Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Chanzo Cha yote hayo ni njaa hukosefu wa chakula .

Mimi Nina kilo miatano za mchele na gunia mbili za maharage na Nina pesa za Mboga Sasa ukija kwangu kunitembelea huwezi kugombana na mtu .

Wanawake wana njaa Sana Mnabidi kulifahamu hilo Kama hauna chakula Cha kutosha usimlete ndugu ikiwa unakaa na Mwanamke ataishia kumnyanyasa Mimi nimejionea haya Mambo Nina ndugu yangu yeye anakaaga na vyakula magunia Mengi ya kutosha Sasa pale kwake ndugu wa mke na wa Mume wanakula na kusaza huwezi kuona ugomvi ukitokea Sasa njoo huku kwa Hawa sijui Mwalimu sijui nurse sijui nani huko pamoto Sana.
Inategemea, kuna wanawake hawana njaa wana chakula cha kutosha, ila ni wachoyo hatari DR HAYA LAND
 
Nilienda kusoma tuition nikiwa A Level, kwa kweli nikiri wazi mwanaume hakuwa na shida kabisa [emoji1787][emoji1787] lakini mwanamke alipiga stop kupewa chakula mchana lakini kisiri siri bila mme wake kujua, alisababisha nikasitisha tuition na kurudi nyumbani tu na sikurudi tena huko..
 
Duh ila ndugu wa mume jamani kuishi nao yataka moyo.nimekuja kugundua kwanini watu wengi wanaishi na ndugu zao kuliko ndugu wa mume.nikiishi na mdogo wangu namtuma nitakavyo hata nguo zangu nampa anifulie hutomsikia kunung'unika, ndugu wa mume mtume hata mara moja ukoo wao mzima watajua . Nako hapa naishi na wifi yangu kaachika kwa mume wake yaani ni kero jamani nyumba imekuwa kama na wanawake wawili mimi napanga kipikwe hiki yeye anapika kile mavyakula anapika mengi anaishia kumwaga yaani ilimradi fujo.hapa napanga na mimi niondoke niende kuishi kwa kakaangu
 
Tangu lin wanawake wakaelewana ndiyo mlivyo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe ulikua na kazi sasa ulikua na sababu gani kuendelea kukaa hapo?
Hata kutoka ilikuwa uncle hatak maana utaskia kila kitu kipo hapa unataka uende uishi wapi bas natulia ila yalinizid nkalazimisha kutoka kimagumashi sema doh yule mwanamke bas tu ngj nisiongee vby maana hata sjajua nan ntamuoa atakuwaje kwa ndugu zangu
 
Kwa ndugu noma sitasahau ile sauti kali na iliyojaa ulevi mkuu usiku ule nikiwa ugenini "humu ndani hakujawahi kuibiwa kitu humu wala udokozi wa mboga" hapo alileta samaki na mwanae mwenyewe akadokoa mimi hata mfupa sikulamba ila mzee yule alinishambulia indirectly ila vibay sana nilitamani ardhi ipasuke
 
Ila kuna ndugu wengine ukikaa kwao hadi raha, mm ni shahidi, mtakula wote kilichopo, mtafanya wote kazi zilizopo, watakutreat vizuri utakua kama mtoto wa hio nyumba Ulweso Ms eyes
Kuna watu wengine wapo hivyo, kwanza mimi eti kuna watoto nyumbani wakulingana na wanao akija mtu unaanza utambulisho huwa sibarikiwi kabisa, mambo yakubagua misosi mmm.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Chanzo Cha yote hayo ni njaa hukosefu wa chakula .

Mimi Nina kilo miatano za mchele na gunia mbili za maharage na Nina pesa za Mboga Sasa ukija kwangu kunitembelea huwezi kugombana na mtu .

Wanawake wana njaa Sana Mnabidi kulifahamu hilo Kama hauna chakula Cha kutosha usimlete ndugu ikiwa unakaa na Mwanamke ataishia kumnyanyasa Mimi nimejionea haya Mambo Nina ndugu yangu yeye anakaaga na vyakula magunia Mengi ya kutosha Sasa pale kwake ndugu wa mke na wa Mume wanakula na kusaza huwezi kuona ugomvi ukitokea Sasa njoo huku kwa Hawa sijui Mwalimu sijui nurse sijui nani huko pamoto Sana.
Hapana sio chakula roho tu ya mtu, mbona kuna watu wana pesa lakini hawasaidii wenye shida! Kutoa huwa ni moyo wa mtu, hujawahi ona ndugu mwenye maisha ya kawaida lakini kwake wageni hawapungui lakini mwenye uwezo wake watu wanamkwepa!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Hahahaaaa haya maisha yasikie Tu Kwa watu Mimi nilikaa Kwa uncle Kama wewe Ila nilitimiliwa usiku wa Saa sabaa tukiwa tunaishi mabibo kwenye Kota za jeshi chanzo nilipata mishe super market ya kuwa auditor wao wa muda duh shangazi yangu alilipuka Kwa kusema mbona hujasema kuwa unafukuzia KAZI kwendraaa niliumia Sana Kwa kuwa sikuwa na mshahara hata mmoja but now days mwamba alitumbuliwa pale MSD na magu yupo Kama muokota makopo
 
Mwaka 2008 kuna jamaa kama watano walikuja dar kumtembelea jamaa yao. Wawili kati yao walikuja na wake zao na mmoja alikuwa na mtoto mchanga. Jamaa aliwaribisha vizuri ila wakati wa msosi akaenda nao kwenye mgahawa wale yeye akaagiza wali magarage wageni wakaagiza wali kuku ugali mbuzi nk ilipokuja bili akalipa sh mia nane tu ya wali alio kula wageni libidi walipie walichokula baada ya hapo wakarudi tena kwa jamaa na jamaa akawa anawapigisha tu story za kuwauliza mambo ya kijijini etc ilipo fika usiku akawapeleka gesti ya bei nafuu na kuwaambia watalipia hela asubuhi.. kesho jamaa waliondoka bila kuaga. Jamaa alikuwa kauzu zaidi ya dagaa
 
Siku nshaondoka naanza life nikatoka kizungu kwa binamu.
Oven taka zote nnazo.
Dah siku wamekuja kusalimia kuna binti kalala mle ndani ana mimba.
Ikawa anhaa weh hivi tumekupa umeleta jeuri umekuja ukaoa.
Wakabeba tena vyoote🤣🤣🤣.
Wakatimua navyo.
Demu nae anasema kumbe vitu sio vyako?
Katimua,
Nikaona afadhali sasa niko huru🙌
 
Back
Top Bottom