kama anataka niishi apendavyo yeye.na sio kama hivyo vingine yeye hatumii hapana anatumia ila fujo tu.hapo bado atapika sufuria kubwa la chakula kesho unakikuta kwenye dustbin.haya asubuhi ataamka atapika chai ya rangi hapa kwangu kuna bili ya maziwa bado atapika na uji🙄 sio kama anamtoto wala hanyonyeshi siku mbili kilo ya sukari kwisha. hapo sijazungumzia mafuta,huwa nanunua viazi kwaajili ya chai lakini yeye kila siku asubuhi atapika chips anywe na chai,asa nakuta mafuta hayakai vile nlivyokusudia kumuuliza dada mnatumiaje mafuta aunt anapika chips kila mara asubuhi.na sio mjamzito .sawa kwake alikuwa yeye pekeyake na mume wake huenda alikuwa anaishi hivyo lakini mimi ninafamilia na sio kama tumetusua maisha jamani mimi na mume wangu wote ni wahanga wa ajira tuko mtaani tunaunga unga tu na tumepanga bado kwanini haelewi? Kila pesa tunayoipata tunaipangilia sana
Si umchambe ukweli. Shida nini.
 
Hivi sijui kwa nini...wanawake waliotoka kwenye dhiki wakaolewa mahali penye unafuu huwa wanakuwa washenzi sana
Hahahah tabia za kiwaki hizo huwa wanaona kama umekuja kufaidi mali za mme wake. Wanasahau kwamba wale watoto wake ni ndugu zako pia 🤣 ni mambo ya ajabu sana. Nimeishigi mazingira hayo toka mdogo hadi nafikia balehe.

Nilinyanyasika sana yani hadi siku naondoka ile nyumba nilihisi nimepewa uhuru toka Gwantanamo. Mama alikuwa mnafiq na mchoyo sijapata kuona.
 
Sijui kama umenielewa, huyu wifi yangu katoka kwa mume wake kaja hapa kwa kaka yake kuishi.ishu inayokuja kwa mfano hapa kwangu nina ratiba ya chakula asubuhi mchana na jioni,asa utakuta ratiba yangu jioni ni kupika hiki yeye atapika kile,hafu maagizo yote hela huwa namuachia binti wa kazi lakini ukirudi ulicho tegemea kukuta sicho kuuliza ooh aunt kasema tupike hiki. Kwahiyo ni kama anataka niishi apendavyo yeye.na sio kama hivyo vingine yeye hatumii hapana anatumia ila fujo tu.hapo bado atapika sufuria kubwa la chakula kesho unakikuta kwenye dustbin.haya asubuhi ataamka atapika chai ya rangi hapa kwangu kuna bili ya maziwa bado atapika na uji🙄 sio kama anamtoto wala hanyonyeshi siku mbili kilo ya sukari kwisha. hapo sijazungumzia mafuta,huwa nanunua viazi kwaajili ya chai lakini yeye kila siku asubuhi atapika chips anywe na chai,asa nakuta mafuta hayakai vile nlivyokusudia kumuuliza dada mnatumiaje mafuta aunt anapika chips kila mara asubuhi.na sio mjamzito .sawa kwake alikuwa yeye pekeyake na mume wake huenda alikuwa anaishi hivyo lakini mimi ninafamilia na sio kama tumetusua maisha jamani mimi na mume wangu wote ni wahanga wa ajira tuko mtaani tunaunga unga tu na tumepanga bado kwanini haelewi? Kila pesa tunayoipata tunaipangilia sana
Pole sana ila approach nzuri ni kuongea na kaka yake. Yeye ndio anaweza kumnyoosha bila kuleta taharuki. 🤣

Maisha magumu sana sahizi kuchezea vyakula hovyo. Ila ukimsema directly bila kumjuza braza wake utaonekana unamnyanyasa au mchoyo. Elekezaneni kibingwa tu.
 
Wifi yangu mmoja aliolewa tokea maisha ya shida, alivyofika ndani yaani mbona tulijuta. Chakula kinapikwa kinawekwa chumbani. Enzi hizo nasoma, ikafika time mi nikazira msosi wa home. Siku ya siku ndio braza anashtuka eti we huwa unakula wapi maana ht nilikuwa nikiwakuta wanakula mi sijali wala nn. Nilimwambia braza muulize mkeo. Mungu si Juma wala Abdalah ubaya wa wifi ulifika mpk lwa mama mkwe na mashemeji, kiliwaka sana mpk akaachika na sasa karudi kule kule kwenye maisha yake ya taabu.
Wifi yako naye alikuwa mshamba sana. Yani mimi ni kama nimeathirika kisaikolojia mwanamke mbinafsi na mchoyo simtakagi hata kudeiti nae kwa bahati mbaya. Yani nikiona hizo dalili tu jua biashara inaisha mapema sana 🤣!
 
