Bora nyie mlinyanyaswa na mashemeji zenu...
Miaka fulani ya nyuma nilimtembelea ndugu yangu maana alikuwa analalamika sifiki kwake.
Nikapewa chumba nyumba ndogo ya nje ambayo alikuwa anakaa bro na mke wake ila chumb changu kinajitegemea tofauti kabisa na jamaa, hata choo nilikuwa namtumia cha nje ila jamaa kwake ilikuwa ni master bedroom.
Sasa huo usiku mkojo umenibana, ile natok nje tu nakutana na 2 grown Dobermanns with cropped ears na mwingine hadi mkia amekatwa[emoji15][emoji15]. I was like hee kumbe humu ndani kuna mbwa tena wakubwa hivi na hawaniambii hawa si wauwaji kabisa kwa kweli sikupenda[emoji1787][emoji1787]. Ikabidi nirud geto, nikampigia simu bro akaja akawashika mbwa nikaenda msalani.
Ilikuwa kero maana karibia kila siku nampigia jamaa anisindikize chooni kama mtoto mpaka jau, jamaa akanipanga hawana shida hao wakishakuzoea. Kesho yake nikawa nipo nao karibu tunacheza nao mixa wanapewa maelekezo wanizoee, yule mmoja alinirukia yani over nilitupiwa kakiroba cha kilo 50!! Nilipata ka upenyo nilijikuta nasepa ka upepo, yule mbwa anakuja nyuma ananikimbiza, anadhani tunacheza kumbe mwenzie ndio nasevu hivo[emoji1787][emoji1787]. Ilifika wakati ikifika kuanzia saa 9 au kumi sinywi maji mpaka kesho yake!
Sasa huo usiku nataka kwenda chooni kama kawaida, ile nafungua mlango tu yakanyanyuka masikio yamewasimama kama antenna yani kama washajiandaa kwa kitu fulani so alerted, nikasema hapana nikarud ndani pigia sana bro simu haipatikani. Mkojo unazidi kubana na ndani hakuna hata chupa. Nikachungulia tena nikawaona wako mbali kidogo nikachomoka kama mkuki mpaka chooni, yalikuja kwa kasi yakaanza kuparua mlango. Wakat nataka nirudi nkayaona yamesimama kwa mbali kidogo yapo serious sio mchezo, nikayachekiii nikaanza kuambaa ambaa na fence kuutafuta mlango wa geto, nayo yakaanza ku move kunifata. Nikajisemea hapana hii sio ishara nzuri nikarudi mbio mpaka chooni, majamaa yakaja speed mpaka pale mlangoni yanaunguruma mixa kuparua mlango.Nilienda na simu chooni, piga sana simu ya jamaa haipatikani nikajisemea leo nimeisha[emoji16]. Nikavuta ndoo ya chooni nikakaa kuanzia saa 9 hivi kuelekea 10mpaka 12 hadi nikapitiwa na usingizi na ile baridi sio poa. Nashukuru Mungu choo kilikuwa kisafi.
.......hapo sijaelezea tukio lengine la kukimbizwa na hao mbwa kidogo ning'atwe hawakuwa wamefungwa vizuri plus kukojoa mlangoni.....
Asubuhi baada ya kuyafungia namimi ndio nikajifanya natoka chooni, yule mzee akaniuliza umeingia chooni saa ngap sijakuona?! I was pissed off sikutaka hata kumwambia yaliyonikuta maana mjadala ungekuwa mrefu na sikuwa n huo mda wa kuanza kuoneana huruma, kwanza nausingiz/kichwa kinauma na hapo nafikiria kama naweza pata bus la saa mbili au la[emoji1787]. Jioni yake nikaaga kesho narud kwetu, mzee akamaind sana akapiga simu nyumbani sikubadili maamuzi. Kesho yake asubuhi nikasepa!
Zile siku chache nilizokaa pale ndani zilikuwa ni mateso, wale mbwa walinikosesha raha kabisa hasa usiku. Maana mda wote ilibidi niangalie huku na huku nijue wako wapi kabla sijafanya movement kama vile navuka barabara maana wana eneo kubwa. Na hadi leo sijawahi kwenda tena!
Japo niliwapendea ile tough and aggressive looking yao lakini haiondoi ukweli kwamba mimi na mbwa bado haziivi kivileee.
View attachment 2693982