My story, mazingira ni kijijini.
Nilihamia kwa uncle nikiwa 9yrs old baada ya home kutokuwa hapasomeki kutokana na uhohehahe wa home. Ilikuwa rahisi kwenda kwa uncle sababu nilikuwa naishi huko kwa bibi(kabla hajafariki, baada ya kufariki nilipelekwa nyumbani) ambapo mji ulikuwa mmoja kama tunavyojua vijijini kaya huwa zipo pamoja kwa asilimia kubwa.
Lengo la kwenda uncle ilikuwa ni kupata unafuu wa maisha, bila hiyana nilipokelewa vizuri ila nilipoulizwa jinsi nilivyoondoka home nilidanganya kuwa nimeondoka kwa ruhusa ila home nilitoroka, kule kwa uncle nilisema nimekuja nitakuwa nawasaidia kuchunga ng'ombe. Bila hiyana wakakubali maana walikuwa wananifahamu tangu nikiwa naishi kipindi bibi yupo hai. Wao pia walikuwa wanajua hali halisi ya nyumbani kwetu
Nature ya uncle na mkewe ni uonevu, kunyanyasa mtu yeyote asiyekuwa mtoto wao wa rika lolote anayeishi hapo, tabia hiyo inajulikana na watu wote mtaani.
Maisha yakaanza bana, kwa kuwa nilisingizia nimekuja kuwasaidia kuchunga nikaianza hiyo kazi. Nikawa napigishwa kazi nyingi sana hapo nyumbani mbali na kuchunga, nikawa kila kazi ikitokea nalazima niitwe nikaifanye hata kama ni kazi ndogo ambayo watoto wao wanaweza kuifanya, kama sipo(nimeenda kucheza kwa majirani lazima nitafutwe niinde nikaifanye, ilifikia kipindi nikawa natoka bila wao kujua ili nikacheze kwa majirani kukwepa kazi ndogo ndogo ila na wao wakawa wananiambia nisitoke maana nilikuwa natoka baada ya lunch, kumbuka hapo nikiwa sijaenda kuchunga).
Nikawa natumwa kwenda kusaga unga mashineni ila mzigo ninaoupewa ni mkubwa hadi nasota, nikiwa najikongoja nao kichwani nakutana na watu hadi wanashangaa na kusema mama fulani hafanyi vizuri anampa mtoto mzigo mkubwa, endapo ikitokea anaandaa mzigo halafu majirani wakawa pale kwenye kupiga story na akaambiwa mbona unamfungia mzigo mkubwa sana anasema sio mkubwa na huyu ni mtoto mkubwa. Watu wanabaki kumuangalia tu.
Mwaka mmoja baadae nikiwa pale nikafundishwa kuendesha baiskeli, hapa palikuwa nafuu nikawa napiga kazi nyingi kwa baiskeli. Kusaga ikawa jambo nafuu, kuchota maji ikawa kazi yangu(watoto wao wanafanya kwa hiari, jla mimi ni shurti na siwezi kukataa)
Baada ya wao kuona napiga kazi vizuri wakaamua kunipeleka/kuniandikisha shule nikiwa umri ushaenda (10yrs) ingawa kwa kijijini ilikuwa kawaida. Mimi pia nilikuwa nataka shule nikafurahi bila hiyana, kwa umri huo tulikuwa wanafunzi wengi tukaenda kuanzishwa darasa la pili. Hapa kwenye kunipeleka shule walicheza kama The late Pele maana kwa miaka kadhaa hadi nimalize la saba lazima wanifaidi katika kazi, na kweli walinifaidi maana nilikuwa mtiifu sana.
Kuhusu sare za shule na daftari nilikuwa najinunulia mwenyewe kupitia kufanga vibarua vya kulima hasa msimu wa kulima, mara nyingine wao wananipa kibarua kwenye shamba lao napiga kazi wananipa hela naenda kununulia daftari, nikiwa shule endapo daftari ikiisha labda ya somo la hisabati nikiomba hela nitaambiwa kachanganye kuandika, yaani nikaandikie kwenye daftari ama la kiswahili au sayansi. Kwa hali hii nikawa nikipata hela naitunza ili ije inisaidie kununua daftari. Wakati mimi napambana na hali hii ila watoto wao hela zao wakipata kwenye vibarua wanaenda kununulia soda, biskuti, pipi hadi zinaisha maana madaftari yakiisha tu wananunuliwa mengine.
Kwenye msosi ikawa ni mwendo wa kupunjwa kama ni maziwa mimi nitaambulia nusu kikombe wengine wanapata kikombe full halafu mimi ndio kinara wa kwenda kuchunga, watoto wao wanaona hiyo hali ila hawasemi, mara nyingine uncle anajishtukia ananiongezea kutoka kwenye maziwa yake na endapo mkewe akiwa karibu na akiona anachukia kiaina. kitendo cha kupunjwa kila mtu aliyewahi kuishi pale asiye mtoto wao alikipitia. Pia unaweza kupewa mboga zilizoisha muda wa matumizi yaani mboga ya juzi unaweza kuipewa leo uitumie na usiweze kusema kitu, unaishia kugusa na kula tonge kavu kavu.
Ikiwa sijaenda kuchunga halafu ni weekend huwa tunafua nguo za shule, mimi nitaambiwa fua nguo zote hadi za wanawe hata kama wapo na hawana kazi maana suala la kufua wanamuachia mama yao na yeye ananipa huo msala. mara nyingine nilikuwa napewa nguo za mume wake naambiwa zifue, kama hamna maji hapo nyumbani naambiwa nenda kafulie mtoni.
Wakati wa kulima mimi nitaaamshwa alfajiri saa kumi na moja ila watoto wao wanaamka muda wowote wakipenda na mara nyingine wakisema hawaendi kulima waachwa, mimi siwezi kufanya hivyo maana mziki wake si wa kitoto nitakaoupata kuanzia kuchezea stick hadi kunyimwa msosi(binafsi sikufikia level ya kunyimwa msosi ila wapo waliowahi kunyimwa), stick ndio nimezichezea sana pamoja na kutukanwa kwa kosa dogo tu.
Life langu la primary likawa hivyo hadi nikamaliza la saba na sasa nishasahau hizo tabu zote na kupitia wao ndio inekuwa chachu ya kubadili maisha ya kwetu niliyoyakimbia enzi hizo ingali ni mdogo na endapo nisingekimbia sijui kama ningekuwa hapa nilipo sasa, hata kama ningekuwa hapa sasa labda sijui ningepitia njia gani maana mlango wa kutokea ulikuwa mgumu sana.
Jambo zuri walilokuwa nao hawa walezi walikuwa na exposure ya elimu japo kunipigisha kwata za kazi ila walikuwa wanafurahia maendeleo yangu mazuri kwenye masomo na walikuwa wanajidai mtaani kuhusu hasa wakiwa wanaambiwa sifa zangu na juhudi shuleni.
Nawapa MAUA yao hawa walezi walinitoa jalalani kama yule Prof wa awamu iliyopita.