Ni uchoyo tu wa mtu hasa wanawake. Katika vitu ambayo sina uchoyo navyo ni vyakula
Naishi na ndugu zangu wa 5 ( watoto wa dada 3 ,wa kaka 1 na mjukui wa dada 1) . Huwa nanunua kila kitu ,kama siku hiyo hamna mboga naacha 10k. Huwa sipangii mtu muda wa kula, chakula kikipikwa kila mtu ana uhuru wa kula muda anaotaka. Na kwa muda wote huo tunaishi kwa furaha kabisa. Nilishawahi ishi na jamaa wa rafiki kwangu na sikuwahi kupangia mtu kazi etc. Utajiongeza mwenyewe ukiwa kwangu. Kwa uhuru ninaowapa, ukifika home kila kitu kipo safi. TV hata wakeshe wanaangalia watajijua wenyewe na usingizi wao. Sitaki stress ambazo hazina mashiko.
Hahahah we umeumbwa na roho safi. Kuna mtu hio tv kuangaliwa tu ni kero kwake. Atasema hata mnavuruga makochi ilimradi awape tabu tu 🤣
 
Kiufupi kama mzazi una uwezo wa kutunza mtoto wako basi Kaa naye umtunze usimpeleke kwa ndugu unless kuwepo na sababu maalumu ya kumpeleka mtoto kwa ndugu,
Vinginevyo kinachotokea n chuki baina ya huyo mtoto na ndugu.
Kukaa kwa ndugu ni Kero sana hasa upande wa wanawake Wana roho mbaya sana sitaki kusema ila yote nasemehe maisha mengine yaendelee
Yeah hili liko wazi. Mtoto atanyanyasika tu akikaa mahali ambako mwanamke sio ndugu yake. Hawezi kuwa huru lazma atasumbuliwa kihisia tu. Wanawake wengi wana roho za kishetani sana wakikaa na ndugu za waume zao. Tena hasa huyo ndugu awe na uchumi mzuri balaa huwa zito. Kwa niliyopitia staki kuja kuona mtoto wangu anakaa mahali ambapo sio kwao.

Bora tushindie mikate na chai ila sio kumpeleka kwa baba wadogo au baba wakubwa wake. Yani hata nikifa bora akae na shangazi yake tu. 🤣
 
K.u.m.am.a.m.ak.e.keeeee
ndugu wakibongo ni wase.nge tu ku.m.a.ni.na zao

1. Ukipata pesa kuzidi yeye utaambiwa unaiba.

2. Ukipata deal ya pesa utaambiwa unauza unga au jambazi.

3. Ukiwa na demu au msela kitaani utaambiwa malaya.

4. Ukijiongeza uka move ukaishi kitaani ukaacha kuishi na ndugu utaambiwa mjeuri ku.ma.ma.ma.keeee

5. Ukinunua gari ukajenga mjengo utaambiwa FREEMASONRY.

6. ukivuta sigara, kunywa pombe, unaambiwa unatumia pesa vibaya kana kwamba wao wanakulipa mshahara was.enge hao.

7. basi ukivuta bangi utaambiwa umejiunga na makundi ya hovyo. 😀😀😀😀😀😀😀😀😀

Habari za muda huu, ni siku tulivu sana hapa. Jiji la Dar es Salaam kumekucha salama, ingawa kulikuwa na upepo wa baridi sana, poleni na natumaini kila mmoja wetu ni mzima kabisa. Nawatakia kila la kheri katika pilika za kuijenga Tanzania kuwa kubwa tena, yenye amani na upendo. Twende kwenye mada.

Kuna kipindi kwenye Life cycle ya kimaisha ilinifanya nihamie kwa uncle wangu kuishi nae ili kuangalia uwezekano wa kufanya maisha. Enzi zile ndio nimemaliza masomo nipo home tu nikapata mchong huo, nilikuwa very excited sana na hili, maana nilikuwa ninavuta picha fulani hivi kabla ya kufika kwa uncle Dar.

Siku mbili baada ya kupewa taarifa ya safari nilijiandaa lakini ilikuwa ghafla sana kutokana na uchu wa safari ya kuja huku hata watu niliokuwa nawadai pesa zangu wengi niliwapotezea, kitu ninachojutia sana.

