Sijui kama umenielewa, huyu wifi yangu katoka kwa mume wake kaja hapa kwa kaka yake kuishi.ishu inayokuja kwa mfano hapa kwangu nina ratiba ya chakula asubuhi mchana na jioni,asa utakuta ratiba yangu jioni ni kupika hiki yeye atapika kile,hafu maagizo yote hela huwa namuachia binti wa kazi lakini ukirudi ulicho tegemea kukuta sicho kuuliza ooh aunt kasema tupike hiki. Kwahiyo ni kama anataka niishi apendavyo yeye.na sio kama hivyo vingine yeye hatumii hapana anatumia ila fujo tu.hapo bado atapika sufuria kubwa la chakula kesho unakikuta kwenye dustbin.haya asubuhi ataamka atapika chai ya rangi hapa kwangu kuna bili ya maziwa bado atapika na uji[emoji849] sio kama anamtoto wala hanyonyeshi siku mbili kilo ya sukari kwisha. hapo sijazungumzia mafuta,huwa nanunua viazi kwaajili ya chai lakini yeye kila siku asubuhi atapika chips anywe na chai,asa nakuta mafuta hayakai vile nlivyokusudia kumuuliza dada mnatumiaje mafuta aunt anapika chips kila mara asubuhi.na sio mjamzito .sawa kwake alikuwa yeye pekeyake na mume wake huenda alikuwa anaishi hivyo lakini mimi ninafamilia na sio kama tumetusua maisha jamani mimi na mume wangu wote ni wahanga wa ajira tuko mtaani tunaunga unga tu na tumepanga bado kwanini haelewi? Kila pesa tunayoipata tunaipangilia sana