Siku ya safari ikawadia, panda nikapanda basi safari mpaka Dar, nifika mida ya saa moja hivi enzi za ubungo terminal pale, akaja mshakaji aliyekuwa anakaa kwa huyo uncle, wakanichukua freshi mpaka home.

Hapo nipo so excited na wishes nying sana how it's going to be in the up coming day's, nikachil, nikafika home. Yale mapokezi tuu yakanidropisha point. Yule mke wake alikuwa anagubu sana, nilivyofika nikaona hapa chakike.

Picha linaanza kulipokucha tunaamshwa saa kumi na moja tufanye usafi, duuhh nilichoka. Kumbe wanafuga mbwa, sehemu padogo mbwa wanajisaidia, morning ni kuzoa na kusafisha kumwaga maji, nilichoka. Ila nikajikaza kumbe bado kuna kuosha magari usiku unaamshwa uoshe, kibaya zaidi ni kila siku iwe mvua au jua.

Kibaya zaidi ni huyo mke wake alikuwa na visa na maneno ya shombo, mara hataki watu watoke nje ya geti anafunga, mara hataki watu wakae sebuleni, hata kunywa maji ya kwenye friji jau, akinunua matunda mpaka akupe yeye na atakupa wakati linaanza kuharibika ukila atakuja kuongea mpaka ujute.

Kwa kipindi kile ilikuwa ni mateso sana, sabuni ya kuogea unajinunilia, mafuta ya kujipaka pia, tulikuwa tunajitegemea kama tumepanga hata kipindi tunaenda K/Koo ilikuwa ni taabu sana.

Ilinipasa kuishi kama mtoto wa miaka kumi kushuka chini, maana ni kama sikuwa najielewa. Maana watu walikuwa wanakuja pale wanashangaa tunawezaje kuishi na hawa, hata wadogo zake na yule mama walishindwa kukaa nae, wengine walikimbia na kutoroka. Ila ndo changamoto tunazokutana nazo katika maisha ya wengi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Niliwahi kuishi Kwa ndugu. Mkewe alikuwa balaa kuamka saa 10 usiku hata kama hujui pa kwenda. Na ukiamshwa huamki unajikuta katikati ya mafuriko. Siku nyingine unajikuta wewe chini godoro liko juu yako.
Yule mama alikuwa balaa
 
Mwaka 2008 kuna jamaa kama watano walikuja dar kumtembelea jamaa yao. Wawili kati yao walikuja na wake zao na mmoja alikuwa na mtoto mchanga. Jamaa aliwaribisha vizuri ila wakati wa msosi akaenda nao kwenye mgahawa wale yeye akaagiza wali magarage wageni wakaagiza wali kuku ugali mbuzi nk ilipokuja bili akalipa sh mia nane tu ya wali alio kula wageni libidi walipie walichokula baada ya hapo wakarudi tena kwa jamaa na jamaa akawa anawapigisha tu story za kuwauliza mambo ya kijijini etc ilipo fika usiku akawapeleka gesti ya bei nafuu na kuwaambia watalipia hela asubuhi.. kesho jamaa waliondoka bila kuaga. Jamaa alikuwa kauzu zaidi ya dagaa
Alikuwa sahihi kwa asilimia 100.
Ukitaka enda kwa Mtu angalia kwanza uwezo wa mtu husika.

Angalia ratiba zake

Angalia umuhimu wa kwenda msalimia

Mtaarifu
 
Ni uchoyo tu wa mtu hasa wanawake. Katika vitu ambayo sina uchoyo navyo ni vyakula
Naishi na ndugu zangu wa 5 ( watoto wa dada 3 ,wa kaka 1 na mjukui wa dada 1) . Huwa nanunua kila kitu ,kama siku hiyo hamna mboga naacha 10k. Huwa sipangii mtu muda wa kula, chakula kikipikwa kila mtu ana uhuru wa kula muda anaotaka. Na kwa muda wote huo tunaishi kwa furaha kabisa. Nilishawahi ishi na jamaa wa rafiki kwangu na sikuwahi kupangia mtu kazi etc. Utajiongeza mwenyewe ukiwa kwangu. Kwa uhuru ninaowapa, ukifika home kila kitu kipo safi. TV hata wakeshe wanaangalia watajijua wenyewe na usingizi wao. Sitaki stress ambazo hazina mashiko.
Nyinyi ndo sababu watu kuzaa hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom